in , , ,

“Wambura alikufa 2010”

Michael Wambura

KAMATI ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imemtaka aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais ya klabu hiyo, Michael Wambura, kuwaomba radhi kutokana na kitendo chake cha kuwadhalilisha na kueleza kwamba Katibu huyo wa zamani wa Chama cha Soka Nchini (FAT sasa TFF) ‘alikushakufa’ tangu mwaka 2010.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Damas Ndumbaro, alisema mgombea huyo ameidhalilisha kamati hiyo kwa kueleza kwamba imekula rushwa ya ngono na fedha ili kupitisha majina ya baadhi ya wanachama waliokuwa wanawania nafasi za uongozi kwenye klabu hiyo.
20140206-130555.jpg

Ndumbaro alisema kwamba kauli aliyoitoa Wambura dhidi ya Kamati ya Uchaguzi imewadhalilisha na inamtaka awaombe radhi kwa kutumia njia ile ile aliyoitumia kutoa ‘kashfa’ na endapo hatafanya hivyo watamchukulia hatua.

Alisema kuwa kamati yake haikumuengua Wambura ila yeye mwenyewe ndiye aliyejiondoa kutokana na kosa la kuipeleka Simba mahakamani mwaka 2010 na kupelekea kusimamishwa uanachama wake.

“Wambura ni bingwa wa kwenda mahakamani, Simba ilimpitisha 2010, akagonga kisiki TFF kwa kumuondoa, kuipeleka Simba mahakamani ni sawa na kifo na kwa sababu alishakufa, kamati imemzika kwa kuamini kwamba alishakufa,” alisema Ndumbaro.

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kwamba kamati yake haikutaka kuanika ‘madudu’ yaliyofanywa na Wambura ikiwemo kuwasilisha barua ‘feki’ iliyosainiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Simba , Evodius Mtawala, lakini sasa itamuweka wazi.

“Kamati ilimuhoji Mtawala kuhusu barua ya kueleza Simba haina tatizo na uanachama wake, kiongozi huyo ameikana, nasema hivi Wambura amejivua nguo mwenyewe…alipaswa kuchutama badala ya kukimbia kama alivyofanya, na ndiyo maana hata uchaguzi wa mwaka 2010 hakushiriki alitolewa nje na aliondoka, ” Ndumbaro aliongeza.

Alieleza pia kamati yake inasisitiza kwamba inatambua Wambura alisimamishwa uanachama tangu Mei 5 mwaka 2010 na Kamati ya Utendaji iliyokuwa madarakani na kuhudhuriwa na wajumbe tisa na saba ndiyo hawakuhudhuria kikao hicho hivyo maamuzi yaliyotolewa ni halali.

Aliongeza kwamba kutokana na kusimamishwa uanachama wake, Januari 21 mwaka huu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji walihoji kuteuliwa kwake kuwa mjumbe wa kamati hiyo kwa sababu hakuwa na sifa zinazostahili.

“Ilibaki nafasi moja tu ya mjumbe kutoka Baraza la Wazee, na Wambura hakuwahi kuwa mjumbe wa baraza hilo, na pale alipotakiwa kujisafisha kwanza uanachama wake na Hanspoppe (Zacharia) alitoa lugha chafu akimjibu Hanspoppe aache siasa za jikoni, pia aliwahi kutoa kugha chafu dhidi ya Lyatto (Deogratius- mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF),” alieleza Ndumbaro.

Alisema pia Wambura ameenguliwa katika chaguzi nyingine tano alizowania hivyo hakuna anayemuonea kwa sababu tu mgombea huyo ameenda kinyume na katiba ya Simba, TFF na FIFA ambayo inakataza mdau yoyote kwenda mahakamani.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Fabregas anauzwa pauni mil. 30

Moyes: Laiti ningepewa muda Man United