in , , , ,

Yanga wanataka kuchukua kila kitu?

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu Yanga yupo kileleni akiwa na pointi 58. Nafasi ya pili imeshikiliwa na mahasimu wao Simba wakiwa wamejikusanyia pointi 57, huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na mabwanyenye wa Chamazi, Azam F.C. hadi sasa klabu hii imeonesha nia ya kutetea ubingwa wake mbele ya Simba. Lakini msimu huu Simba wamekuja kivingine wakiwa na ushindani mkali na tofauti ya pointi ni moja kati ya timu iliyopo kileleni na nafasi ya pili. Yanga na Simba zote kwa zimecheza mchi 22 kila mmoja za Ligi Kuu. Azam wao wamecheza mechi 23 wakiwa mbele moja dhidi yaSimba na Yanga.

TANZANIASPORTS inachambua mwenendo wa Yanga katika Ligi Kuu Tanzania ambapo tathmini inaonesha wanatamani kutwaa kila kitu katika msimu mwingine. Kuanzia viongozi, benchi la ufundi, na wachezaji wanaonekana kupania kufanya maajabu zaidi msimu kuliko ilivyozoeleka. 

Mfungaji bora

Hadi sasa kwa mechi 23 ambazo timu nyingine zimecheza, huku Yanga wakiwa na kiporo kimoja wanaonekana kuongoza kwa upachikaji wa mabao. Msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu unaonesha kuwa Yanga ndiyo timu kinara kwa upachikaji kutokana na idadi yake hadi sasa. Kati ya wafungaji 12 bora wa Ligi Kuu hadi sasa ni Yanga pekee ndiyo wameingiza wachezaji wengi. Simba ndiyo kinara katika ufungaji bora kwani mchezaji wao kiungo mshambuliaji Jean Ahoua amepachika mabao 12 katika mechi 22 za klabu hiyo. 

Kwa ujumla Simba wamefunga mabao 29 kwa wafungaji wake ambao wapo katika 12 bora ya upachikaji wa mabao. Jean Ahoua (12), Steven Mukwala (9), Leonel Ateba (8). Katika orodha ya wafungaji 12 bora Ligi Kuu Simba wana wachezaji watatu (3), wakati Yanga wanao wachezaji wanne (4). Yanga imepachika jumla ya mabao 34 kutoka kwa wachezaji wake Clement Mzize (10), Prince Dube (10), Stephene Aziz Ki (7) na Pacome Zouzoua (7). Singida United wanashikilia nafasi ya tatu kwa mabao 16 kutoka kwa Elvis Rupia (9) na Jonathan Sowah (7).

Vinara wa Asisti Ligi Kuu

Kinara wa kupika mabao Ligi Kuu hadi sasa ni Feisal Salum (Fei Toto) mwenyue jumla ya asisti 12. Lakini kwenye kipengele hiki tena wachezaji wa Yanga wameibuka vinara kwa kupika mabao. Wachezaji wanne (4) wa Yanga wanaongoza kwa kupika mabao Ligi Kuu. Max Nzengeli ametengeneza mabao 7, Stephane Aziz Ki (7), Prince Dube (7), na Pacome Zouzoua (6). 

Wachezaji hao wa Yanga wamepika jumla ya mabao 27 na kuwa vinara katika Ligi Kuu kwa upande wa asisti za mabao. Simba wenyewe Jean Ahoua ambaye ametengeneza mabao 7, ndiye mchezaji pekee wa klabu hiyo kwenye kipengele hiki.

Kwenye ‘Cleansheet’ wamo

Simba wameibuka vinara katika kipengele hiki na kuipiga kumbo Yanga. Golikipa wa Simba Moussa Camara ndiye anayeongoza kwa kuondoka na ‘cleansheet’ 15. Mpinzani wake wa karibu katika umahiri golini ni Djigui Diarra ambaye anashikilia nafasi ya pili akiwa ameondoka na ‘cleansheet’ 11. Kisha nafasi ya tatu imeenda kwa golikipa wa Azam, Mohammed Mustafa mwenye ‘cleansheet’ 10. Huu ni ushindani ambao umezidi kuifanya Ligi Kuu kuwa maarufu zaidi kwa sababu makipa wote watatu ni raia wa kigeni. Mustafa (Sudan), Diarra (Mali) na Camara (Benin).

Beki mwenye mabao mengi

Katika mchuano wa mabeki kupachika mabao Ligi Kuu, jina la mchezjai wa Ynaga ndilo limejitokeza na kuwashinda wengine. Ibrahim Hamad Bacca ameibuka kinara kwa upande wa mabeki kwa kupachika mabao manne (4). Bacca ndiye beki anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania. Wapo mabeki wengine mahiri kama Dickson Job (Yanga), Che Malone (Simba) ambao wana uzoefu mkubwa na Ligi Kuu lakini wamepitwa na Afande Bacca.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

20 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Pep Guardiola kuondoka Man City

Tanzania Sports

Siasa kwenye mpira wa miguu ni kero England