Mwanamageuzi Man United

Tangu kuingia kwa Mreno Bruno Ferndnandes kwenye kikosi cha Manchester United, pamekuwapo mapinduzi makubwa namna wanavyocheza na hakika ametia nguvu na kasi mpya.

Jamaa huyu alitabiriwa makubwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer, na kweli akaanza kwa kasi japokuwa ni kwa bahati mbaya kwamba bada ya mechi chache Ligi Kuu ya England (EPL) kama ligi nyingine mbalimbali imesimama kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Fernandes anaonesha kuwa na kipaji cha uchezaji mahiri lakini pia uongozi, akiwapanga vyema wenzake dimbani lakini pia katika vyumba vya kubadili nguo, mageuzi haya yakiwagusa wadau wengi wa Old Traffors kiasi cha kumrejea kama ‘Portuguese Magnifico’.

Ametumia muda mfupi sana kuzoea Man U na wachezaji wenzake, akitokea kuwa shujaa na hata alihusika kwa kiasi kikubwa kumnyamazisha Pep Guardiola – kocha wa Manchester City, kwani mechi yao utani wa jadi kwa jiji la Manchester, United waliibuka na ushindi mzuri bila kutarajiwa.

Kiungo huyu amethibitisha kwamba haikuwa makosa kwa United kuwalipa Sporting Lisbon pauni milioni 47 kwenye dirisha dogo la usajili la Januari mwaka huu. Tangu awasili na kuanza kuchezwa, United hawajapoteza mchezo wowote.

Anaelezwa sasa kama mchezaji bora zaidi kupata kusajiliwa tangu kustaafu kwa kocha Sir Alex Ferguson mwaka 2013. Amecheza mechi tisa, akisababisha mabadiliko makubwa uwanjani na kuwafaidia Man U, mambo ambayo wachezaji waliomtangulia hapo – kama Radamel Falcao, Angel di Maria na Alexis Sanchez walishindwa kufanya na kila mmoja akaondoka baada ya muda mfupi kwa wakati wake.

Kusimamishwa ghafla kwa ligi kutokana na COVID-19 ambako hakukuwa kumetarahiwa, kwa namna moja au nyingine kumempunguza kasi yake, na kwa baadhi ya wachezaji huwezekana wakashindwa kurudi na makali yale yale waliokuwa wakienda nayo kabla.

Ferdnandes (25, ambaye jina kamili ni Bruno Miguel Borges Fernandes yupo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa Ureno, akiwa pia amechezea klabu za Novara, Udinese, Sampordia na Sporting alikotoka Januari mwaka huu, akikubalika sana kwenye kiungo na akitumia vyema urefu na nguvu zake.

Washabiki wa United walishindwa kujizuia na tayari wameshaweka kawimbo na kulitaja jina lake kwa upekee. “Bruno, Bruno, Bruno, anatoka Sporting Lisbon kama Cristiano. Aenda kushoto, aenda kulia, awzifanya ngome za adui kuonekana takataka. Huyu ndiye ‘Portuguese Magnifico’ wetu.

Mawimbi yake, kama ingekuwa sawa kuita hivyo mambo yake adimu uwanjani, yanawapelekesha hasa washabiki na kocha Solskjaer anafurahia mno hali hiyo. Januari ulikuwa mwezi mgumu, ambapo United walichezea vichapo viwili mfululizo kutoka kwa Liverpool na Burnley, kiasi cha kuzusha tena maswali juu ya iwapo Solskjaer anafaa kusgika nafasi hiyo.

Jamaa alikuja na kumwokoa kwenye sintofahamu, Mnorway huyo akaanza tena kutembea kifua mbele na macho juu tangu Januari 27. Ferndandes amepata tuzo ya uchezaji bora wa mwaka mara mbili huko kwao na pia kutwaa Kombe la Ligi na la Ligi Kuu.

Huko Ureno alikuwa mchezaji mahiri kwa misimu hiyo miwili, akifunga mabao 39 na kutoa usaidizi kwa mengine 28. Hakuna mchezaji mwingine huko aliyehusika na mabao mengi kiasi hicho – na akitengeneza nafasi 239, zikiwa ni 25 zaidi ya yule anayemfuata – Alex Telles wa Porto.

Tangu mwanzoni mwa Februari hadi ligi iliposimama, United wameshinda mechi sita, kwenda sare tatu, kufunga mabao 22 na kuruhusu nyasi zao kutikiswa mara mbili tu huku wakitoka uwanjani bila bao kuingia kwao mara saba. Ni wakati huo waliweza kupunguza pengo kati yao na Chelsea wanaoshika nafasi ya nne kwa tofauti ya alama tatu. Walisonga mbele kwenye Kombe la FA na pia katika 16 bora za Ligi ya Europa.

Ferndandes mwenyewe alihusika katika mabao matano kwenye ligi – akifunga mawili na kutoa asisti tatu. Hakuna mchezaji kwenye EPL aliyehusika kwa idadi kubwa hivyo ya mabao kwa wakati huo. Kwa uwezo wake, kadhalika, ameshinda tuzo ya uchezaji bora wa mwezi katika EPL.

“Ameingia (Man United) na kuzoea haraka kwa uzuri sana. Historia inaonesha kwamba ni ngumu kuingiza wachezaji wapya kutoka ligi nyingine Januari na wao kuzoea haraka. Huyu amekuwa tofauti kabisa,” anasema mmoja wa wanajopo la ukocha wa Man United, Michael Carrick.

Anaonekana kwamba ana uwezo wa kucheza vyema kama Roy Keane kwenye kiungo, ana maono na uwezo wa pasi za uhakika kama Paul Scholes, lakini anaigusa mipira mithili ya Eric Cantona. Nahodha Harry Maguire wa Man United anasema kwamba Fernandes ni mtu mwenye haiba ya hali ya juu, akizungukwa na hali njema sana.

Mshambuliaji wa zamani wa United, Dimitar Berbatov, anasema kwamba klabu yake hiyo ya zamani imebadilika kabisa ikiwa na kijana huyo, anayejituma sana kwenye mazoezi na kupigania timu yake ipate ushindi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Nyakati ngumu kwa soka

Tanzania Sports

Kichuya, Muzamiru na Mo-Ibrahim, nidhamu ilivyowaua