in , , ,

Arsenal wachukua Barclays

*Mata alijua mapinduzi Man United

Arsenal walio kwenye matayarisho ya msimu mpya wamefanikiwa kutwaa taji la Barclays Asia baada ya kuwafunga Everton 3-1 kwenye mechi ambayo kiungo wake, Santi Cazorla alionesha kiwango kikubwa.
Wakati golini alianza kipa aliyesajiliwa kutoka Chelsea, Petr Cech, Cazorla alichangia upatikanaji wa mabao yote matatu. Msimu uliopita alicheza vyema na kutakiwa na baadhi ya klabu, wakiwamo Atletico Madrid, mwenyewe akiwa ni Mhispania.

Theo Walcott alifungua kitabu cha mabao katika nusu ya kwanza baada ya winga huyo kumalizia vyema mpira aliotiliwa na Cazorla. Walcott, mmoja wa wachezaji wenye kasi zaidi aiitumia kuwazidi mbio walinzi wa Everton.

Katika nusu ya pili Cazorla alikuwamo tena na kwa jitihada kubwa binafsi aliwapa Arsenal bao la pili na kufanya ubao kusomeka 2-0. ‘Mchawi’ huyu wa soka alimfaulisha James McCarthy, akimzunguka mara mbili kabla ya kutia kimiani mpira aliopiga kwa mguu wa kushoto.

Bao la tatu lilipatikana na Cazorla kumpatia mpira vyema kiungo mwenzake, Mesut Ozil aliyefanya matokeo kuwa 3-0. Ross Barkley wa Everton alichomoa bao moja, lakini kwa ujumla ulikuwa usiku wa Arsenal.

Arsene Wenger alitumia mechi chache za majaribio kuwapima wachezaji wake, ambapo aliowaanzisha kwenye fainali hii zaidi ni wale ambao aliwaacha katika mechi za awali.

Orodha ya Arsenal ilikuwa: Cech, Bellerin, Koscielny, Chambers, Gibbs, Ramsey, Cazorla (Coquelin, 76′), Wilshere (Oxlade-Chamberlain, 46′), Ozil, Walcott (Arteta, 71′), Giroud (Akpom, 76′)

Kwa upande wa Everton wanaofundishwa na Roberto Martinez, wachezaji walikuwa: Robles, Coleman, Stones (Browning, 84′), Jagielka (Hibbert, 84′), Garbutt, Barry, McCarthy (Osman, 61′), Deulofeu (Mirallas, 46′), Naismith (Barkley, 46′), Cleverley, Kone (Lukaku, 61′)

Katika hatua nyingine, mchezaji wa Manchester United, Juan Mata amesema kabla ya kujiunga nao Januari mwaka jana alishaelezwa mpango wa kukisuka upya kikosihicho.

Tangu Mata kuingia Old Trafford kwa pauni milioni 37.1 chini ya kocha David Moyes, wachezaji 10 wamewasili. Mata anadai aliambiwa yeye ni muhimu katika mabadiliko hayo, na angekuwa na uhakika katika kikosi cha kwanza.

Klabu wamekamilisha usajili wa viungo Bastian Schweinsteiger kutoka Bayern Munich na Mfaransa Morgan Schneiderlin ambaye kwenye mechi ya kujiandaa na msimu ujao alifunga bao.

Jumla ya pauni milioni 228.1 zimetumika kuwaingiza Old Trafford wachezaji hao, ikiwa ni pamoja na pauni milioni sita za kumchukua kwa mkopo wa msimu mzima uliopita Radamel Falcao ambaye sasa amejiunga Chelsea.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

UZEMBE UNAPOMSHIKISHA SINGANO MAMILIONI YA LEWANDOWSKI

Lionel Messi ndani ya Afrika