Baraza la michezo la taifa hapa nchini Tanzania BMT kesho kutwa litakutana na viongozi na wadau wa chama cha mchezo wa mpira wa mikono TAHA ili kupanga mikakati ya uchaguzi wa chama hicho.
Kaimu katibu mkuu wa baraza hilo, Mohamed Kiganja amesema mkutano huo utatoa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao ulitakiwa kufanyika wiki iliyopita na kuhairishwa kutokana na kujitokeza kwa wagombea wachache katika kuwania nafasi za uchaguzi huo.
Aidha Kiganja amesema kumekuwepo na mwamko kwa wagombea na tayari jumla ya wagombea Kumi na sita
wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho.
Hapo awali BMT ilisogeza mbele uchaguzi huo baada watu waliojitokeza kugombea nafasi kwenye chama hicho kutotimia huku baadhi ya nafasi zikikosa wagombea na sasa BMT inasema wagombea wamefikia idadi inayofa na ndio maana watajadili lini uchaguzi huo ufanyike.
Mikoa ambayo ni wanachama wa chama hicho ni mikoa miwili na vilabu ambapo wanachama wa chama hicho watakutana kuangalia suala la kuongeza idadi ya wanachama wa kupiga kura katika chama hicho.
Comments
Loading…