in ,

Arsenal wameanza kama walivyomaliza msimu

Arsenal

Hakuna raha nyingine zaidi ya kuanza msimu kama ulivyomaliza uliopita. Ndivyo ilivyokuwa kwa kikosi cha MiKel Arteta ambaye alimaliza msimu wa 2019-2020 kwa kutwaa kombe la FA. Leo jumamosi amefungua pazi la msimu wa 2020-2021 kwa kutwaa taji la Ngao ya jamii baada ya kuwazaba mabingwa wa Ligi Kuu, Liverpool kwa njia ya mikwaju ya penati 5-4 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley.

Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang aliifungia timu yake bao la kuongoza baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Liverpool baada ya kupokea pasi maradadi kutoka kwa Nketiah.

Pierre alimzidi ujanja Marco Williams kabla ya kusogea eneo la hatari kupiga shuti kali lililomwacha hoi mlinda mlango wa Liverpool, Alisson Becker akiwa hana la kufanya. Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipomalizika, Arsenal walikuwa kifua mbele.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu, huku Liverpool wakitafuta bao la kusawazisha. Juhudi za Liverpool zilifamikiwa baada ya kufanya mabadiliko ambapo Takumi Minamino aliingia dimbani kuchukua nafasi ya Roberto Firmino.

Mabadiliko hayo yaliipa uhai Liverpool ambapo ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia Takumi Minamino kunako mdakika 72 ya mchezo. Mabao hayo yalidumu kwa dakika zote 90, hivyo mwamuzi kuamuru zipigwe penati kuamua mshindi wa mchezo huo.

Katika hatua ya mikwaju ya penati, Liverpool walitumbukiza mikwaju minne, baada ya mkwaju wa mchezaji chipukizi Rhian Brewster kugonga mtambaa panya na kutoka nje. Kwa upande wao Arsenal walifanikiwa kutumbukiza mikwaju yote mitano, ambapo mpigaji wa mwisho alikuwa  Peirre Emerik Aubameyang.

HESHIMA KWA ‘WAKANDA’

Aubameyang ameanza msimu kama alivyomaliza uliopita ambapo alikiongoza kikosi cha Arsenal kutwaa taji la FA akifunga mabao mawili muhimu dhidi ya vijana wa Frank Lampard, Chelsea.

Tanzania Sports
Mabingwa……

Baada ya kupachika bao la kwanza  kwa timu yake Aubameyang alishangilia kwa staili ya kutoa heshima ya ‘Wakanda forever’. Staili hiyo ni kutoa heshima kwa mwigizaji nyota wa filamu ya Black Panther, Chadwick Boseman ambaye amefariki duniahivi karibuni kutokana na ugonjwa wa saratani.

BAO LA KWANZA

Licha ya Arsenal kutwaa Ngao ya Jamii, katika mchezo huyo pia umeshuhudia nyota wa Liverpool, Takumi Minamino akifunga bvao la kwanza la msimu huu kwa timu yake. aidha, ni bao la kwanza tangu kujiunga na klabu ya Liverpool.

‘NGEKEWA’ YA MIKEL ARTETA

Hilo ni taji la pili la Mikel Arteta tangu alipokabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha Arsenal. Kutwaa kombe la Ngao ya Jamii kunampa ahueni kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ambaye alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo akiwa hana uzoefu wa kutosha katika mikikimikiki ya kuongoza timu akiwa bosi wa mwisho. Taji la kwanza ni la FA bila shaka nalo litakuwa chagizo la mafanikio zaidi ya Arsenal chini yake.

UCHU LIVERPOOL EPL

Mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2019-2020, Liverpool wana kikosi kipana kwa sasa na wanatarajiwa kukabiliwa na changamoto ya kutetea ubingwa wake.

Kipindi cha pili kilionesha namna ambavyo wanaweza kutetea ubingwa wao huku wakiwa na kikosi chao kamili kikiongezewa nguvu kutoka kwa Takumi Minamino na baadhi ya wachezaji chipukizi ambao wameonesha kuwa tayari kutetea taji lao.

Kiu ya ushindi bado wanayo, na wanaonekana kujiandaa kucheza na mabeki wawili wa kati huku viungo wakabaji wawili wakiwa na majukumu tofauti katika mfumo wa 3-5-2.

Fabinho alirudishwa nyuma kama kiungo mkabaji mwenye jukumu la kutawala eneo la beki nambari nne, huku Nabil Keita akiwa na jukumu la kupandisha mashambulizi ya Liverpool kutoka katikati. Kisha Takumi Minamino akiwa anashambulia kutoka pembeni na eneo la ushambuliaji kwa wakati mmoja.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
HN

Kati ya Bumbuli na Nugaz mmoja atoke Yanga

Wachezaji wa Yanga

Mabadiliko ya kiutendaji yaja Yanga..