Nilikuwa nawaangalia Manchester United wikiendi iliyopita kwenye mchezo wao wa mashindano ya FA dhidi ya Fulham. Katika mchezo huo Fulham walitangulia kupata bao, na kuwalazimisha Man United kusaka bao la kusawazisha kwa muda mrefu. Hata baada ya kupata goli la kusawazisha Man United wlaiendelea kucheza vizuri na kujaribu kufanya mashambulizi ya kuongeza la pili. Hata hivyo haikuwa siku yao, na walipoteza nafasi mbili za penati na hivyo kutolewa kwenye mashindano ya FA. Katika makala haya nachambua masuala kadhaa ambayo timu hii na mashabiki wake wanapaswa kujua.
Nguvu na kasi havifanani
Adama Traore anajulikana kuwa mchezaji mwenye nguvu za mwili na kasi. Alivyokuwa Barcelona na alivyo sasa ni tofauti. Ni mchezaji mwenye nguvu za mwili na kasi yake huwa inatisha. hata hivyo kikosi cha Man United kinakosa nguvu za mwili. Mara kadhaa wachezaji wa Fulham walikuwa wanatumia mabavu kushindana na Man United. Kila lilipofika suala la matumizi ya nguvu ilikuwa vigumu kudhani Fulham wangekuwa imara kuliko klabu kubwa kama Man United.
Kwa wachezaji wengi wa Man United wanatakiwa kuimarishwa kwenye nguvu za mwili, ingawaje kocha wao Ruben Amorim si muumini wa hilo. Wachezaji wake wanapaswa kuongezewa nguvu ili kukabiliana na Ligi yenye kila aina ya matumizi ya nguvu za miili kuliko masuala ya ufundi. Kwa Man United yake kupambana na Newcastle United wenye ‘maguvu’ mengi mno ndani ya dimba. Mashabiki wa Old Traford walizoea mafanikio, kushindwa namna hii huku wachezaji wakiwa hawana utimamu wa kimwili ni kuwakosea heshima.
Hakuna ‘muuaji’, hakuna mshambuliaji
Kila timu inahitaji wachezaji ambao wanatumika kuamua matokeo pale timu inaposhindwa. Ufaransa walikuwa na Zinedine Zidane sawa na Real Madrid walivyokuwa na Cristiano Ronaldo, Barcelona wlaikuwa Lionel Messi na kadhalika. Kila timu inahitaji kuwa na wachezaji wale ambao wanamaliza mchezo pale hali inapokuwa ngumu. Ukikitazama kikosi cha Man United kinavyocheza, hali ya wachezaji wake haionekani kama yupo ambaye anaweza kumaliza mchezo na kuokoa jahazi la timu. Timu inahitaji wachezaji wote, lakini haikosekani kuwa mchezaji tegemeo.
Mchezaji ambaye anaweza kuifanya kazi ngumu kuwa rahisi na kuipa wepesi timu. Ruben Amorim hana mchezaji waina hii. Hata alipojaribu kumtengeneza Amad Diallo, majeruhi yamemnyang’anya. Jambo lingine hakuna muuaji pale mbale. Mshambuliaji ambaye anaweza kuwafanya mabeki wa timu pinzani watetemeke na kucheza kwa tahadhari.
Fikiria Man United wenyewe walikuwa na mabeki wakatili kama Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Patrice Evra walikuwa vyuma vyenye nguvu na ambavyo vilitetemesha washambuliaji. Sasa ukiangalia safu ya ushambuliaji inayopangwa na ile ya akiba, unaona wazi timu hiyo haina muuaji pale. Hakuna mshambuliaji mwenye uhakika wa kumpa mabao 20 kwa msimu mmoja. Hakuna kombinenga yenye faida kwake. Mshambuliaji chipukizi Obi ndiyo anaanza, anakua na anayo safari ndefu lakini si wa kutegemewa.
Eneo la kiungo mkabaji ushambuliaji
Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari ambazo zinadai kuwa kocha Ruben Amorim anatarajiwa kuwaondoa wachezaji wengi kikosini. Hata hivyo anayo faida kwenye eneo la kiungo mkabaji yupo Carlos Casemiro ambaye jua linaelekea kumchwea, lakini changamoto ya ubovu wa timu inamfanya awe mbovu. Kwahiyo Man United wanahitajika kuwa na kiungo mkabaji ambaye anaweza kuongeza maarifa zaidi kwenye kikosi chao ama ifanye kazi ya kumwimarisha Kobi mainoo ili awezeshwe kucheza eneo la kiungo mkabaji kama jukumu lake jipya.
Si hapo tu, uchezaji wa eneo la kiungo mshambuliaji nalo linahitaji kuimarishwa. Man United inaposhambulia huwa inakosa mtu wa kusimama nje ya 18 ambaye anaweza kuamuru shambulizi liende wapi ama akaachia fataki kuelekea lango la adui. Nje ya 18 wanapokuwa lango la adui, hata wakicheza pasi fupi fupi (one on one) bado wanakosa ule muono wa mbali ambao mchezaji anaweza kuona na kupenyeza akili zake hapo mbali ya mfumo wa kocha. Bruno Fernandes anahitaji kusaidiwa ama aimarishwe ili aondokane na hali ya kuwa legelege.
Makosa mengi
Yapo makosa mengi katika timu hii. Ni makosa yanayostaajabisha sana. Man United haifungwi kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kujilinda bali makosa binafsi ya wachezaji yanawagharimu mno. Mathalani penati mbili walizokosa zinatokana na ufundi mdogo wa wapigaji. Pia wawili hao walichaguliw asbabu hakuna wapigaji hodari wa penati. Ukiacha hilo suala la timu kufanya makosa yanayojirudia mara kwa mara ni tatizo lingine linawafanya waonekane ‘wachovu’. Dirisa lijalo la usajili Man United wanatakiw akufanya mambo mengi makubwa kwa maslahi ya timu yao kabla jahazi halijazama. Ni timu inahiyohitaji mambo mengi kwa wakati mmoja, hata kama watafukuza makocha, lazima wakiri timu yao haijawa imara wakati wowote.
Comments
Loading…