Ligi Kuu ya England ndiyo inayoongoza kwa umaarufu duniani, hivyo kwa kufuatiliwa kwa karibu na washabiki wa soka kupitia njia mbalimbali.
Moja ya mijadala mikubwa iliyopata kuibuka na hata kupamba vichwa vya habari ni kuhusu aina ya wachezaji wanaoshiriki kwenye klabu zake.
Ndiyo kusema kia anapotokea mchezaji mpya, watu huwa na shauku ya kujua anatoka nchi gani, lakini pia klabu ipi.
Baada ya pazia la ligi hiyo ya EPL kufungwa kwa msimu wa 2011/2012, ni vyema kutupia macho klabu na aina ya wachezaji zilizokuwa nao.
Wapo wachezaji wengi wa kigeni humu, kuliko ligi nyingine nchini hapa, kwa sababu ndiyo kubwa, na ina mvuto wa kimataifa.
Hata hivyo, ni jambo la kushangaza kwamba wachezaji kutoka mataifa 68 tofauti walishiriki kwenye Ligi Kuu kwenye msimu huo uliopita, mmoja tu pungufu ya walioshiriki kwenye Ligi ya Championship, iliyo ngazi moja ya chini ya EPL.
Kati ya wachezaji 522 waliocheza kwenye Ligi Kuu England, 212 walikuwa Waingereza. Hiyo ni idadi kubwa na ya kutosha kwa kocha wa timu ya taifa kuchagua wachezaji wake.
Ukweli ni kwamba mijadala kuhusu kutaka kanuni ziwekwe ili kutoa nafasi zaidi kwa wachezaji wa Kiingereza dhidi ya wale wa kigeni kwenye ligi hii haina maana.
Kwa kuzingatia idadi kubwa ya Waingereza wanaocheza katika ngazi hii ya juu ya soka, wanaoshadidia hilo hawana hoja.
Jedwali lililo hapa chini linaonyesha takwimu kwa kila moja kati ya klabu 24 za Ligi Kuu na uraia wa wachezaji wake waliocheza kwenye msimu wa 2011/2012.
Safu zenyewe zipo kama ifuatavyo – ‘Nats’ inawakilisha idadi ya mataifa ambako wachezaji wa timu husika wametoka wakati ‘Plyrs’ ni jumla ya idadi ya wachezaji wote wa timu.
‘Eng’ ni idadi ya wachezaji wa England walioshiriki, wakati ‘Sco’ ni wa Scotland, ‘Wal’ ni wa Wales, ‘NI’ ni Ireland Kaskazini na ‘Ire’ ni wale wanaotoka Ireland.
Tukiendelea hapa ni kwamba, ‘%Eng’ ni asilimia ya wachezaji wa England katika jumla ya wachezaji wa klabu nzima wakati ‘%B&I’ ni asilimia ya wachezaji wanaotoka England, Wales, Scotland, Ireland Kaskazini na Jamhuri ya Ireland.
Ni muhimu kufahamu kwamba England, Wales, Scotland na Ireland Kaskazini ndizo nchi zinazounda Uingereza, ambapo katika baadhi ya mashindano ya kimataifa kila moja hushiriki kivyake, lakini ni taifa moja – Britain.
Japokuwa inaeleweka kwamba Ireland ni nchi ya kigeni, imetumika hapa kwa sababu kipimo chake kinahitajika kwani wachezaji kutoka Ireland wamekuwa sehemu muhimu ya vikosi katika piramidi ya soka kwa miaka mingi.
Mgawanyo wa wacheazji wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2011/2012
Hakuna timu iliyochezesha wachezaji wengi wa England kama Queen Park Rangers (QPR) katika msimu huo, ikiwa na jumla ya wachezaji 19.
Hata hivyo, ni muhimu kutilia maanani kwamba QPR ilikuwa ikitumia wachezaji wengi zaidi (35) pia kwa ujumla wake katika kipindi hicho.
Stoke City ilikuwa na idadi ndogo ya jumla ya wachezaji (lakini bila shaka kwa muda mrefu), kwani ilikuwa nao 23, wakati Wigan ndiyo ilitumia wachezaji wachache zaidi wa England, watatu tu, katika msimu huo.
Wolves walioangukia pua msimu huo kwa kushushwa daraja, wakiisubiri Ligi ya Championship msimu ujao ilikuwa na wachezaji sita wa Ireland, ikiwa ni idadi kubwa kuliko klabu zote na watatu kutoka Wales.
Swansea hata hivyo, ndiyo ilichezesha zaidi wachezaji wake wa Ireland, na walikuwa wanne kwenye msimu huo, maana kuna tofauti ya kusajili na kuchezesha.
Manusura ya Wigan Athletic iliyokuwa kwenye kingamo la kushuka daraja yaelekea yalitokana na kuwa na wachezaji watatu kutoka Scotland huku West Brom na Fulham zikiwa na wawili wawili kutoka Ireland Kaskazini kwenye kampeni zao za ligi msimu uliopita.
Ni asilimia 28 tu ya wachezaji wa wababe wa Ligi ya Mabingwa, Chelsea ambao ni Waingereza na wa Ireland, tofauti na hao, Norwich ikiwa na asilimia 85 ya wachezaji kutoka nchi hizo mbili.
Timu inayoweza kuitwa ‘jeshi la kigeni’ ni Arsenal waliokuwa na asilimia 22 tu ya wachezaji wanaotoka Uingereza na Ireland kwenye msimu wa soka wa 2011/2012.
Wigan Athletic bado tunayo, kwani ilichezesha asilimia ndogo zaidi ya wachezaji wa England, huku iliokuwa nao kibindoni wakiwa ni asilimia 13 ya kikosi chake kizima.
Comments
Loading…