in , , ,

Carragher na kashfa ya kutema mate

MCHAMBUZi wa soka kwenye televisheni, Jamie Carragher ameingia kwenye
kashfa nzito kwa kumtemea mate shabiki wa Manchester United.
Alifanya kitendo hicho akiwa kwenye gari yake, baada ya timu yake ya
zamani, Liverpool kufungwa 2-1 na Man U.

Kitendo cha mchambuzi huyo kimemgharimu, kwani amesimamishwa kazi na
Sky Sports kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu.

Alitema mate kumwelekea msichana mwenye umri wa miaka 14, baada ya
ubishani wa muda mfupi baina ya Carragher na baba wa huyo juu ya
matokeo ya mechi husika.

Tangu ajiunge na Sky Sports 2013 baada ya kustaafu soka, Carragher
ametokea kuwa maarufu miongoni mwa watazamaji wa televisheni kutokana
na aina yake ya uchambuzi wa soka.

Lakini sasa kazi yake mpya baada ya soka inaelekea kuwa katika kingamo
la kupotea, kwa kuwa waajiri wake wanatafakari upya juu ya nafasi ya
mchambuzi huyo.

Mlinzi huyo wa zamani wa Liverpool alikuwa ashiriki kwenye uchambuzi
wakati wa mechi baina ya Manchester City na Stoke Jumatatu hii jioni,
lakini alizuiwa huku miito ikitolewa kumtaka ajiuzulu moja kwa moja.

Carragher ameeleza kujutia kwake tukio hilo ambalo wapita njia
walilirekodi kisha kurusha kwenye mitandao mbalimbali ya jamii na
waajiri wake wakaona na kumchukulia hatua.

Carragher alieleza kwamba alichofanya ni kosa baya zaidi katika
kipindi chake cha kazi ya miaka 25 – uchezaji na uchambuzi wa soka,
akisema mbele ya umma imeonesha picha mbaya.

Clip husika inaonesha gari ikitokea upande wa pili wa lile la
Carragher baada ya mechi hiyo, akafungua kioo, jamaa kwenye gari ya
pili akamtania juu ya matokeo ambayo timu yake ya zamani ilifungwa,
ndipo akatema mate uelekeo wa gari ile na mtoto huyo wa kike
akalalamika kuwa mate hayo yamempata.

Msemaji wa Sky Sports alisema kwamba shirika lake linachukulia kwa
umakini mkubwa suala hilo, linalaani kitendo cha Carragher na kwamba
wamemweleza binafsi juu ya hilo na kumsimamisha kazi.

Carragher (40) atakuwa nje ya kazi wakati hatima yake ikitafakariwa na
wakuu. Amekuwa pia akiandika makala kwenye gazeti la Telegraph ambao
hawajasema lolote juu ya kitendo chake hicho.

Amechezea Timu ya Taifa ya England mechi 38 na anasema kwamba hakujua
iwapo binti huyo alikuwa kwenye gari alipotema mate uelekeo huo na
kwamba anasikitika na atazungumza na familia hiyo kuwaomba radhi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Mkapa Stadium

TUNASHINDWA KUUFANYA UWANJA WA TAIFA KAMA SEHEMU YA UTALII?

Tanzania Sports

THAMANI YA KIKOSI CHA 1.3B SIMBA ITAONEKANA HAPA