in , , ,

Vita ya pili ya Juma Kaseja katika soka

REKODI ya kocha wa Kagera Sugar imeanza vizuri na kusisimua mashabiki wa soka. Kocha huyo ambaye ni golikipa mahiri wa Kimataifa na mwenye uchawi mwingi katika udakaji wake amegeukia kazi ya ukocha tangu Machi 4, mwaka huu na sasa anakiongoza kikosi cha Kagera Sugar cha mkoani Kagera. Sifa za Juma Kasema ni nyingi mno. Timu za waarabu hasa Misri zinamfahamu Juma Kaseja akikaa langoni alikuwa kikwazo chao, unaweza kuwaulzia mashabiki wa Zamalek ambao wanaufahamu vyema umahiri wake.

Tangu alipokuwa Moro United hadi alipojiunga na vilabu vikuba viwili vya Simba na Yanga, bado umahiri wake haukuwa wa kutiliwa mashaka. Katika kikosi cha timu ya Taifa ni kipindi cha kocha Marcio Maximo pekee ndicho ambcho hakupata nafasi nzuri ya kuitumikia kwani Shaban Dihile ndiye alikuwa chaguo lake la kwanza. Ukizungumzia makipa mahiri nchini jina la Juma Kaseja ni miongoni mwa wale 10 waliowahi kutokea nchini kama si Afrika mashariki.

Licha ya kwamba baadhi ya mashabiki na wachambuzi waliowahi kuhoji kimo chake kama kinafaa kuwa golikipa, lakini Juma Kaseja aliendelea na safari yake hadi alipoamua kutundika daruga kwa hiari yake. Kwa ujumla Juma Kaseja ni mwakilishi wa wachezaji mahiri uwanjani ambao wamegeukia kazi ya ukocha. Baadhi ya wachezaji mahiri ambao waliwahi kutikisa viwanjani hawana umwamba wowote kwenye kazi ya ukocha. Baadhi ya wachezaji mahiri walitikisa uwanjani kama Mecky Mexime ambaye amejiandikia rekodi nzuri ya kuwa kocha mzawa mwenye uwezo wa kufundisha lakini wengine hawajafua dafu. Ivo Mapunda alikuwa akikiongoza kikosi cha Songea United bado hajaonekana kama mahiri kwenye kazi ya ukocha.

Kifupi wapo wachezaji ambao walikuwa na kiwango cha wastani lakini walipoamua kugeukia ukocha walikuja kuwa magwiji. Kwa mfano katika soka la nchi zilizoendelea wapo wachezaji mahiri na waliotikisa dunia kisha wakageukia ukocha ambako wamefanya vizuri hadi sasa. Kwa mfano Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alikuwa mchezaji mahiri huko nchini Italia, sawa na Zinedine Zidane ambaye aliweka rekodi ya kunyakua taji la Ulaya mara tatu mfululizo. Dedier Deschamp kocha wa Ufaransa alikuwa kiungo katili wakati fainali za Kombe la Dunia mwaka 1998 na Euro mwaka 2000 kabla ya kuangukia pua kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002. Deschamp ni kocha ambaye ametwaa kombe la dunia akiwaongoza Ufaransa. Diego Maradona aliwaongoza Argentina mwaka 2010 kwenye fainali za Kombe la Dunia lakini hakufika mbali na kazi yake haikulingana na umahiri wake wa kusakata kandanda.

Pele hakuwahi kuwa kocha kabisa. Wayne Rooney alikuwa mshambuliaji mkali akiwa Manchester United, lakini kwenye kazi ya ukocha hali ya mambo imekuwa tofauti. Amekuwa kocha wa kufukuzwa mara kwa mara kwenye timu anazopewa. Hali kadhalika Ole Gunnar Soskjaer naye amekuwa kocha wa hapa na pale ingawaje naye amepata medali ya ukocha tofauti na Rooney.

