Menu
in

Wabongo Hawana Shukrani Kwa Kiduku

Tanzania Sports

Bondia namba mbili kwa ubora Tanzania Twaha Kiduku ameendeleza kuoensha ubora wake kwa kumtandika Sirimongkhon Lamthuam huku Babu Tale akitangaza kumsimamia.

Watanzania mara nyingi hawana uzalendo wa vitu vyao, siku zote hawataki maendeleo hata kama mtu akitumia uwezo wake mwenyewe.

Yaani hata ikitokea Yanga na Simba katika michuano ya Afrika wakipata timu ambayo itapoteza magoli mengi watasema wamepata kibonde muda wote wanawaza mawazo hasi yaani Tanzania hakuna chochote wao kupoteza tu.

Kijana wetu Twaha Kiduku amejitahidi na kupambana katika ajira yake ya ngumi lakini bado watu wanambeza.

Wakati naangalia ule mpambano katika kibanda umiza pale Kinondoni Moscow kwa Uwesu Matope maarufu kama ‘Ngwabi Stadium’ kabla mpambano haujaanza wakati huo wanaingia ulingoni  mashabiki walikuwa wamegawanyika kuna waliokuwa kwa Mthailand na kwa Mtanzania, sio kesi ushabiki haulazimishwi.

Kilichonifanya nipaze sauti baada ya matokeo kuna mneno ya dharau yaliongewa ambayo sijayapenda, naamini kinachosemwa Moscow ndicho kinachosemwa Kiwalani Kwagude.

KABLA YA MCHEZO

Wale waliokuwa upande wa Mthailand walikuwa wanasema maneno yafuatayo kwa Twaha Kiduku.

Wa kwanza “Leo amepatikana hapa amekwaa kisiki, amezoea kupata mabondia dhaifu tutaona leo,”

Mwingine  ‘’Huyu mzungu bingwa amepiga mapambano mengi leo lazima akae huyu Kiduku wenu maana amezoea kupewa ushindi,”

Wa mwisho “Hiki kibaba kitamkalishga mapema huyu Twaha anauzoefu wa hali ya juu,”

Hebu tukomee hapo kwa waliokuwa upande huo wa Mthailand na tambo zao.

Hawa wa upande wa Twaha Kiduku akiongozwa na Kabo wenyewe wanamuita ‘Ba Mdogo’ yeye alikuwa anaongea mazuri huku akiamini Twaha Kiduku angeshinda.

Siweki maoni ya upande wa Kiduku kwakuwa ujumbe huuu kwa waliokuwa wanambeza baada ya ushindi.

BAADA YA PAMBANO KUISHA

Baada ya bondia  Sirimongkhon kusalimu amri raundi ya saba sasa maneno kutoka kwa upinzani yaligeuka na kuanza kuongea shombo ambazo kama mwanamichezo hazikuwa sawa.

“ Bondia mwenyewe mzee, kibonge hajui hata kupigana si wamemleta ili ashinde tu,”

“Huyu bondia hata ingekuwa mimi asinge nipiga hawezi kabisa kupiga ngumi,”

“ Mapromota wameleta mtu ambaye hana uwezo wamempa ushindi tu , ningejua nisinge angalia,” walisema.

Hayo yalikuwa maneno ya baadhi ya mashabiki wa upinzani waliokuwa wanampinga Kiduku.

Tuelewane halazimishwi mtu kushabikia kitu ama mtu ila inapotokea mtu katumia jitihada zake na ukweli umeuona basi mpongeze.

REKODI ZA SIRIMONGKHON ZIKOJE ?

Amezaliwa Juni 2, 1977 huko nchini Thailand ameanza kucheza mchezo wa ngumi mwaka 1994 katika uzito mblimbali ukiwemo ‘Light Heavy’.

Amepigana mapambano 102 akipiga mapambano 61 kwa ‘KO’ , hivi ni kweli bondia kama huyu hajui kupigana kweli ?

Baada ya mpambano japo hata kuongea Kingereza ilikuwa taabu ila aliongea maneno machache na kusema kuwa Twaha Kiduku ni bondia mzuri.

Labda kejelei za wapinzani wangesema juu ya umri kidogo ingekuwa na mashiko, lakini miaka 43 bado kijana sana.

Kiduku alipata mashabiki wengi baada ya kumtandika Dulla Mbabe pia wapinzani walianzia hapo.

Kwa uwezo wake huku anaonekana anajitunza inawezekaana ikawa hadhina kubwa kwa taifa katika mchezo wa ngumi.

Watanzania wengi wanatamani kuona pambano likichezwa kati ya Hassan Mwakinyo na Twaha Kiduku, baada ya kumaliza ile ‘Show’ wengi walionekana kuhitaji mpambano huo.

Marcelo Kigu yeye ameweka wazi kuwa anatamani kuona Mwakinyo na Kiduku wakipatiwa pambano wazichape.

“Nafikiri sasa ni wakati wa Hassan Mwakinyo kukubali kupigana na Twaha Kiduku ili tujue nani mwamba,”alisema.

Mwingine ambaye alitamani  pambano katia ya mabondia hao wakutane ni Mwenyekiti wa Barcelona Zaidi ya Kinondoni Moscow  Ramadhani Salamata ‘Nyoka’  aliweka wazi kuwa wote wawili wapo katika kilele na mmoja anatakiwa apigwe ili ajue bingwa wa kweli nani Tanzania.

“Hawa wote ni bora natamani wakutane wazichape ili tuone nani namba moja wa kweli Tanzania ,”alisema.

Uwesu Ngwabi ambaye yeye ndio mmiliki wa Kibanda umiza hicho amesema kuwa ili utamu uzidi kukolea niingependa tambo ziendelee kama wakikubaliana iwe mwezi wa nne mwakani watakuwa wamejiweka sawa na watapiga hela sana.

“Huu mchezo unatakiwa taimingi, hawa watu wote bora waache watambiane wasikubali kwa sasa ifike muda kidogo hata mwezi wanne kisha mapromota waweze pesa mezani naamini itakuwa bora sana,” alisema Ngwabi.

Unachochote cha kutueleza  basi ungana nasi katika mitandao yetu ya kijamii weka maoni yako tutakujibu katika hali ya kujdiliana

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version