kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.Kirwa anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range. Waamuzi hao wasaidizi ambao
vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini
hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa
na msisimko wa aina yake.
*MTIBWA SUGAR YAICHAPA TOTO 3-1 KOMBE LA UHAI*
Mtibwa Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14 mwaka huu) imeibuka na
ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mechi ya
michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini
ya miaka 20 (U20) za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Juma Luzio alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Alifunga
mabao hayo dakika za 44,81 na 88.
Hata hivyo, Toto Africans ndiyo walioanza kufunga katika mechi hiyo ya
kundi A. Bao hilo katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said
Salim Bakhresa kupitia maji Uhai lilifungwa dakjika ya 22 na Pastol Makula.
Nayo Simba imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya Tanga katika
mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa
Azam ulioko Chamazi. Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe dakika
ya 19, Mohamed Salum dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya 89.
Michuano hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting na
Kagera Sugar iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa
itafanyika saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi nyingine za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume),
African Lyon vs Azam (jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na
Yanga inachezwa leo Uwanja wa Chamazi.
Kesho (Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea
Jumapili kwenye viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na
Uwanja wa Azam- Chamazi.
*PONGEZI KWA UONGOZI MPYA DRFA*
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika juzi (Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi Garden.
Ushindi aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti pamoja na
wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa DRFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DRFA
ambayo hivi sasa ina kinara mpya, na kwamba ina changamoto kubwa ya
kuhakikisha inaendesha shughuli za DRFA kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya Juma Simba na
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha
uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo (Mwenyekiti), Meba
Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said
(Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu),
Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari
Mapande.
* *
*CAF KUFANYA UKAGUZI WA ‘LESENI ZA KLABU’ JANUARI*
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi
ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania
kabla ya kutoa leseni kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo
vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni
hiyo.
Kwa mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani
ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi
katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika
mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla
ya mechi.
Baadhi ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na
ofisi (physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo kwa
vijana, sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa (audited
accounts) na benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa zinazostahili.
Comments
Loading…