Katika bara ya Afrika magwiji wa soka kama vile Jay Jay Okocha hajageukia ukocha, wala Nwankwo Kanu hajawa kocha kabisa. Wapo mastaa wengine kama MacDonald Yobe wa Malawi, Benjam Mwaruwari, Sunday Oliseh, Marcell Dessailly, Lucas Radebe, Hans Vonk wote hawajageukia kazi ya ukocha. Safari ya Juma Kaseja inaweza kufanana na mashambuliaji wa zamani wa FC Porto na kocha msaidizi wa Man United, Benni McCarthy wa Afrika kusini ambaye mwaka huu ameajiriwa kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Kenya, maarufu kama Harambee Stars. Kwahiyo kazi hii inahusisha pande mbili; wachezaji waliokuwa mahiri na wachezaji wasiokuwa mahiri. Mfano Ruben Amorim hakuwa mahiri dimbani lakini ni mchezaji ambaye alitoa mchango wake. kabla ya kuwa kocha Ruben Amorim alikuwa mchambuzi wa soka kwenye Televisheni. Lakini hivi leo ndiye kocha wa Manchester United na maarufu kote duniani.

Tukirudi kwa Juma Kaseja ni dhahiri anawakilisha kizazi cha akina Zinedine Zidane. Hawa ni wale wachezaji waliokuwa wanategemewa kwenye timu. Ni wachezaji ambao walijulikana kwa ufundi, maarifa na umahiri wao. Ni wachezaji ambao wana mambo mengi ya kuthibitisha kati ya ubora wao na kazi ya ukocha. Zidane kwa nafasi yake amefanya sambamba na Ancelotti na wengineo. Kuwa mchezaji mahiri si kigezo cha kuwa kocha mahiri. Kuwa mchezaji wa kawaida si kigezo cha kuwa kocha mahiri, lakini wachezaji wengi ambao walikuwa wa kawaida wamekuwa makocha wazuri sana kwenye ulimwengu wa soka.

Vita vya Juma Kaseja

Kwa kuangalia namna alivyoanza kazi kama kocha wa makipa ungeweza kusema Juma Kaseja angebaki nafasi hiyo kuanzia ngazi ya klabu hadi Timu ya Taifa. Lakini sasa Juma Kaseja ameingia kwenye kazi ya ukocha ambao inamfanya awe sehemu ya uamuzi wa kusuka timu, usajili na masuala ya uendeshaji. Majukumu hayo ni ya amocha ambao wanajua kazi hiyo kw aufasaha. Juma Kaseja anaingia kwenye vita vya pili kuonesha kwamba yeye ni sio mahiri tu golini bali hata kwenye kazi ya ukocha anajua kufanya kazi yake. Tangu alipokabidhiwa jukumu la kuinoa Kagera Sugar hajapoteza mchezo wowote kati ya mitatu aliyoiongoza timu hiyo. Juma Kaseja alianza rasmi kazi yake Machi 4, mwaka huu akichukua nafasi ya kocha Melis Medo aliyeondoka Februari 25, 2025. 

Kagera Sugar ilianza kumpa ushindi wa mabao 2-1 Juma Kaseja katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Machi 7 mwaka huu. Michezo miwili iliyofuata ni ile ya Kombe la Shirikisho la FA. Katika michezo ya FA, Juma Kaseja aliwaongoza Kagera Sugar aliitoa Namungo ya Ruangwa, Lindi kwa kuichapa mabao 3-0 katika hatua ya 32, huku kwenye hatua ya 16 bora aliishushia kipigo Tabora United kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare bao 1-1 ndani ya dakika 90. Kazi kubwa aliyonayo sasa ni kuhakikisha anaweka rekodi kwenye kazi ya ukocha kama ambavyo alifanya kipindi akiwa  golikipa mahiri nchini.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

17 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Argentina na Brazil ni kama Simba na Yanga

Tanzania Sports

Estevao mgeni mpya EPL