in

CHAN fainali ya mnyonge na mbabe

HATIMAYE mashindano ya CHAN yanatarajiwa kufika tamati baada ya kushuhudia miamba miwili kutoka Dar Es Salaam na Nairobi kutinga hatua ya fainali. Mashindano hayao yalikuwa yakichezwa kwenye vituo vinne; Dar Es Salaam (Tanzania), Zanzibar (Tanzania), Kampala (Uganda), na Nairobi (Kenya) ambapo wenyeji wote walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kushuhudia miamba ya soka kama Algeria, Burkina faso na Afrika kusini zikitupwa nje ya mashindano hayo. TANZANIASPORTS inakuleta uchambuzi yakinifu kuhusiana na mchezo wa fainali utakavyokuwa.

Wababe wa Nairobi na Dar Es Salaam

Fainali ya CHAN mwaka huu inawakutanisha timu mbili zenye historia zinaofanana. Morocco walichapwa bao 1-0 na wenyeji Kenya katika mchezo wa hatua ya makundi kwenye dimba la Moi Kasarani. Madagascar nao walizabwa mabao 2-1 na wenyeji wenza Tanzania kwenye dimba  Benjamin Mkapa. Madagascar inawakilisha kundi lililopangiwa kucheza mechi zao katika dimba la Benjamin Mkapa, huku Morocco ikiwakilisha kundi la Nairobi.

Washindi wa pili katika fainali

Tanzania Sports
Madagascar

Madagascar haikutabiriwa kumaliza nafasi ya pili mbele ya Burkina Faso, Mauritania na Tanzania. Lakini ilishuhudiwa nchi hiyo licha ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tanzania ilifanikiwa kusonga mbele hadi mchezo wa fainali. Katika kundi lake Madagascar ilimaliza nafasi ya pili nyuma ya wenyeji Tanzania. Hali kadhalika Morocco walimaliza nafasi ya pili nyuma ya wenyeji Kenya. Hivyo basi hii ni fainali inayozikutanisha timu zilizoshika nafasi ya pili na zile zilizomaliza vinara kwenye makundi yao zimeshindwa kufua dafu.

Je, Morocco na Madagascar zina taswira gani katika fainali?

Morocco ni wababe wa soka kuanzia ngazi ya klabu hata timu ya Taifa. Kwenye mashindano ya Kimtaifa Morocco inashikilia rekodi ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 2022 nchini Qatar. Katika mashindano ya vilabu Morocco imekuwa tishio na ligi yake imeshuhudia miamba kama Raj Casblanca, Wydad Casablanca, RS Berkane na nyinginezo zikitamba kwenye mashindano ya CAF. Lakini upande wa Madagascar klabu zao hazifui dafu kwenye mashindano ya CAF na hivyo kuwa wanyonge zaidi. Morocco wana sifa zote za kuwa wababe kutokana na viwnago vyao vya soka. Madagascar wametinga fainali hii baada ya mashindano yaliyopita kuishia hatua ya nusu fainali, kwahiyo ni mafanikio makubwa kwao.

Mbinu za kiufundi

Timu zote mbili zinapendelea kupiga pasi fupi fupi na kupanga mipango yao kwa mfumo rasmi. Katika mchezo dhidi ya Senegal tuliona Morocco ikihaha kusaka bao kutokana na mpinzani imara. Morocco walitumia zaidi mfumo wa 5-2-3 kila walipokuwa wanakibiliana wapinzani wao katika kulinda lango. Lakini walipokuwa wakishambulia watumia mfumo 3-4-2-1. Mfumo huu wa kushambuliaji unawapa nafasi ya kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza na kasi kubwa. Tofauti yao na Madagascar ni kwamba hawa wanyonge wanapenda kucheza soka la kitabuni. Kwa Madagascar wanafurahia kucheza soka la wazi, pasi fupi, kumiliki mpira kwa wingi, na kushambulia na kujilinda kwa pamoja. Kama ungechagua mfumo wao Madascar wanatumia ‘total football’ yaani kila mchezaji anawajibika kwenye ulinzi na ushambuliaji. 

Morocco wameongeza kasi, hiki kitu kinaweza kuwa mwiba kwa Madagascar. Kasi ya Morocco imegawanyika katika pande mbili; kuna mipira mirefu inayopigwa kutoka upande wa kulia kwenda langoni mwa adui, pili wanacheza kwa pasi haraka na kasi kubwa kutoka nyuma kwenda eneo la 18 za adui. Kisha akifika eneo la 18 hatua ya kwanza ni kubadilisha muundo na kuanza kupigiana pasi fupi za haraka na kutengeneza nafasi za kufunga. 

Mtindo huu ulitumika dhidi ya Tanzania baada ya benchi la ufundi kumtoa kiungo mkabaji Yusuf Kagoma na kulifanya eneo la kiungo kulegezwa zaidi kwani hapakuwa na uwiano kati ya ulinzi na kushambulia.

Katika mifumo ya uchezaji, mbinu binafsi za Morocco zimeifanya nchi hiyo kuwa bora zaidi. Madagascar wanategemea zaidi uchezaji wa pamoja kwedna kushambulia na kurudi nyuma, lakini hawana kasi kama ya Morocco. Hata hivyo hii inakwenda kuwa fainali ya aina yake na huyu mnyonge akidharauliwa ndipo huonesha makucha. Hata hivyo ni fainali ambayo Morocco inapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kiwango chao. Fainali haina mwenyewe, lakini anaweza kuwa yule anayeaminiwa kuwa na uzoefu, ushindani na mbinu imara.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Nyota wanaosaka klabu mpya msimu huu

Mikel Arteta bado anadaiwa na Arsene Wenger

Mikel Arteta ni ubingwa au kuondoka Arsenal