Menu
in

Vilio Tanzania, Kenya zikitolewa CHAN

Taifa Stars

Taifa Stars

ILIKUWA Ijumaa iliyojaa huzuni kwa waandaaji wenza wa michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani – CHAN baada ya Tanzania na Kenya kutolewa katika hatua yar obo fainali.

Walikuwa ni Kenya walioanza kufungashwa virago na Madagascar kwa changamoto ya mikwaju ya penati, baada ya Kwenda sare ya 1-1 katika mud awa kawaida wa dakika 90 na nyongeza ya nusu saa, ikimaanisha walicheza jumla ya dakika 120.

Kabla na wakati wa mchezo, Kenya walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali, lakini mechi ilipoanza na kuendelea mamvbo yakawa kinyume chake, Madagascar wakisimama imara kujitetea.

Ndoto za Taifa Stars wa Tanzania kuingia nusu fainali kwenye CHAN 2024 zilikufa baada ya kushindwa kufumania nyavu za Morocco, huku wakiruhusu bao moja, ushindi mwembamba ambao hata hivyo uliwavusha Simba hao wa Atlas.

Wakicheza mbele ya maelfu ya washabiki waliokuwa wakicheza na kushangilia ndani na nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa tangu asubuhi, Stars walijitahidi kukabiliana na miamba hao wa Afrika lakini hawakuweza kutoboa ng’o.

Mechi ilianza kwa kasi, Taifa Stars wakijitahidi kupandisha mashambulizi, huku lango lao likilindwa vyema na golikipa Yakoub Ali ambaye kwa mechi ya jana aliokoa mabao kadhaa yaliyoonekana yangekuwa ya wazi.

Stars walisumbuliwa na wachezaji wa Simba hao kama vile Oussama Lamlioui , Iddi Selemani na golikipa wao, Elmehdi Al Harrar. Ilikuwa almanusra Taifa waongoze muda mfupi kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza, ambapo Clement Mzize alishindwa kutumia mbinu takikana kupata bao, akipiga shuti dhaifu baada ya kuwa amekwatulia kidogo ndani ya eneo la penati.

Katika kipindi cha pili Morocco walionekana kujikusanya vilivyo na kuwa wakali, wakishambulia kwa nguvu, ambapo kipa Ali aliokoa madhara waliyotakiwa kuwapatia Stars.

Baada ya ‘zuia zuia’ za hapa na pale, hatimaye Stars waliachia katika dakika ya 67 ambapo hatimaye Lamlioui alizifumania nyavu na kuwanyamazisha washabiki wa nyumbani waliokuwa wakisubiri kwa hamu kuona vijana wao wakifunga bao.

Abdul Suleiman nusura afunge dakika ya 70 wakati Nassoro Saadun alijitahidi bila mafanikio katika dakika ya 81, ikaonekana wazi kwamba ngoma ilikuwa ngumu na kwamba jahazi la Tanzania lilikuwa likizama taratibu.

Huko kwenye Uwanja wa Moi International Sports Centre jijini Nairobi, Kenya nao walilowanishwa kwa matuta, baada ya kwenda sare ya 1-1 kwenye dakika 120 za mchezo. Madagascar walipata ushindi kwa kufunga penati nne huku Kenya wakipata tatu ambazo hazikutosha.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version