Timu ya Yanga itasajili wachezaji tisa msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom kwa taarifa kutoka ndani ya timu hiyo.
Yanga ambayo bado ina mapungufu makubwa imejinasibu kupitia viongozi wake kuwa watasajili wachezji tisa, ikiwa watano wa kimataifa huku wanne wakiwa wa wachezaji wa ndani.
Taarifa zinasema kuwa wachezaji 16 wataondoka ndani ya timu hiyo, ikiwa katika hao wengine waliomaliza mikataba yao, huku wengine watavunjiwa mikataba.
Yanga ambayo inahangaika kumaliza katika nafasi ya pili msimuu huu inahitajika kufanya uchaguzi sahihi wa wachezaji kwa ajiri ya msimu ujao.
Timu hiyo ilisajili wachezaji 22 msimu uliopita ambao wengi wao hawakuisaidia timu kufika pale inapotakiwa.
Baada ya dirisha dogo waliweza kuwaondoa zaidi ya wachezaji watano katika wale 22 waliosajili hapo awali.
Yanga imechukua makombe 27 ya ligi kuu bara huku ikiwa na kombe moja la michuano ya ‘Azam Sports Federation Cup’ huku wakichukua kombe la Afrika Mashariki maarufu kama Kagame mara tano.
Waliosajiliwa msimu huu unaokaribia kuisha ni pamoja na David Molinga, Benard Morrison, Issaa Bigirimana, Lamine Moro, Metacha Mnata, Ally Ally, Ally Sonso, Farouk Shikalo, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Adeyun Saleh, Sadney Urikhob, Mayben Kalengo, Mustafa Suleiman, Balama Mapinduzi, Makame, Eric Kabamba na Juma Balinya.