*Ubelgiji, Ujerumani, Colombia wafuata
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limewatangaza Argentina kuwa timu inayoongoza kwa ubora wa kiwango cha soka duniani, ikiwa ni mwaka mmoja hivi tangu walipofika fainali ya michuano ya Kombe la Dunia na kushindwa kutwaa ubingwa huo.
Argentina wanajivunia kwa kuwa na kikosi kizuri ambacho wachezaji wake wanakipiga katika klabu kubwa nchi tofauti duniani, wakiwamo Lionel Messi wa Barcelona, Sergio Aguero wa Manchester City na kipa mpya wa Manchester United, Sergio Romero.
Nafasi ya pili inashikwa na Ubelgiji, ambao wametokea kuwa wazuri katika miaka ya karibuni, wakitamba wachezaji katika Ligi Kuu ya England, kama vile Romelu Lukaku wa Everton, Marouane Fellaini wa Manchster United, nahodha wa Man City, Vincent Kompany na kiungo mpya wa timu hiyo, Kevin De Bruyne. Yumo pia mchezaji bora wa mwaka jana England, Eden Hazard.
Mabingwa wa dunia, Ujerumani, wanashika nafasi ya nne ikiwa ni karibu mwaka tu tangu wachukue taji hilo kubwa zaidi duniani. Nafasi ya nne imekwenda kwa Colombia wakati Brazil, wana Samba wapo nafasi ya tano.
Ureno wenye mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo wanashika nafasi ya sita wakifuatiwa na Romania. Chile waliotwaa ubingwa wa Copa America wakiwa na wachezaji nyota Arturo Vidal wa Bayern Munich na Alexis Sanchez wa Arsenal wanafuatia.
England wamepigwa butwaa kipindi hiki, na kwao ni habari kubwa kwamba ndugu zao wa Wales wamewatangulia kwa kushika nafasi ya tisa na England wenye ligi maarufu zaidi duniani wakishika nafasi ya 10. Hii ni mara ya kwanza kwa Wales kushika nafasi hiyo.
Comments
Loading…