Menu
in , , , ,

Arsenal na tamko la ubingwa na laana ya Emery

Iwapo Arsenal wataunyakua Ubingwa la Ligi Kuu mwezi Mei, msisimko wa mbio za ubingwa utakumbukwa kwa furaha, huku njia ngumu walizopitia zikipewa thamani yake halisi. Huu ulikuwa ushindi wa kauli—uthibitisho kwamba maumivu na mateso yanaweza kuwa na maana. Timu ya mabingwa mara nyingi hulazimika kuteseka kabla ya kufika kwenye nyakati za uzuri. Ushindi wa kubahatisha dhidi ya Wolves, Everton na Brighton sasa unaweza kusherehekewa sambamba na usiku wa shampeni wa kuhitimisha 2025.

Uzoefu wa Arsenal wa kuwinda ubingwa kadri ligi inavyoelekea tamati umezaa wasiwasi usioepukika. Aprili na Mei hapo awali zimekuwa miezi yenye ukatili zaidi, lakini Desemba imejaa hofu pia. Kabla ya mechi, wimbo wa “North London Forever” uliimbwa kwa sauti ya kuyumba, mashabiki wakitafuta joto la pamoja kuondoa mashaka binafsi miongoni mwao, kuhusu ndoto yao. Kwa dakika 45, mashabiki, wachezaji na kocha walibaki na maumivu yao ya ndani, hadi kipindi cha pili ambacho Arsenal walicheza soka pana na lenye kujiamini kama la ubingwa, wakifunga mabao manne na kuyeyusha kabisa hofu.

Tanzania Sports
Msimamo wa EPL, baada ya michezo ya jana

Aston Villa walikuwa wapinzani wa kuogofya na wanaofahamika sana. Kukatisha ghafla mfululizo wao wa ushindi—na huenda ndoto yao ya ubingwa—kuliongeza ladha ya ushindi huo, kukizika kivuli cha hivi karibuni na hata baadhi ya waliowahi kuwa wafanyakazi wa klabu. Emi Martínez, aliyewahi kuwa Gunner, alichochea hasira kwa kupoteza muda, na alizomewa alipokuwa anaelekea mapumziko. Jinsi gani mashabiki wa nyumbani walifurahia kuona akihusika katika bao la kwanza la Arsenal. Ilikuwa siku 24 tu zilizopita tangu bao la ushindi la dakika ya 95 la Emi Buendía huko Villa Park liwaache wachezaji wa Arsenal wakidondoka ardhini kana kwamba Mei ya kukatisha tamaa ilikuwa tayari imefika.

Si mara nyingi Mikel Arteta huwa ndiye meneja asiye na shughuli nyingi zaidi katika eneo la benchi, lakini Unai Emery alionekana mwenye wasiwasi mkubwa zaidi, akivuta pumzi ndefu za hewa ya usiku wa London kana kwamba amenaswa na harufu isiyopendeza. Kero yake ilieleweka: Villa wangeweza kuwa mbali mbele kufikia mapumziko, ila mashambulizi yao ya kushtukiza yaliyoiumiza Chelsea hayakuwatumikia safari hii. Ollie Watkins alilaumiwa zaidi; bao lake la saba katika mechi 12 dhidi ya wapinzani anaowapenda lilikuja wakati hatima ya Villa ilikuwa tayari imeshaamuliwa.

Muda umekuwa mwema kiasi kwa kipindi cha Emery katika Uwanja wa Emirates, kazi aliyochukua katika mazingira magumu. Kuachishwa kwake miaka sita iliyopita kumeonekana kuwa uamuzi sahihi kwa pande zote, hasa kwa Arteta—kocha aliyepitwa kwa niaba ya ‘Mbasque'( eneo katika spain linalotaka kujitenga na mamlaka) mwenzake. Mashabiki wa Arsenal waliomdhihaki Emery wangeweza badala yake kusherehekea ushindi wa saini wa Arteta dhidi ya “mwanaalchemia” aliyeipeleka Villa kwenye viwango visivyoonekana kwa miongo kadhaa, na ambaye hapo awali alikuwa na namba ya mrithi wake—Arteta akiwa na ameshinda mara mbili tu kati ya mara nane. Mpango wa Emery si siri: kaa nyuma, usitafute umiliki mkubwa, haribu inapobidi; na wakati wa maamuzi, shambulia bila huruma. Kufungwa kwanza si tishio; ushindi wao watano mfululizo ugenini ulitokana na kuachwa nyuma bao moja. Lakini kufungwa mawili, kisha matatu, halafu manne, hakukuwa kwenye mpango wowote.

Pasi ya Martin Ødegaard kwa Martín Zubimendi aliyefunga kwa utulivu bao la pili iliachilia homoni za afueni kwa umati uliopata sauti mpya isiyolenga tena kumshambulia mwamuzi Darren England. Sherehe za bao la Leandro Trossard zilicheleweshwa na uhakiki mrefu wa VAR. Bao la nne la Gabriel Jesus lilikuwa la kwanza kwake msimu huu—kwa mshindi pekee wa zamani wa Premier League ndani ya kikosi—likikumbusha nguvu iliyo mikononi mwa Arteta.

Kurudi kwa nguzo ya ulinzi ya Gabriel Magalhães na William Saliba kulikuwa habari njema kuliko hofu ya kabla ya mechi kuhusu jeraha la goti la Declan Rice—tahadhari zaidi kuliko msiba. Kukosekana kwa Rice kulimaanisha huu ulikuwa wakati wa mashujaa wengine. Kikosi kikubwa na cha gharama cha Arteta kiliundwa kwa dharura kama vita. Kuona viungo warefu wa Villa wakichukuwa mpira kwa umbali mrefu kupitia maeneo ambayo kawaida Rice hupatikana kulitawala kipindi cha kwanza chenye mateso, ambacho Viktor Gyökeres alikosa nafasi mbili za vichwa. Pia alipoteza mpira katika mchakato uliopaswa kuzaa bao la mapema zaidi kwa Watkins.

Msweidi huyo hayuko peke yake katika kubeba mzigo wa matarajio, lakini Arsenal wanahitaji zaidi kutoka kwa mchezaji aliyenunuliwa kama mshambuliaji wa msingi wa mradi; kurejea kwa Kai Havertz kwenye benchi kunaweza kuutikisa mradi huo, kama itakavyokuwa kurejea kwa Jesus. Tukio la kishujaa zaidi la Arsenal katika kipindi cha kwanza lilikuja pale kidole cha mguu wa Saliba kilipomnyima Watkins fursa ya kusukuma mpira wavuni. Kurudi kwa mwenzake kulikusanya tena ndoto ya, “Set piece tena,” waliimba mashabiki wa nyumbani baada ya Martínez kuparuza mpira na picha ile ile ya beki Mbrazili akifungia. Kuanzia hapo, mvua ya mabao na kelele ilikumbusha kwamba safari ya Arsenal kuelekea utukufu si lazima iwe ya tabu na mateso pekee. Ndani yao wana uwezo wa kufanikiwa kwa utulivu zaidi.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version