Waandaaji wa sherehe za ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia wameboronga kwa kupeperusha bendera ya Niger badala ya Nigeria.
Katika sherehe za jioni ya Alhamisi jijini Sao Pailo, Brazil, ilipeperushwa bendera ya nchi ambayo haishiriki mashindano hayo.
Bendera ya Nigeria ina rangi tatu kwa michirizi ya kutoka juu kwenda chini ikiwa na rangi za nyeupe katikati na kijani kulia na kushoto, nembo ya taifa ikiwa katikati.
Bendera ya Niger, taifa la Afrika Magharibi pia kama Nigeria, ina michirizi ya mlalo, juu ikiwa rangi ya chungwa juu ya michirizi mweupe na kijani na ndiyo ilipeperushwa kimakosa.
Hizo ni nchi zinazopakana zikiwa na mpaka wa maili 450 zenye urafiki mkubwa lakini zinazongwa na machafuko ya hapa na pale.
Hata hivyo, wakati Nigeria inashika nafasi ya 44 kwa ubora wa viwango vya soka duniani, Niger ni ya 122.
Hii si mara ya kwanza bendera isiyotakiwa inapeperushwa kwenye sherehe za ufunguzi wa mashindano makubwa, kwani mwaka juzi kwenye ufunguzi wa michuano ya Olimpiki jijini London, ilipeperushwa bendera ya Korea Kusini ilipeperushwa wakati timu ya Korea Kaskazini, jirani na hasimu mkubwa, ikikaribia kuingia uwanjani.
Ilikuwa kwenye soka ya wanawake, na ilibidi mechi icheleweshwe wakatafute bendera sahihi na kuitundika kwenye mlingoti husika. Kutokana na uhasama uliopo baina ya mataifa hayo mawili, wachezaji walikataa kuingia uwanjani.
Comments
Loading…