Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez amepigiwa kura kuwa mchezaji bora miongoni mwa washabiki wa soka.
Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA) kimetangaza kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile amewapiga kumbo Eden Hazard wa Chelsea na Sergio Agüero wa Manchester City.
Sanchez katika msimu wake huu wa kwanza England, amefunga mabao 16 na kutoa pazi zilizozaa mabao manane. Hazard ndiye aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wakati Aguero alitwa akiatu cha dhahabu. Sanchez alikuwa kwenye mchujo wa wachezaji bora wa PFA pia.
Zaidi ya kura 200,000 zilihesabiwa baada ya mchujo wa wanasoka kufika 10 kutangazwa mwanzoni mwa mwezi huu.
Sanchez, 26, alisajiliwa Arsenal kwa ada ya pauni milioni 30 akitoka Barcelona alikokuwa hapati fursa ya kucheza soka mara kwa mara. Sanchez alizaliwa Desemba 9, 1988 na alianzia soka yake Cobreloa, kabla ya kuhamia Udinese Calcio mwaka 2006.
Baada ya kutolewa kwa mkopo kwa klabu za Colo-Colo na River Plate, alirudi na kucheza Ligi Kuu ya Italia kisha mwaka 2011 akasajiliwa na Barcelona kwa pauni milioni 25, akiwa mchezaji wa Chile aliyehamishwa kwa bei kubwa zaidi katika historia ya soka ya nchi hiyo.
Aliposajiliwa Arsenal Julai mwaka jana alitokea kuwa mchezaji wa pili kwa kulipiwa ada kubwa ya uhamisho na Arsenal, nyuma ya Mesut Özil aliyenunuliwa kutoka Barcelona. Sánchez amechezea Timu ya Taifa ya Chile tangu 2006 na amechezea taifa lake mechi 75, ikiwa ni pamoja na fainali mbili za Kombe la Dunia 2010 na 2014