in

Wachezaji bora huanzia na kuwa na makocha wazuri.

Haya tena kwa mara nyingine tena, tunashuhudia ambavyo shirikisho la soka la Uingereza likisukumia lawama zake kwa kocha mkuu Stephen |McClaren na zaidi kufungua mlango wa majadiliano wa nani atanyakua nafasi yake kwa matumaini ya kwamba atakuwa kocha bora na sio bora kocha. Ni kitendawili kigumu kutegua ukizingatia kocha hupimwa kwa matokeo ya dakika 90 ambapo ni wachezaji ndio wenye kusukuma gozi uwanjani wakati kocha akiwa nje ya nyasi akiangalia ujuzi na mafundisho yake yakiwekwa katika vitendo zaidi.

Kuondoka kwa Stephen McClaren kunaiacha Uingereza palepale ilipokuwa miaka saba iliyopita, wakiwa wanatafuta kwa juhudi zote kocha mwingine wa kuziba pengo la kiuongozi na uwezo wa kujinasua katika mchafuko/mkorogo/ walioutengeneza wenyewe.

Kukosekeana kwa mechi zenye upinzani na ushindani wa kutosha kuanzia sasa hadi msimu ujao yanatoa nafasi ndogo sana ya kuwa na mwanzo mzuri ambao unategemewa kujumuisha uamuzi wa wa kusaka na kubadilisha kikundi kizima kinachojulikana kama “kizazi cha dhahabu” yakiwemo majina makubwa pamoja na wachezaji chipukizi/vijana wenye kutegemewa.

Lakini ukosefu wa aina yoyote ya ufundi na busara katika zoezi zima la kumchagua kocha maana yake kwa mara nyingine tena Shirikisho la mpira wa miguu linachukua hatua ambayo kwa wapenzi wa soka ni kama kuchomwa kisu gizani na zaidi matumaini na ndoto ya Taifa zima kwa ujumla inabaki mikononi mwao.

 

 

Sio siri, kitendo cha kumng’oa Stephen McClaren kimechukua msisimuko wa pekee kwa kila mpenda soka duniani. Ilikuwa ni vigumu kuamini na kuendelea kuangalia sura za wanaume zikitangaza kuondoka kwa McClaren maana ilikuwa ni kama kuangalia pete yako ya ndoa ikidondokea kwenye mto wenye kasi kubwa. Ni vigumu sana kwa wapenzi wa soka kuwa na hali ya matumaini kwa mpira wa miguu kwa siku zijazo. Sijui kama hawa watawala wanatambua au hawatambui utata uliopo, vilevile tukumbuke hata wao wako madarakani kwa kuaminiwa na Taifa. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa wao pia wamekuwa wakiongoza kwa makosa mengi katika majukumu yao ambayo inatupa ujumbe wa wazi kuwa wao nao watamfuata McClaren. Swali kubwa la kujiuliza ni nani atachukua nafasi zao kama wakiwatimua sasa?Je hao wapya watakaowateua watakuwa tofauti na waliowatangulia?staz2.jpg


Madiliko na mwelekeo mpya kutokana na kihoro hasa baaada ya kushindwa au kufanya vibaya katika jambo fulani na kufanya maamuzi yote yaonekane kama ya “mfa maji haachi kutapatapa”. Katika muongo wa nyuma tulikuwa na bwana wa mbinu kali (Hoddle) akifuatiwa na kipenzi cha wengi (Keegan), akitoa njia kwa kocha wa vibweka vingi vya ufichoni (Eriksson) naye akifuatiwa na bwana mwenye matumaini na mapenzi ya mpira (McClaren). Kwa kuwa uwezekano kisheria kuajri kocha toka nje upo, je watawala wataweza kumteua bwana Martin O’Neill, bwana mwenye kipawa cha pekee na asiyehitaji kuelezwa cha kufanya maana anajua afanyalo.

