in , ,

Arsenal wawakung’uta Bayern

 
Arsenal wamefufua matumaini yao kwenye hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baadaya kuwafunga Bayern Munich 2-0.

Wakicheza mbele ya maelfu ya washabiki wao katika dimba la Emirates Jumanne usiku, Washika Bunduki wa London walipata mabao yao kupitia kwa mshambuliaji wa kati, Olivier Giroud na kiungo Mesut Ozil.

Kocha Arsene Wenger alitangulia kusema kabla ya mchezo kwamba Bayern walikuwa na udhaifu kwenye baadhi ya maeneo, huku matumaini ya washabiki yakiwa yamepotea baada ya kukubali vichapo viwili kwenye mechi za mwanzo.

Haikuwa kazi rahisi, hata hivyo, kuwashinda Wajerumani hao wanaofundishwa na Pep Guardiola, na ilibidi Arsenal wasubiri hadi dakika ya 77 kupata bao la kuongoza lililotiwa kimiani na Giroud, baada ya kipa Manuel Neur kufanyia kosa mpira wa adhabu ndogo wa Santi Cazorla.

Advertisement
Advertisement

Bayern walitawala mpira kwa ujumla, lakini Arsenal walitumia mbinu kuhakikisha wanashinda, ambapo bao la pili lilifungwa na Ozil akiitendea haki majalo ya beki wa kulia, Hector Bellerin ambaye sasa amekuwa mzuri katika kupandisha mashambulizi.

Neur alijaribu tena kuuondoa mpira huo lakini waamuzi wakamaizi kwamba ulishavuka mstari mweupe na kuwa bao la pili lililoshangiliwa hasa na Arsenal. Kipa Petr Cech wa Arsenal alifanya kazi ya ziada, akiziba makosa yaliyofanywa awali na David Ospina kwenye mechi dhidi ya Olympiakos.

Arsenal walitakata hapo jana
Arsenal walitakata hapo jana

Aliokoa hatari mbili kubwa zaidi kutoka kwa Thiago Alcantara na Arturo Vidal. Arsenal bado wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi za marudiano, kwani wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi tatu sawa na Dinamo Zagreb, wakati Olympiakos wanazo sita sawa na Bayern Munich.

Katika matokeo mengine, BATE Bor walifungwa 2-0 na Barcelona, Bayern Leverkusen wakaenda sare ya 4-4 na Roma, Dynamo Kiev wakaenda suluhu na Chelsea, Fc Porto wakawafunga Maccabi Tel Aviv 2-0, Valencia wakashinda 2-1 dhidi ya KAA Gent na Zenit St Petersburg wakawafunga Lyon 3-1

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Pistorius atoka jela

Tanzania Sports

LIGI YA MABINGWA ULAYA: