Bao la pili la Yanga lilitokana na kasi ya Kennedy Musonda kuliandama lango la adui…..

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania, Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASAS Djibout Telecom katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Azam Complex Chamanzi jijini Dar Es Salaam. Mabao ya Stephane Ki Aziz na Kennedy Musonda yaliwapa ushindi katika mchezo wa kwanza ambapo Yanga walikuwa ugenini. Mechi zote mbili za hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa zinachezwa nchini Tanzania baada ya Djibout kukosa viwanja vyenye vigezo vya CAF. 

TANZANIASPORTS ilishuhudia mtanange huo wa kukata na shoka, lakini Yanga wanatakiwa kujilaumu wenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi mnono. Yanga walikuwa na nafasi kubwa ya kufunga hata mabao matano, lakini maarifa yao mbele ya lango la ASAS Djibout yalikosa umaliziaji.

NANI AFUNGE

Bao la pili la Yanga lilitokana na kasi ya Kennedy Musonda kuliandama lango la adui. Shuti lake la mguu wa kulia lilikwenda kugonga kwenye kona ya inayounganisha vyuma ambayo hakuna kipa angeweza kugusa. Ni bao ambalo limeonesha kwanini Yanga walimsajili. Yanga inacheza Bila Fiston Mayele na safu ya ushambuliaji inawategemea Clement Mzize na Kennedy Musonda huku nyuma yao wakiwa Aziz Ki na Mudathir au Max Nzengeli. 

Tanzania Sports

Changamoto waliyonayo Yanga ni nani awe na jukumu la kufunga. Mechi nyingi kila mchezaji anayesogelea eneo la adui amekuwa na hamu ya kupachika mabao. Mashuti ya Yanga ni mengi kuelekea lango la adui. Huenda ukawa mpango mzuri kuondoa utegemezi kwa mshambuliaji mmoja, lakini inapora pia majukumu ya safu nzima kwani kila mmoja anataka kufumania. Ni swali ambao kocha Miguel Gamando anatakiwa kulijibu, nani awe jukumu la kufunga na timu icheze kwa ajili yake? 

GAMONDI ATATAPISHA DAMU

Mfumo wa uchezaji wa Yanga ni ule ambao unataka muda wote wawe na kasi. Iwe wakiwa na mpira au bila mpira lazima wacheze kwa kasi. Yanga wakipoteza mpira, haraka wachezaji watatu walianza kukaba kwenye 18 za adui yao. Clement Mzize,Kennedy Musonda na Mudathir Yahya walikuwa wa kwanza kuanzisha kasi ya kukaba mabeki wa timu pinzani waliokuwa wanaanda mashambulizi. 

Wakati watatu hao wakianza kukaba, Stephane Aziz Ki alikuwa anarudia hadi eneo la katikati ya Dimba kutibua mipango ya adui waliokuwa wanapenyeza mipira kuelekea kwa viungo wao. Aziz Ki alikuwa na kazi ya kusahihisha na kuwasaidia wachezaji watatu waliokaba mbele pale wanapoanzisha shambulizi. Vilevile alikuwa akibadilishana na Mudathir Yahya. Ni sababu hii ASAS Djibout Telecom walijikuta wanashindwa kuvuka mstari wa katikati kuelekea lango ya Yanga. 

Mipira yao mingi ilifia kwa wachezaji watatu waliokuwa wanakaba kuanzia kwenye 18 zao hadi katikati ya uwanja. Mfumo wa kucheza kasi ukiwa na mpira au bila mpira unahitaji wachezaji walio na utimamu wa mwili na kasi, pamoja na pumzi ya kutosha. Yanga walionekana kuwadhibiti wapinzani wao kwa mbinu hii hivyo wakawalazimika kupiga mipira mirefu. 

DIARA KAMA MWALIMU

Mchezo wa Yanga dhidi ya wenyeji wao, umedhihirisha zaidi kuwa Djigui Diarra ni mwalimu wa makipa wa soka Ligi Kuu. Ni kipa ambaye alikuwa anacheza hadi yadi 26 kutoka eneo lake la kawaida. Ni kipa ambaye anawapa mabeki wake kujiamini 

BEKI MBILI IKO KAZI

Kuna wakati unaweza kudhani beki wa kulia wa Yanga ndiye winga wao. Uchezaji wa beki wao mpya aitwaye Yao ni kiwango cha juu. Ni beki mwepesi,kasi,kotroo ya mpira na anashambulia hadi kwenye boksi la adui. Yao alikuwa beki ambaye anacheza kwa nguvu na muda wote anaomba nafasi, anatengeneza nafasi na kuliandama lango la adui. Kama kuna silaha kubwa waliyonayo Yanga basin i beki huyo wa kulia. Kwa hakika mabeki wa kulia waliopo benchi wana kibarua kigumu kumpoka namba nyota huyo. Nafasi ya beki kulia inaweza kuchezwa na Dickson Job, Ibrahim Bacca na Kibwana Shomari. Ni eneo ambalo Yanga wanapaswa kujivunia haswa.

WALIPOISHIA, SAFARI YAO NI NDEFU

Yanga wakivuka katika hatua hii, wanatakiwa kufanya marekebisho mengi ikiwemo kuua mchezo mapema. Katika mchezo dhidi ya ASAS, Yanga walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hawakuzitumia ipasavyo. Hili ni baya kwa mbele ya wapinzani wenye umahiri wa mechi za kimtaifa.

Pili, makosa yanayojirudia katika safu ya ulinzi. Nahodha Bakari Mwamnyeto na wenzake walikuwa wanataka kupiga chenga ndani yay a 18 zao. Wakati mwingine badala ya kutoa pasi haraka wakajikuta wanaliweka lango lao hatari kwa kushindwa kumiliki mpira ipasavyo huku wakiwa bila maadui. 

Tatu, kufanya uamuzi wa haraka katika kuondoa hatari langoni. Kipindi cha kwanza kulikuwa na makosa madogo madogo ambao yangeweza kuing’arimu timu hiyo, mfano umakini,kuzubaa,kuchelewa kutoa pasi, kukimbia umbali mrefu badala ya kuichezesha timu, kupoteza mipira kirahisi sana eneo la kiungo na safu ya ulinzi. Haya ni mambo yanayohatarisha mafanikio kwa timu yoyote. Yanga wachukue tahadhari kwa kurekebisha makosa hayo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba wanamaanisha kwa mbili hizi au bado?

Tanzania Sports

Kalvin Philips na taswira tata ya Guardiola