Kutoka katikati ya kiwanja kulifikia lango la adui, Yanga walikuwa na uwezo wa kupiga pasi 6 mtawalia. Katika eneo lao kutoka langoni mwa Abdutwalib Msheri hadi katikati ya kiwanja Yanga walikuwa na uwezo wa kupiga pasi 14 mtawalia. Mchezo mkubwa wa Yanga ulikuwa unaanzia kwenye 18 za Fountaine Gate. Je ilikuwa kwenye mchezo huo ambao Yanga wameibika na ushindi wa mabao matano kwa nunge? hii ni tathmini ya TANZANIASPORTS.
Je kiufundi Yanga walipangaje?
Katikati ya dimba kuelekea lango la adui (Fountain Gate) Yanga walipanga wachezaji 6 ambao walikuwa na kazi ya kuzuia Fountaine Gate kuvuka eneo hilo. Wachezaji watatu walikuwa kwenye durasa wakijigawa mmoja nyuma ya duara na wawili mbele ya duara. Kisha wachezaji watatu walisimama nje ya 18 ya lango la Fountain Gate kuwazuia mabeki wao kuanzisha mashambulizi. Hivyo Fountain Gate kila walipotaka kuanzisha mpango wa kushambulia kuelekea lango la adui walijikuta wanakabiliana na wachezaji sita wakiwa eneo lao hivyo mipira mingi ya Fountain Gate ilifia katika miguu ya wachezaji hao. Wachezaji wawili wa ulinzi walikuwa wakilinda lango lao, huku wawili wa pembeni kulia na kushoto wakiungana na wale sita wa wa eneo la duara katikati ya kiwanja kuelekea lango la adui. Hapo ndipo kocha wa Fountain Gate Mohammed Muya alifia kiufundi.
Yanga wamebadilika kiasi gani?
Kuzungumzia mabadiliko ya kiufundi kutoka kwa Miguel Gamondi na Sead Ramovic ni kwamba tofauti yao ni katika matumizi ya wachezaji. Kutokana na kuchez amfululizo, kocha wa Yanga wa sasa alichofanya ni kuwarudishia kujiamini na uwezo wao wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi. Ni sawa na kusema ‘Rotations’ ndicho kitu pekee ambao Yanga wamefanikiwa kukifanya sasa. Kila mchezaji anapata nafasi ya kucheza na kuimarisha uwezo wake.
Tofauti hiyo nji kwamba wakati wa Miguel Gamondi kuna wachezaji kama ni kama wal,ijikatia tamaa ya kupata nafasi. Lakini kocha mpya alichokiingiza na kinafanyika kwa haraka ni kubadilisha wachezaji na kuwapa nafasi kila inapobidi pamoja na kuwapunguzia dakika za kucheza kiwanjani. Kwa mfano Stephane Aziz Ki, Prince Dube wlaijikuta wakitolewa uwanjani katika dakika 70, ikiwa na maana kimchezo walicheza kwa dakika 50 kamili mbali ya muda wa mpira kurusha, kushangilia magoli na matibabu.
Kwahiyo wale wanaoingia kuchukua nafasi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza inawasaidia kuimarisha uwezo wao. Farid Mussa, Salum Abubakar, Dennis Nkane na wengine wananufaika kwneye hii ‘Rotation’. Miguel Gamondi alichelewa kutumia mbinu hii kwani alipojaribu kwenye mchezo dhidi ya Tabora United wachezaji waliowaingiza hawakuwa tayari kubeba majukumu hayo. Kwmaba walipaswa kupewa dakika katika mechi zilizopita ili waweze kujiweka sawa.
Je eneo la golikipa linaridhisha?
Bila wasiwasi wowote, Abdutwalibu Msheri ameonesha hali ya kujiamini na kuwa tayari kubeba majukumu ya kuwa kipa wa Yanga. Uzuri ni kwamba kipa huyu amejiboresha katika uwezo wake wa kutumia miguu na anaweza kusogea hadi yadi 30 kutoka langoni mwake hadi eneo la mabeki wa kati. Anakimbia vizuri, anatumia miguu yake vizuri. Ni dhahiri amechoma mengi mazuri kutoka kwa golikipa namba moja Djiqui Diarra.
Nani aondoke, nani abaki
Yanga wana kila sababu ya kujivunia wachezaji wao, ili dirisha la usajili litakapokamilika watakuwa na uhakika kwamba wachezaji gani wanaweza kutolewa kwa mkopo au wengine kuachwa kabiwa. Hadi sasa kwa uchezaji wa mzunguko unavyondelea ni dhahiri Yanga wana kibarua kigumu cha kuamua juu ya wachezaji wa kuruhusu waondoke. Hata hivyo ni timu ambayo inanufaika kwa kukaa pamoja muda mrefu na hata aina ya mabao wanayofunga sasa yanatokana na kufahamiana vyema kuliko umahiri wa kiufundi wa mwalimu. Timu ya Sead Ramovic bado haina kile kitu ha kiufundi ambacho kinatishia wapinzani. Badala yake sasa kuna umahiri wa wachezaji ambao unaweza kuwatisha wapinzani wa Ligi Kuu. Je itakuwaje kwenye mashindano ya Kimataifa hasa kwa mechi za Ligi ya Mabingwa? Hakika Yanga hii wanacheza, wanagusa bila kufanya nakshi nakshi za kitimu.
Comments
Loading…