in , ,

Yusuph Kagoma ni mali halali ya Yanga

Baada ya sakata la mchezaji Yusuph Kagoma kushika kasi kmati tendaji ya klabu ya Yanga imemwelekeza mwanasheria wa klabu ya Yanga kutoa msimamo kuhusu sakata la mchezaji Yusuph Kagoma.

Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga yaliyopo mtaa wa jangwani na twiga, ambapo Tanzania Sports ilikuwepo, mwanasheria huyo wa klabu ya Yanga amedai Yusuph Kagoma ni mchezaji wa Yanga

Mnamo tarehe 24 mwezi wa tatu ( 3) mwaka 2024 klabu ya Yanga kupitia kamati tendaji ilianzisha mazungumzo na klabu ya Singida Fountain Gate ya kumsajili Yusuph Kagoma.

Baada ya mazungumzo ya pande zote mbili yani klabu ya Yanga na klabu ya Fountain gate, pande hizo zilikubaliana kuuziana mchezaji huyo kwa thamani ya shilingi za kitanzania milioni 30.

Fedha hii ingelipwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilitakiwa kulipwa na klabu ya Yanga mwisho wa mwezi wa nne ambayo ni nusu ya pesa hiyo ambayo ni milioni 15  na Yanga walitakiwa kumalizia fedha hiyo mwisho wa mwezi 6 ambayo ni milioni 15 jumla kuwa milioni 30.

Tarehe 30 mwezi wa 4 klabu ya Yanga ilituma fedha kiasi cha milioni 30 kwenye account ya bank ya Singida Fountain Gate kama malipo ya huyo mchezaji Yusuph Kagoma. Hivo ikawa imetimiza masharti yote kwa kutoa fedha yote ya usajili kwa ajili ya Yusuph Kagoma

Kabu ya Yanga iliruhusiwa kufanya maongezi na Yusuf Kagoma ambapo tarehe 27 mwezi wa tatu Yanga ilimtumia Yusuf Kagoma ticket ya ndege ya Airt Tanzania kutoka Kigoma kuja Dar es SaSalaam.

Baada ya mazungumzo kati ya mchezaji na klabu ya Yanga walikubaliana kusaini mkataba wa misimu mitatu. Mchezaji alikuwa chini ya mwanasheria wake Leonard Richards ambapo wote walisaini mkataba kwa pamoja.

Baada ya hapo tarehe 6 mwezi wa 7 klabu ya Yanga ilipokea barua kutoka kwa Singida Fountain Gate ikiimba klabu ya Yanga kuwa yale malipo ya milioni 30 waliyofanya awali yawe malipo ya Nickson Kibabage.

Tarehe hiyo hiyo ya 6 mwezi wa 7 klabu ya Yanga ilituma milioni 30 kwa klabu ya Singida Fountain Gate kama malipo ya mchezaji Nickson Kibabage.

Kwahiyo Yanga ikawa imelipa milioni 60 jumla kwa ajili ya wachezaji wawili wa Singida Fountain Gate yani Nickson Kibabage na Yusuf Kagoma. Maelezo hayo kutoka kwa mwanasheria wa klabu ya Yanga yaliambatana na ushahidi wa mikataba kati ya Yanga na Singida Fountain Gate na Yanga na mchezaji husika Yusuph Kagoma.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Usajili wa Kiangazi EPL 2024:

Tanzania Sports

Yanga wanadanganya kuhusu Kagoma