Lakini tukumbuke kuna Fabio Capello na Marcello Lippi, makocha wa kutumainiwa wenye kuongoza kwa mafanikio japo sifa zao hazifanani wameonyesha hamu yao ya kumpokea McClaren kijiti ili kuendelea mbio za soka la Uingereza, na bila ubishi shirikisho la mpira (FA) wanauwezo wa kuwamudu kigharama kama wanavyoweza kummudu Jose Mourinho ambaye kwake sifa sio klabu ya soka kutangaza nafasi ya kazi bali je klabu yenyewe inasifa nzuri? Kwa msemo mwingine chema chajiuza kibaya chajitembeza. Hapa ndio pa kujiuliza je FA wawe na matumaini ya kumpata Jose Mourinho? Bila ubishi uwezo wake kama kocha ni wa kiwango cha juu na cha kimataifa na huenda kipawa chake chaweza kubadili mtazamo wa wapenzi wa mpira wa miguu na kufanya timu ya Uingereza iwe kwenye kundi la chema chajiuza.

Je nani anajua kuwa hao makocha wanaopendekezwa watafanya vizuri kuliko McClaren, au zaidi ya Ericksson. Ni Lippi pekee yake ndio amefundisha timu kongwe ya kimataifa, wanaosalia kama Alan Shearer, Alan Curbishley na hata majina mengine yote ni utata mtupu na yatuonyesha jinsi ambavyo tunajiongezea utata na mashaka makubwa kwa nafasi kubwa na yenye kutumainiwa kama ya kocha wa timu ya taifa ya Uingereza.

Kihistoria hakuna kanuni ya “kufanikiwa” maana tumekuwa mashuhuda wa kuona mbinu moja iliyofanikisha timu moja ndio inakuwa sababu ya kuidondosha timu nyingine. Tunakumbuka Aime Jacquet aliibukia kutoka kamati ya ufundi ya shirikisho la soka la ufaransa na kushinda kombe la dunia

Ni siku chache zilizopita tumeshuhudia wagonjwa wakitibiwa kwenye gari la wagonjwa (ambulance) nje ya hospitali ya PFI iliyoko Norwich hapa Uingereza kutokana na uhaba wa vitanda hospitalini hapo kuweza kulaza wagonjwa zaidi. Swali la kujiuliza je sasa ni wakati muafaka kuacha kuhofia kuhusu mpira ambako nafasi ya juu kama kocha anaweza kulipwa mshahara paundi milioni tano kwa mwaka kama atafanya kazi yake vizuri na paundi milioni 2.5 kwa ambaye hatomudu vizuri.

Unategemea nini kutoka kwa kijana mdogo ambaye ni mchezaji kuweza kumudu na kuwa mtiifu kwa kipaji chake na hata kuweza kuwa na hamu ya kujiimarisha kwa juhudi binafsi wakati akiwa na miaka 22 anaweza kushinda na kuonekana hana hatia ya udhalilishaji nje ya klabu ya usiku kwa madai kuwa alikuwa anajihami kwa kuhofia kuna mtu alitaka kumuibia saa yake yenye thamani ya paundi elfu 64? Huyu ni kijana Anton Ferdinand wa West Ham ambaye alitenda kosa hili siku chache zilizopita, na tukumbuke kuna Vijana wengi ambao ni wachezaji wazuri sana lakini hawajapata bahati ya kuvaa kofia ya kuwa mchezaji wa kimataifa ambayo tayari wapo wanaoivaa na hawaonyeshi kuithamini au kuienzi.

Itakuwa na makosa na kutomtendea haki kama tutategemea kocha mpya aje abadili sura nzima ya soka la Uingereza kwa ujumla wake lakini kama ni kuchafuka kwa hewa ni vyema aanzie kusafisha uozo uliopo katika mfumo uliopo sasa kabla ya kuanza kufikiria kupata mafanikio katika timu.

Pamoja na yote ni wakati mwingine wa kuhesabu hasara maana kama FA ilimlipa Ericksson paundi za kumwaga kwa makosa ya kusitisha mkataba mapema sijui kwa McClaren watapata hasara gani japo ni wazi atatia kibindoni paundi milioni 2.5 kama kifuta jasho na kwenda barbados kujiliwaza huku akiwaacha wazee wa Shirikisho la Mpira wakikuna vichwa kutafuta mrithi wake.

Utawezaje kuunda timu bora? Fuata mfano wa Croatia

Ni vigumu kuamini lakini pia ni ukweli ambao ulitarajiwa kuona Uingereza ikienguliwa kutoka orodha ya timu zitakazoshiriki kombe la Ulaya 2008 (Euro 2008). Hauwezi kubeza au kuonyesha dharau kwa Croatia waliojitwalia ushindi hasa Luka Modric.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Company Profile

New England manager Fabio Capello has promised to deliver World Cup glory.