in , , ,

Vita kali PSG na Real Madrid

Mbappe

Mbappe anaendelea kukipiga PSG licha ya kuwepo msuguano wa ndani kati ya kambi yake na uongozi wa klabu hiyo chini ya Nasser El Kheleif….

Ripoti zinaeleza kuwa klabu ya Real Madrid itatuma ofa ya kumsajili nyota wa PSG Kylian Mbappe ambayo haitakataliwa na uongozi kwa vile itakuwa siku za mwisho za kufunga dirisha la usajili. Mshambuliaji wa PSG Mbappe ameshaanza kuitumikia klabu hiyo msimu mpya licha ya kufukuzwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza kilichopo chini ya kocha Luis Enrique. 

Inaonekana kuwa Real Madrid wamepania kumsajili mchezaji huyo katika dakika za mwisho lakini wanatumia mbinu ya kuwaweka roho juu wenzao wa PSG ili ofa itakayotolewa siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa wasiweze kuikataa, vinginevyo watalazimika kukosa hata shilingi mia Juni 2024 ambapo Mbappe atakuwa anaondoka bure klabuni hapo. 

Tanzania Sports

Ripoti hizo zinasema kwamba Real Madrid wamepania kutumia mbinu hiyo kwa sababu klabu hizo hazina uhusiano mzuri kuanzia kwenye suala la usajili hata mengine ya kitaasisi. Inasemekana kuwa miamba hiyo ya Hispania itatuma maombi ya kumsajili Kylian Mbappe kwa PSG kati ya Agosti 29 na Septemba mosi mwaka huu, ikiwa ni siku za mwisho za usajili wa wachezaji. Maombi ya Real Madrid yanatarajiwa kuwa ya kiasi cha Euro milioni 120 sawa na Dola milioni 130. 

Mbappe anaendelea kukipiga PSG licha ya kuwepo msuguano wa ndani kati ya kambi yake na uongozi wa klabu hiyo chini ya Nasser El Kheleif. Kwa mujibu ya habari zilizoripotiwa na gazeti la Bild la Ujerumani na kukaririwa na vyombo vya habari vingine duniani zimesema kuwa mpango wa Real Madrid umekubaliwa na Bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo. Kiasi kilichopangwa kuwasilisha kwenye maombi ya usajili huo ni kidogo kulinganisha na kile kilichotangazwa na PSG. Klabu ya PSG iliweka dau kubwa karibu euro milioni 150 sawa na dola milioni 163 kwa timu inayotaka kumsajili Kylian Mbappe. Lakini mpango wa kuzipata fedha hizo huenda ukafeli ikiwa Real Madrid watawasilisha kiasi cha euro milioni 120 ambacho ni cha chini kuliko matakw aya PSG. 

Hata hivyo, ofa hiyo huenda isikataliwe kulingana na dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Bodi ya wakugurenzi ya PSG inatafuta namna ya kupata fedha kutokana na kumuuza nyota huyo kuliko kumwacha kikosini akaruhusiwa bure mara baada ya mkataba wake kumalizika Juni 2024. Mbappe amekuwa katika mazingira magumu tangu maandalizi ya msimu huu, ambapo PSG walikataa kuambatana naye kwenda kwenye mechi za maandalizi ya msimu mpya. Pia Mbappe hakuruhusiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza, kabla ya wiki iliyopita kuruhusiwa kuungana nao. 

Katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa, Mbappe aliingia kipinid cha pili wakati PSG ikiwa inamenyana na Toulouse jumamosi iliyopita. Mashabiki wa timu hiyo walipiga kelele kutoka jukwaani walipomwona nyota huyo akiingia uwanjani. Washabiki hao walimzomea yeye na kuonesha mabango ya kupinga tabia zake pamoja na udhaifu wa uongozi wa PSG kwani mwanzoni ulikataa kuruhusu nyota huyo kuichezea tena klabu hiyo. Malalamiko ya mashabiki wa PSG kwa uongozi ni kitendo chao cha kukiuka msimamo waliotangaza kutoruhusu nyota huyo kuichezea tena PSG na kwamba angekaa jukwaani msimu mzima hadi mkataba wake utakapomalizika.

Aidha, uongozi wa timu hiyo umebadili msimamo na sasa wameruhusu nyota huyo aicheee PSG lakini hali ya mambo ndani ya kikosi hicho inasemekana kuwa tete, kwani kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwa wachezaji wanaounga mkono msimamo mpya wa uongozi na wale wanaounga msimamo wa awali wa kumweka pembeni Mbappe.

Wakati huo huo, Real Madrid inahitaji mshambuliaji mpya wa kiwango cha kimataifa ambaye atafanya kazi sambamba na nyota chipukizi wa kikosi chao Jude Bellingham,Vinicius na Rodrygo. Mbappe anategemewa kuwa usajili bora kwa kikosi cha Real Madrid ambao wamepania kuichachafya Ulaya msimu huu kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa. siri ya mpango wa kuwasilisha maombi ya usajili wa Mbappe katika dakika za mwisho kabla ya kufungwa dirisha la usajili ni kutaka kuidhibiti PSG isiwe na muda wa mwingi wa kujadiliana juu ya uhamisho huo. Madrid wanajua PSG watalazimika kupokea dau hilo au wasipate kabisa na kuruhusu nyota huyo aondoke bure kikosini mwao. Hicho ndicho kibarua kizito na vita kali kati ya PSG na Real Madrid. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kalvin Philips na taswira tata ya Guardiola

Tanzania Sports

Kuna Azam FC Kimataifa?