in

Wenyeji Ivory Coast waitesa Taifa Stars, Maximo asema poa tu

KIONGOZI wa kikosi cha Ivory Coast katika uwanja wa mazoezi, kocha mkuu, Kouaudio Georges ameonyesha mchecheto na kuwaamuru askari kuizuia Taifa Stars chini ya Mbrazili Marcio Maximo kubaki ndani ya basi kwa saa moja wakisubiri kuanza mazoezi.

Ujumbe mzima wa Stars ulilazimika kubakia kwenye basi lao waliloandaliwa na wenyeji hao kwa muda huo juzi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast (FIF), kilometa 25 nje ya jiji kwa ajili ya mazoezi kwa mujibu wa ratiba waliyokuwa wamepangiwa.

Kitu cha ajabu, walipowasili uwanjani hapo waliwakuta wenyeji wao, Ivory Coast wakiendelea na mazoezi yao na kocha wao alitoa amri kwamba wachezaji wa Stars wazuiwe kushuka kwenye gari ili wasione mazoezi yao.

Kwa upande wao, Stars wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye uwanja huo na wachezaji na kocha wa Ivory Coast wakiacha shughuli zao na kukaa kando wakiwaangalia kama filamu kwa kipindi chote cha mazoezi.

Hata hivyo, baada ya kuwazuia Stars kutoingia uwanjani, wengi walidhani kocha Maximo angepingana na amri hiyo, lakini badala yake aliwaruhusu vijana wake kutulia kimya kwenye basi kusubiri hadi hapo watakaporuhusiwa kuteremka.

Baada ya kumaliza mazoezi kikosi hicho cha Kouadio walifanya mazungumzo kwa takribani nusu saa katikati ya uwanja huo hali iliyofanya Stars kufanya mazoezi kwa kipindi kifupi zaidi kwa kuwa baadaye maofisa wa timu hiyo walisema taa haitawashwa huku wakitoa amri kama kichekesho kwa wachezaji wa Stars wajitahidi kuutumia uwanja huo kwa umakini ili kuepusha kumaliza majani, kitu kilichomfanya kila mtu kuangua kicheko.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Maximo ambaye jioni hiyo kikosi chake kilifanya mazoezi kwa dakika 50, alijibu: ”Vizuri kama kila mtu ameona hicho ni kitu cha ajabu, sisi tunajua kilichotuleta hapa na hakuna wa kutuzuia kufanya hivyo”.

Kwenye mashindano kuna mambo mengi na mengi huenda yakatokea. Si jambo muhimu sana,alisema.

Kocha wa Ivory Coast ndiye alifunga safari kutoka kwao kwenda Uganda kuishuhudia Stars, pia Zambia na Zimbabwe wakati zikishiriki michuano ya Chalenji na kusifia uwezo wa kikosi cha Maximo.

Ukiachana na hali hiyo, wenyeji wamekuwa wakijitahidi katika suala la maandalizi na kuzipa timu karibu kila kitu ukiachana na suala la uwanja ambalo siku mbili zilizopita lilizua mtafaruku mkubwa baada ya Maximo kupangiwa kufanya mazoezi mara moja kila siku, kitu alichokipinga hadi yalipofanyika mabadiliko.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Premier League – What the managers said

Watatu Stars watakiwa Ulaya