in , ,

Al Ahly watupwa nje


*TP Mazembe, AS Vita wasonga mbele

Vinara wa Misri, Al Ahly waliotwaa ubingwa wa Afrika mara nane wametupwa nje ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Mashetani Wekundu hao wa Cairo walirudishwa nyumbani baada ya kupoteza mechi yao ya marudiano dhidi ya Al Ahli Benghazi wa Libya kwa mabao 3-2.

Katika mechi ya kwanza, Ahly waliowatoa Yanga kwa matuta jijini Cairo, walifungwa bao 1-0 kwa bao safi la Edward Sadomba.

Waarabu hao walikuwa wakiwinda ubingwa huo kwa mara ya tatu na walianza kuonesha dalili kwamba wangeondolewa walipocheza na Yanga, ambapo jijini Dar es Salaam walichezea kichapo cha bao 1-0 kabla ya kupata ushindi wa 1-0 Misri na kupigiana penati, wakawazidi Yanga kwa moja tu.

Al Ahli Benghazi sasa wanaingia kwenye awamu nyingine yenye fedha nyingi ambayo ni ya makundi.

Timu nyingine iliyovuka ni Zamalek wa Misri waliowafunga Nkana Red Devils wa Zambia
5-0 kwenye mechi ya marudiano, kupitia mabao ya Ahmed Tawfiq, Moemen Zakaria, Omar Gaber, Hazem Emam na Ahmed Gaafar. Mechi ya kwanza iliisha kwa suluhu.

Kukutana kwa timu hizo kumekumbushia mechi baina yao 1984, ambapo Zamalek walishinda mara zote nne walizokutana.

TP Mazembe wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo walikuwa wa kwanza kufuzu baada ya kuwapiga Sewe San Pedro wa Ivory Coast.

Mazembe walishatwaa kombe hilo mara nne, na kufuzu kwao kumewezeshwa na Mtanzania Mbwana Samatta aliyeingia kipindi cha pili na kutupia bao pekee. Samatta pia alifunga katika mechi ya kwanza Abidjan ambapo walipoteza kwa 2-1 hivyo kuvuka kwa faida ya bao la ugenini.

Kongo pia watawakilishwa na klabu nyingine, AS Vita waliowafurusha mashindanoni Kaizer Chiefs wa Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 5-0.

Sfaxien wa Tunisia nao wamevuka baada ya kushikilia rekodi yao safi kwa kuwafunga
Horoya wa Guinea 2-1 baada ya mchezo wa kwanza pia kushinda 1-0.

Mabingwa wa 1988, Entente Setif wa Algeria nao wamevuka kwa kuwatoa Coton Sport wa Cameroon kwa jumla ya mabao 2-0.

Esperance kutoka Tunisia tena wanaendelea kutokana na kuwaondosha mashindanoni Real Bamako wa Mali. Al Hilal wa Sudan pia wamepenya kwa faida ya bao la ugenini kwani walikwenda suluhu mechi ya marudiano nyumbani kwao wakati mechi ya kwanza dhidi ya Leopards wa Kongo Brazaville jijini Omdurman walikwenda sare ya 1-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Azam wakaribia ubingwa

Jezi za England hazishikiki