MFUKO wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda, magodoro na mashuka ili kusaidia serikali katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali za uma.
Msaada huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, alioutoa kwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali hiyo wakati akiwa naibu waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama wajawazito waliofika hospitalini hapo kujifungua wengine wakilala chini kutokana na uhaba wa viotanda, alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa ni Mfuko unaotoa huduma kwa jamii, nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na kuirejesha kwa jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya matibabu ni wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.
Kufuatia maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015, ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, alikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Akipokea vifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Temeke, Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, aliishukuru PSPF, kwa moyo huo wa kusaidia jamii.
“PSPF mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati wakisubiri kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.” Alisema