in , , ,

Arsenal, Man U, nguvu sawa

 
*Spurs wawaangamiza Newcastle
*Liverpool wapigana na kushinda

 
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester United jana walifanikiwa kucheza kwa kujihami muda mwingi wa mchezo na kwenda suluhu na Arsenal.

Katika mechi hiyo niliyoishuhudia na haikuwa nzuri sana, tangu mwanzo, kocha David Moyes anayekabiliwa na shinikizo la matokeo mabaya ya sare na kufungwa, aliwapanga wachezaji wake katika mfumo huo.

Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti Arsenal na inashangaza kwa matoleo ya suluhu wakati Man U wamekuwa wakifungwa msimu huu sana na timu ndogo au kwenda sare, kama ilivyokuwa Jumapili dhidi ya Fulham.

Wayne Rooney ambaye kwa kawaida ni mshambuliaji, alionekana zaidi katika kiungo huku aliyetakiwa kuwa pacha wake kwenye ushambuliaji, Robin van Persie akifunikwa.

Katika mechi hiyo ya kusisimua, Arsenal walijaribu kila njia kupenya kiungo na ngome ya Man U na mara chache walipofanikiwa fursa zilipotezwa na akina Olivier Giroud aliyekosa bao la wazi alipomwagiwa majalo na Bacary Sagna.

RVP mara mbili alijaribu bila mafanikio kumtungua Wojciech Szczesny, dakika za mwanzo kabisa alipozawadiwa na Mikel Arteta lakini shuti lake kali likadakwa na kipa.

Kipindi cha pili alimpa mtihani kipa huyo wa Arsenal kwa kichwa kizito, lakini Szczesny alipangua kwa kuusukuma mpira juu ya mtambaa wa panya.

Kwa matokeo hayo Arsenal wamebaki nafasi ya pili kwa pointi 56, moja nyuma ya vinara Chelsea na mbili mbele ya Manchester City wenye mchezo mkononi baada ya mechi yao dhidi ya Sunderland kuahirishwa kutokana na hali mbaya ya hewa huko Eastlands.

Mechi nyingine baina ya Everton na Crystal Palace iliahirishwa kwa sababu hizo hizo pia, ambapo upepo mkali ulikuwa ukivuma.

Newcastle walichezea kichapo cha 4-0 wakiwa nyumbani kutoka kwa Tottenham Hotspur, Swansea wakaena sare ya 1-1 na Stoke na Liverpool wakashinda kwa tabu 3-2 dhidi ya Fulham baada ya kuanza kufungwa.

Liverpool wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 53, tatu zaidi ya Spurs wakati Everton ni wa sita wakiwa na pointi 45.

Nafasi tatu za mwisho zinashikwa na Sunderland wenye pointi 24 sawa na Cardiff huku Fulham wakiwa na pointi 20 mkiani. Hata hivyo Sunderland wana mchezo mmoja mkononi.
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TWIGA STARS IKO VIZURI KUIVAA ZAMBIA- KOCHA

Rio

Man United yanyemelewa na hasara