in , ,

Vigogo FIFA wakamatwa

Vigogo wawili wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wamekamatwa nchini Uswisi, wakituhumiwa kwa makosa ya kupokea mlungula wa mamilioni ya dola.

Polisi walivamia hoteli ya kifahari ya Baur iliyopo jijini Zurich na kuwadaka maofisa hao walikokuwa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kamati kadhaa za FIFA. Ni humo pia ambako Mei mwaka huu maofisa waandamizi wa shirikisho hilo walidakwa.

“FIFA tumepata taarifa za matukio hayo yanayofanywa chini ya Wizara ya Sheria ya Marekani. FIFA tutaendelea kushirikiana kabisa na uchunguzi unaofanywa na Marekani ambao wanaruhusiwa na sheria za Uswisi, lakini pia ushirikiano utatolewa kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Uswisi (FoJ),” taarifa ya FIFA iliyotolewa Alhamisi hii imesema.

Mei mwaka huu maofisa saba wa FIFA walikamatwa baada ya Marekani kuomba kwa mamlaka za Uswisi, kwani wahusika hao na wengine nje ya FIFA wanatuhumiwa kwamba kwa miongo kadhaa wametumia shirikisho hilo kujihusisha na wizi, utakatishaji wa fedha na rushwa.

Alfredo Hawit, Raisi wa Concacaf, 9kushoto), na Juan Ángel Napout, Raisi wa Conmebol, walitiwa mbaroni jijini Zurich, siku ya Alhamis.
Alfredo Hawit, Raisi wa Concacaf, (kushoto), na Juan Ángel Napout, Raisi wa Conmebol, walitiwa mbaroni jijini Zurich, siku ya Alhamis.

Watu wengine saba walikamatwa katika maeneo tofauti na kufunguliwa mashitaka nchini Marekani, baadhi wakiwa ni watu waliopata kushika nafasi kubwa za umakamu mwenyekiti wa FIFA au urais kwenye mashirikisho ya nchi zao.

Rais wa FIFA, Sepp Blatter aliyetetea kiti chake Mei mwaka huu na anayepanga kung’atuka Februari mwaka huu amefungiwa kujishughulisha na soka kwa siku 90 sambamba na Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), Michel Platini. Uchunguzi juu ya wawili hao kupeana mlungula unaendelea. Platini anawania kugombea urais wa FIFA hiyo Februari mwakani, lakini jina lake limeachwa kusubiri matokeo ya upelelezi huo

FoJ wamesema kwamba watu wawili walikamatwa alfajiri na kwamba wanatuhumiwa kutwaa fedha kwaajili ya kuuza haki za soko kuhusiana na michuanoya soka barani Amerika pamoja na kwenye mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

“Maofisa wawili zaidi wa FIFA wamekamatwa leo Zurich. Wanashikiliwa wakisubiri kupelekwa Marekani. Kwa mujibu wa maombi ya Marekani, wanatuhumiwa kupokea hongo za mamilioni ya dola,” FoJ imesema.

Mamlaka za Uswisi nazo zinachunguza kutumika mlungula katika kupata uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qtar na vyote vinakwenda sambamba na upelelezi huru wa Marekani.

Maofisa waliokamatwa Mei, isipokuwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Marekani, Jeffrey Webb na kiongozi wa zamani wa soka wa Brazil, Jose Maria Marin, walipinga mahakamani kupelekwa Marekani na mashauri yao yanaendelea.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Garry Neville kocha Valencia

Tanzania Sports

PSPF wapeleka huduma mpya ya Bima ya Afya Majira, Mwananchi