Menu
in , , , ,

Bayern wamnyakua Diaz wa Liverpool

Bayern wamnyakua Diaz wa Liverpool

BAYERN Munich wa Ujerumani wamemsajili wing awa Liverpool Luis Diaz ambaye ametamba kuwa amekamilisha kazi huko kwa waajiri wake wa zamani.

Diaz aliyesema alitimiza vyema majukumu yake, amekamilisha uhamisho ambao umegharimu Pauni milioni 65.5.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kukaa Anfield kwa mud awa miaka mitatu unusu.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 aliachwa nje ya kikosi cha Liverpool katika mechi ya utangulizi wa msimu dhidi ya AC Milan Jumamosi iliyopita kwa sababu tayari kulikuwa na tetesi kwamba hatma yake haingekuwa klabuni hapo msimu ujao.

Baada ya kukataa dau la awali la Bayern lililosimama kwenye pauni milioni 58, Liverpool walikubali lililofuata na kumwachia mchezaji huyo bila matata, wakimruhusu mara moja kusonga mbele na vipimo vya afya yake.

Winga huyu anawaacha Wekundu hao amba oni mabingwa wa Ligi Kuu England, akiwa ameshinda nao makombe tofauti manne, akisema kuondoka kwake ingekuwa ni ‘kwaheri timilifu’ kama hakungetokea kifo cha mchezaji mwenzake hapo Liverpool, Diogo Jota mapema mwezi huu.

“Niliwasili nikiwa na ndoto nyingi duniani, na nandoka nikiwa najivunia kila kitu tulichoshinda Pamoja,” Diaz aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram.

“Nimekutana na watu wema isivyofikirika, washikaji poa sana na makocha walionisaidia mno, na pia nikawaona washabiki wa aina yake. Liverpool, kwa hakika ni timu isiyo ya kawaida, na nitamweka kila mmoja wao moyoni mwangu.

“Ni vyema kwamba naondoka nikiwa na hisia za kuwa nimetekeleza vyema wajibu wangu, na zaidi ya yote nikiwa naondoka wakiwa mabingwa. Ingekuwa ‘kwa heri timilifu’ kama si kumpoteza mmoja wetu (Jota) katika hali mbaya (ajali) vile.

“Nambeba kila mmoja moyoni mwangu, lakini kwa namna ya pekee ni mmoja wao: Diogo. Sitakaa nimsahau. Hatutamsahau abadan. Asanteni kwa yote,” alisema.

Diaz alijiunga na Liverpool akitoka Porto wa Ureno kwa mkataba wa awali wa Pauni milioni 37, akafunga mabao 41 katika mechi 148 katika kipindi alichohudumu hapo Anfield.

Alitwaa Pamoja nao Kombe la FA na EFL kwenye msimu wake wa kwanza, na alikuwa sehemu ya kikosi kilichopoteza mechi ya Real Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa 2022.

Alifurahia kipindi kizuri zaidi katika kazi yake ya soka msimu uliopita, ambapo alifunga mabao 17 katika mashindano yote. Kuondoka kwa winga huyo kunamaanisha kwamba Liverpool wameshatengeneza pauni milioni 115 kwa mauzo ya wachezaji kiangazi hiki.

Hiyo imesaidia mchango wa kwenye pauni milioni 270 kuwapata Florian Wirtz, Hugo Ekitike, Jeremie Frimpong na Milos Kerkez. Wekundu hao wamebaki wakimtamani mshambuliaji wa Newcastle, Alexander Isak ambaye hakusafiri na Magpies Kwenda Mashariki ya Mbali na alikuwa akitarajia kuondoka klabuni hapo.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version