in ,

AFCON 2019: Vilio, kwa wengine vicheko

WAKATI wa dakika za mwanzo za mechi baina ya Taifa Stars na Kenya, zilisikika kelele za washabiki wa Tanzania wakiwashangilia wachezaji wao, kwa maana mara mbili waliongoza dhidi ya Harambee Stars wa Kenya.

Hata hivyo, msisimko mkubwa waliokuwa nao wananchi wa Tanzania uliishia kwa unyonge mkubwa baada ya Kenya kutoka nyuma mara mbili wakisawazisha kabla ya kupachika bao la ushindi dakika 10 tu kabla ya kipute kumalizika.

Kocha Emmanuel Amunike na wachezaji wake walipambana lakini haikuwa siku yao, wakipoteza mechi ya pili baada ya kuwa wamefungwa 2-1 na Senegal na sasa wanasubiri mechi ya mwisho dhidi ya Algeria wanaoongoza, lakini hakuna tena matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano kutoka Kundi C.

Wamebaki mkiani wakiwa hawana hata alama moja, wenzao Kenya wakiwa nazo tatu sawa na Senegal na wawili hao wanakutana Jumatatu hii kwenye mechi ya kuamua nani aungane na Algeria kwenye mwondoko wa moja kwa moja kuingia kwenye mtoano, kwani ni timu mbili katika kila kundi zinajihakikishia kusonga mbele.

Algeria wenyewe wanazo alama sita, baada ya kuwa wamewapiga Kenya na Senegal kwenye mechi zao mbili za awali. Imebaki mechi moja dhidi yaTanzania.

Afrika Mashariki ilipata pigo jingine baada ya Burundi kupigwa 1-0 na Madagascar ambao walikuwa wakichukuliwa kama wasindikizaji tu. Nigeria wamefuzu kwenye Kundi B, wakishinda pia mechi zao mbili walizokwishacheza, wakifuatiwa na Madagascar huku Guinea na Burundi zikiwa mkao wa kurudi nyumbani.

Wenyeji Misri wameshajihakikishia kusonga mbele kwenye kundi lao baada ya kunyakua alama sita kwenye mechi mbili na Afrika Mashariki wanapata faraja kwa Uganda ambao baada ya mechi mbili wana alama nne, wakiwaacha Zimbabwe na alama moja na Kongo Kinshasa wakiwa hawana kitu na wametolewa.

Katika Kundi D baada ya mechi moja moja, Ivory Coast na Morocco wana alama tatu kila mmoja huku Namibia na Afrika Kusini wakiwa hawana chochote. Kwenye Kundi E Mali wana alama tatu huku Angola na Tunisia kila moja ikiwa na alama moja na wageni Mauritania wakiwa hawana chochote.

Kundi F mabingwa watetezi Cameroon wanazo alama tatu, Benin na Ghana wakiwa na alama moja kila mmoja huku Guinea-Bissau wakiwa hawana chochote baada ya mechi moja moja pia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Soka ya Afrika siku ya tano

Tanzania Sports

Msimu mpya na usajili mpya