Wakati ligi kuu Tanzania Bara inaendelea Tanzania Sports.com tunaendelea kuangalia takwimu mbalimbali kutoka timu zilizopo katika ligi hii huku Yanga, Simba na Azam zikiendelea kuvuna alama tatu muhimu katika hatua ya tatu.
Wachezaji wa kigeni Yanga, Simba na Azam wazibeba timu zao kupata alama tatu muhimu.
Ugumu wa kuifikia rekodi ya raundi ya kwanza kufunga magoli 14 inakuwa ngumu zikiwa zimesalia mechi mbili kumalizia raundi ya tatu kwani magoli 10 yamefungwa katika mechi saba, endelea kusoma takwimu chini.
Hebu tuziangalie kwanza takwimu za mafahari wa tatu kisha tuangalie uchambuzi chini.
Yanga
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu Bara Yanga ilicheza siku ya Jumamosi uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera dhidi ya Kagera Sugar na imeweza kutafuna muwa mmoja na kurudi nao Dar es Salaam.
Yanga wameshinda mchezo huo kwa goli moja kwa sufuri, goli lililolofungwa na Mkongomani Mukoko Tonombe kwa kuunganisha pasi safi aliyoipiga ndugu yake Tuisila Kisinda.
Kwa mantiki hiyo Yanga imeshavuna alama 7 katika michezo mitatu ikiziachia mbili baada ya kutoa sare dhidi ya Tanzania Prisons.
Wanajangwani hao wamefunga magoli matatu na kufungwa moja katika mechi tatu huku watu wakilalamika juu ya ubutu wa kufunga kwa washambuliaji na wengine wakianza kuhoji uwezo wa kocha juu ya kuunganisha kikosi ambacho kinaonekana kiko vizuri.
Magoli yaliyofungwa kipindi cha kwanza kwa timu ya Yanga ni lile alilofunga Michael Sarpong dakika ya 19 ambalo lilikuwa la kusawazisha dhidi ya Tanzania Prisons baada ya Lambert Sabiyanka kufunga goli dakika ya 8 ya mchezo.
Magoli mawili yaliyoipa Yanga alama tatu muhimu yamefungwa kipindi cha pili ikiwa Lamine Moro dakika ya 86 dhidi ya Mbeya City na la Mukoko Tonombe aliyefunga dakika ya 72 dhidi ya Kagera Sugar .
Tutakuja kumuangaliua kocha wa Yanga baada ya michezo mitano tutakuja kumchambua.
Simba
Mabingwa watetezi Simba SC wameendelea kusumbua ligi kuu Tanzania Bara, mchezo wao waraundi ya tatu wameonekana kurejea katika zama zao.
Wameshinda magoli 4-0 dhidi ya Biashara United ambapo kipigo kikubwa cha pili baada ya kile walichokipokea Mbeya City kutoka kwa KMC.
Magoli ya Simba yamegawanyika kipindi cha kwanza na kile cha pili.
Wafungaji wakiwa wachezaji wa kigeni Chama, Kagere na Mugalu.
Magoli 5 yamefungwa kipindi cha kwanza wakati huo mawili yamefungwa kipindi cha pili.
Wafungaji kipindi cha kwanza John Bocco kafunga moja, Mzamiru Yassini kafunga mawili, Chama kafunga mawili huku waliyofunga hayo mawili ni Chrispine Mugalu na Medie Kagere.
Simba imefanikiwa kufunga magoli mengi zaidi katika ile ‘Top three’ ambapo wamepata magoli 7, Azam ikifuatia ikiwa na magoli 4 huku Yanga ikiwa na moja.
Azam FC
Wanarambaramba kutoka Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, wao wamefanikiwa kushinda mechi zote tatu.
Walianza kushinda 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, wameshinda 2-0 dhidi ya Coastal Union na wameshinda dhidi ya Mbeya City goli 1-0.
Goli lao pia limefungwa na mchezaji wa kigeni kutoka Rwanda Ally Niyonzima.
Katika magoli yao yote hayo 2 yalifungwa kipindi cha kwanza wafungaji wakiwa Obrey Chirwa na Ally Niyonzima huku mawili ya mwisho yakifungwa na Prince Dude.
UCHAMBUZI WA MECHI 7
Hadi muda huu tayari mechi saba zimepigwa na magoli 10 yameshadumbukizwa kambani, kila mmoja ana kiu ya kuona ni kweli ile rekodi ya raundi ya kwanza itavunjwa.
Katika raundi ya kwanza timu zote zikichangia magoli 14 ikiwa raundi ya pili yamefungwa magoli 13 na sasa zinasubiriwa mechi 2.
Simba imechangia magoli mengi katika raundi hii ya tatu kabla ya mechi mbili zilizobaki.
Katika raundi hii kwa mechi hizo saba yamefungwa magoli 10 ikiwa matano kipindi cha kwanza na matano kipindi cha pili.
Simba imefunga magoli yake kwa vipindi vyote viwili kwa kugawa kati kwa kati, mawili kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili.
Matokeo yalikuwa hivi, mchezo uliochezwa siku ya Ijumaa Polisi Tanzania na ndugu zao JKT Tanzania wameambulia sare ya kufungana goli 1-1 wakati huo Ihefu FC wamefungwa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Siku ya Jumamosi zilichezwa mechi mbili Tanzania Prisons imeitafuna Namungo FC goli 1-0, mchezo wa jioni Yanga imendeleza ubabe wake kwa Kagera Sugar kwa kuitandika goli 1-0.
Yanga huwa inapata alama tatu muhimu ilipocheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba tangu mwaka 2017.
Siku ya Jumapili zilichezwa mechi tatu, mechi ya mapema zaidi ilikuwa Mbeya City dhidi ya ya Azam FC ambapo Wanarambaramba wameshinda goli 1-0.
Mchezo wa pili ulikuwa wa sare ya kutokufungana kati ya Coastal Union dhidi ya wageni wa ligi Dodoma Jiji.
Na mchezo uliochezwa saa kumi Simba ikifanya mauaji ya mbwa koko baada ya kuibamiza Biashara United magoli 4-0.
Hapo sasa ndipo tunapokomea kuwa magoli 37 yamefungwa VPL katika raundi tatu huku zikisalia mechi mbili.