Argentina wamefika hatua ya Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuwafunga Uholanzi kwa mikwaju ya penati.
Hii ni mara ya kwanza tangu 1990 kwa Argentina kufika hatua hiyo na watakabiliana na Ujerumani Jumapili katika mechi ya mwisho.
Dakika 120 zilimalizika bila timu yoyote kupata bao na changamoto ya penati ikashuhudia Wadachi wakiloa baada ya kukosa penati mbili.
Fainali hii itakuwa marejeo ya mwaka 1986 na 1990 kwa timu hizo. Kipa wa Argentina, Sergio Romero ndiye alikuwa shujaa kwa kuokoa penati za Ron Vlaar na Wesley Sneijder.
Kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal hakutumia mtindo wake wa robo fainali wa kumwingiza kipa Tim Krul kwa ajili ya penati, bali alimwacha namba moja wake, Jasper Cillessen ambaye hakuweza kuwasaidia.
Uholanzi watacheza na Brazil kutafuta mshindi wa tatu Jumamosi hii.
Comments
Loading…