*Man City wafyatua chelsea
*Aston Villa washuka daraja
Matumaini ya Arsenal kupunguza pengo kati yao na vinara wa ligi
Leicester yaliendelea kuyeyuka baada ya kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya
Crystal Palace dimbani Emirates.
Walishindwa kutumia fursa ya Leicester kwenda sare ya 2-2 na West Ham
hiyo hiyo Jumapili ili wapunguze pengo, lakini bao lao moja la kipindi
cha kwanza kupitia kwa Alexis Sanchez lilisawazishwa baadaye kabisa na
Yannick Bolasie.
Katika mechi ambayo Arsenal walitawala kwa raha zao, wangeshinda basi
wangewavuka Manchester City waliowapandia siku moja kabla kwa
kuwacharaza Chelsea 3-0. Wakati Leicester wamefikisha pointi 73,
Tottenham wanazo 65 huku Man City na Arsenal wakifikisha 60.
Katika mechi ya Leicester, mwamuzi Jonathan Moss alilaumiwa na baadhi
ya watu akionekana kuwabeba Leicester kwa kuwapa penati katika dakika
za lala salama za nyongeza. Mpachika mabao hatari wa vinara hao, Jamie
Vardy alilikoroga na kuoneshwa kadi nyekundu. Anadhaniwa ataongezewa
adhabu, kwani alionekana kama kumtolea mwamuzi maneno mshambuliaji wa
West Ham, Andy Carroll alitoa matamshi kwamba mwamuzi aliamua
kuwasawzishia mambo Leicester, na kauli yake hiyo inachunguzwa na FA,
ambapo huenda akatakiwa maelezo na hata kuadhibiwa. Kwenye mechi
nyingine Jumapili hii Liverpool walishinda 2-1 dhidi ya Bournemouth.
ASTON VILLA WASHUKA DARAJA
Jumamosi zilikuwapo mechi kadhaa, ambapo Manhester United walizamisha
jahazi la Aston Villa kwa kuwafunga 1-0 na sasa msimu ujao watakuwa
Ligi Daraja la Kwanza (Championships) wakibaki na pointi zao 16.
Man United waliofunga kupitia kwa chipukizi wao, Marcus Rashford,
wamefikisha pointi 56, wakionekana kukosa uendelevu hivyo kocha wao,
Louis van Gaal akionekana bado kuwa katika hatari ya kufutwa kazi
msimu ujao wa kiangazi. West Ham wanazo pointi 53 na huenda wakacheza
Ligi ya Europa kama hawatakaza kamba.
Matokeo mengine ni kwa Everton kwenda sare ya 1-1 na Southampton;
Newcastle kuwacharaza Swansea 3-0 katika hali ya kushangaza, lakini
inayomtia moyo kocha wao mpya, Rafa Benitez anayejaribu kuwanasua na
balaa la kushuka daraja.
West Bromwich Albion walipoteza 0-1 nyumbani walikowakaribisha
Watford. Baadaya Villa kushuka daraja, timu zilizobaki hatarini ni
Newcastle wenye pointi 28, Sunderland waliofikisha 30 naNorwich wenye
31. Tottenham Hotspur ni wageni wa Stoke Jumatatu hii.