in , , , ,

Buriani Jimmy Hill, utakumbukwa daima

*Alikuwa mchezaji, kocha na mtangazaji

*Alitamba kipindi cha ‘Match of the Day’

Mmoja wa watu muhimu katika soka ya England, Jimmy Hill ameaga dunia
akiwa na umri wamiaka 87, kutokana na maradhi ya Alzheimer
yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na matatizo ya akili na
kuchanganyikiwa.

Hill ametumikia karibu kila jukumu kwenye soka, akianza kwa kuchezea
klabu za Brentford na Fulham katika kipindi cha miaka 12 alichodumu
katika uchezaji. Baada ya hapo hakupoteza muda, bali aligeukia kwenye
ukocha.

Ameelezewa na wengi kuwa mtumishi kuliko kiongozi, kutokana na jinsi
alivyokuwa akitekeleza majukumu yake, ikiwa ni pamoja na ukocha,
uenyekiti wa klabu lakini pia Mwenyekiti wa Chama cha Wanasoka wa
Kulipwa (PFA).

Ni wakati akiwa kwenye wajibu huo, aliwasha moto na kuendeleza kampeni
yake ya kufuta upeo wa mishahara kwa wanasoka wa kulipwa.

Lakini huenda anatambuliwa na atakumbukwa zaidi kwa kazi ya uchambuzi
mubashara wa soka katika kipindi maarufu cha Match of the Day, yeye
akiwa ndiye mwenyeji wa wachambuzi, kazi aliyoianza 1989 na kusimamia
vipindi zaidi ya 600.

Hill aligundulika kuwa na ugongwa huo wa Alzheimer mwaka 2008, na kwa
miaka mitatu iliyopita alikuwa akiishi kwenye nyumba zitoazo huduma
kwa wazee wenye matatizo kiafya.

Wakala wa Hill, Jane Morgan alisema hivi kwenye taarifa yake: “Kwa
masikitiko makubwa Bryony Hill (mkewe) na watoto wa Jimmy Hill
wametangaza kwamba Jimmy ameaga dunia kwa amani leo akiwa na umri wa
miaka 87 baada ya vita ya muda mrefu dhidi ya ugongwa wa Alzheimer.
Bryony alikuwa kando yake wakati mauti yanamkuta.”

Jimmy Hill, wakati wa uhai wake
Jimmy Hill, wakati wa uhai wake

Atafanyiwa maziko ya faragha, lakini siku ya Mwaka Mpya, marafiki na
wale aliopata kuwa nao kwa namna moja au nyingine watafanya ibada ya
pamoja, wakala huyo amesema.

Hill alichukuliwa na wengi kuwa mmoja wa wahambuzi mahiri kabisa wa
mchezo wa soka kwa jinsi alivyowezea fani hiyo, akiijua nje ndani,
tangu uchezaji, ukocha, urefarii kwa kufuzu kozi, uongozi na hatimaye
kwenye kuuchamba mchezo kinadharia.

Kimsingi amekuwa hewani akifanya kazi katika mashindano yote makubwa
kwenye muda wake wa kazi kwa kiasi kisichomithilika. Alikuwa mkuu wa
michezo ITV 1967 kisha akaenda BBC miaka sita baadaye alipoanza
utangazaji wa Match of the Day.

Hill alizaliwa Balham jijini London mwaka 1928, ambapo akiwa kijana
alipata kufanya kazi ya kusafisha madohani huku akikamilisha uhudumu
kwenye jeshi kwa hatua zilizotakiwa za awali kabla ya kuanza kucheza
Brentford alikokipiga mechi 87 kisha akahamia Fulham 1952.

Alitumia muda wake mwingi wa uchezaji Fulham kwani alicheza mechi 276
akiwa mshambuliaji aliyewafungia Cottagers mabao 41 ya ligi kabla ya
kustaafu akiwa na umri wa miaka 33 mnamo mwaka 1961.

 Hill, in his role as the chairman of the Professional Footballers’ Association, successfully campaigned to have the maximum wage abolished in 1961. Here he shakes hands with Joe Richards, the president of the Football League, after attending a successful meeting to discuss players’ wages.

Hill, in his role as the chairman of the Professional Footballers’ Association, successfully campaigned to have the maximum wage abolished in 1961. Here he shakes hands with Joe Richards, the president of the Football League, after attending a successful meeting to discuss players’ wages.

Mwaka huo huo alianza kazi ya ukocha Coventry alikokaa kwa miaka sita
na kuwachangamsha hivyo kwamba ushawishi wake ulifanya klabu wakapewa
jina jipya la utani – The Sky Blue Revolution.

Hill alirudi Coventry na kuwa mkurugenzi mtendaji 1975 na baadaye kuwa
mwenyekiti wa klabu hiyo, akawasimamia vyema na kuwanusuru kushuka
daraja, badala yake Sunderland ndio wakazama.

Huyu ni mtu anayeheshimiwa na umma wa wanasoka na anajulikana sana.
Septemba 16, 1972, wakati Arsenal wakiwa wenyeji wa Liverpool uwanjani
Highbury, mshika kibendera Dennis Drewitt alishikwa na msuli na
kushindwa kuendelea na kazi, na kwa mujibu wa kanuni za FA, mchezo
ilikuwa uahirishwe.

Hata hivyo, mtangazaji alitaka yeyeote ambaye amefuzu kwa kozi za
uamuzi ajitokeze kuokoa jahazi, ndipo Hill aliyekuwa uwanjani hapo
kama shabiki akabeba jukumu hilo hadi mwisho wa mchezo.

Hill ameoa mara tatu; akapata watoto watatu kwa mke wake wa kwanza,
Gloria na wawili kwa mkewe wa pili, Heather. Alipogunduliwa kuwa na
maradhi hayo, wanawe wa mke wa pili walieleza kwamba hawakuwa na
jukumu la kuamua juu ya huduma zake, kwani alikasimu mamlaka yake ya
kisheria kwa mkewe wa tatu, Bryony na wakili wake.

Mwanamichezo huyu pia alikuwa rais wa timu ndogo ya Corinthian Casuals
na alikuwa akiishi Hurstpierpoint, West Sussex. Mwenyezi Mungu ailaze
roho yake mahali pema peponi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Hiddink atua Chelsea

Tanzania Sports

Chelsea sasa ushindi