in

Chachu ya washabiki EPL

Mashabiki wa soka

Wakati Ligi Kuu ya England (EPL) ikikaribia kurejea kwa ajili ya kukamilisha mechi 92 zilizobaki msimu huu, kuna habari njema kwa washabiki na wachezaji kadhalika.

Baada ya hali ngmu wakati wa janga la virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, Covid-19 na kufikiri kwamba huenda ligi isingemalizika kwa namna kadhaa kama kufuta msimu au kutangaza bingwa kwa kumchukua aliyekuwa akiongoza ligi, imekuwa sivyo.

Ipo habari njema kwa sababu Bodi ya EPL imeweka mipango kuwaonesha washabiki katika skrini kubwa pale mabao yanapofungwa, ikiwa ni jitihada za kuwasilisha zile hisia za ushangiliaji kwenye viwanja ambavyo ni tupu, kwani bado kuna ulazima wa watu kukaa kwa kujitenga kiasi.

Washabiki watakaokuwa wakifuatilia mechi kwa kuzitazama kutoka majumbani mwao wataunganishwa na viwanja vya timu zao kwa ajili ya kuweka hali nzuri ya ‘hewa’ kwa wadau – wachezaji wakiona kwamba wapo na washabiki wao ambao watakuwa wanashangilia.

Mpango huo umepewa jina la ‘mrejesho mubashara kutoka sebuleni’ na umeshatumiwa na Ligi Kuu ya Denmark kwa ajili ya kuwaunganisha wachezaji na washabiki wao kupitia mfumo wa makutano ya video – Zoom – kuhakikisha kwamba washabiki wanabaki mchezoni hata kama wapo majumbani mwao.

Mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa watendaji wa EPL na yakakubaliwa. Undani wa jinsi mambo yatakavyokuwa bado kutolewa, lakini vyanzo vya habari vinasisitiza kwamba kila kitu kitakuwa wazi karibia na Juni 17 ambayo ni tarehe ya kurejea kwa ligi hiyo viwanjani kama njia ya kufidia watazamaji kutoruhusiwa viwanjani.

Pamoja na kuleta mfumo huo wa kuunganisha wachezaji na timu zao, klabu zitaruhusiwa kutundika kwa wingi bendera kwa rangi watakazotaka zitakazochukuliwa picha kwa ajili ya kurushwa kwenye televisheni na kuanzisha ule mzuka wa soka.

Kadhalika zitakuwa zikirushwa ujumbe kutoka kwa Bodi ya EPL, lengo likiwa ni kuunga mkono Idara ya Taifa ya Afya na wafanyakazi wake kutokana na jinsi walivyojituma, wakiwa mstari wa mbele kwenye kupambana na Covid-19 bila kujali kuambukizwa na wagonjwa waliokuwa wengi.

Kelele za washabiki hazitakuwa moja kwa moja uwanjani bali watakuwa na fursa ya kubofya kitufe Fulani chekndu kwa ajili ya washabiki watakaokuwa wakifuatilia mechi kutoka majumbani mwao.

Kikao hicho kilikubaliana kwamba kwa mechi 92 zilizobaki kila timu itaruhusiwa kuingiza hadi wachezaji watano wa akiba, ili kuwapa upana wa kikosi baada ya athari za Covid-19 ambapo bado wachezaji hawakupata muda wa kutosha wa kawaida wa mazoezi na kuwa timamu.

Alikuwa ni Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck aliyetoa pendekezo hilo, akalipamba na kutoa ushawishi mzito. Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Peter Moore aliunga mkono mara moja lakini Makamu Mwenyekiti wa West Ham, Karren Brady alikataa, akidai kwamba hilo litafaidisha klabu kubwa tu kwa sababu wana vikosi vipana.

Basi ikabidi wapige kura, ambapo klabu 16 zilikubaliana na uamuzi huo, huku nne zikipinga nazo ni West Ham, Norwich, Sheffield United na Bournemouth. Miongoni mwa mechi zilizobaki, vituo vya televisheni vya Amazon na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kila kimoja kimepewa mechi nne kwa ajili ya kuonesha.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

73 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Lilian thuram

LILIAN THURAM:

Dar Young Aricans

CHAMA amekuja kuua “UFALME” wa NIYONZIMA!