in , , , ,

Van Gaal kocha mpya Man United

*Barcelona wamteua Louis Enrique

Hatimaye Louis van Gaal ameteuliwa na kuthibitishwa kuwa kocha mpya wa Manchester United.

Van Gaal (62) ambaye ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Uholanzi amesaini mkataba wa miaka mitatu na Ryan Giggs atakuwa msaidizi wake, akihitimisha kipindi chake cha soka ya kulipwa.
Van Gaal anachukua nafasi iliyoachwa na David Moyes aliyefukuzwa kazi baada ya miezi 10 kutokana na kushindwa kuvaa viatu vya David Moyes.

Mdachi huyu amepata kutwaa ubingwa alipowafundisha Ajax wa Uholanzi, Barcelona wa Hispania, Bayern Munich wa Ujerumani na AZ Alkmaar wa nchini mwake.
Anatarajiwa kuingia Old Trafford baada ya kumaliza mkataba wake kwenye Kombe la Dunia ambako atawaongoza Uholanzi, akiwamo mshambuliaji wa Man U, Robin van Persie.

Amejigamba kwamba amepata kusimamia mechi Old Trafford na anajua palivyo kwa hiyo hana wasiwasi atakapoanza kazi hapo na kwamba anawasoma vyema washabiki wa klabu hiyo aliyosema ni kubwa zaidi duniani.

Amesema kwamba ilikuwa ndoto yake siku zote kufanya kazi na moja ya klabu za Ligi Kuu ya England na ana uhakika kwa ushirikiano na wenzake wataweka historia mpya.
Naibu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward amesema kwamba baada ya zahama ya Moyes, anaamini kuwa amemteua mtu sahihi kwa kazi hiyo kwa sababu historia yake inaonesha mafanikio makubwa.

BARCELONA WAMTEUA LUIS ENRIQUE
20140519-205430-75270957.jpgLouis Enrique

Wakati Manchester United wakifanya uteuzi wa kocha, Barcelona nao waliopoteza taji msimu huu sawa na Man U wamemteua Luis Enrique kuwa kocha wa kikosi chao cha kwanza.
Enrique (44) aliyepewa mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Gerardo Martino ‘Tata’ aliyejiuzulu baada ya kukosa ubingwa, alikuwa kocha wa timu ‘B’ ya Barca tangu 2008 hadi 2011alipokwenda kuwafundisha Celta Vigo mpaka wiki jana.

Barca walishindwa kutetea ubingwa wao kwa kutowafunga Atletico Madrid wikiendi hii kwenye moja ya mechi za mwisho za La Liga na pia walitolewa kwneye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku wakishuhudia Atletico na Real Madrid wakiingia fainali inayochezwa wikiendi ijayo.

Mkurugenzi wa Soka wa Barcelona, Andoni Zubizarreta anadaiwa kumpendekeza Enrique, aliyepata kufundisha Roma ya Italia kuchukua nafasi ya raia huyo wa Argentina.
Martino (51) alichukua nafasi ya hayati Tito Vilanova aliyekuwa na matatizo ya saratani ya koo, akajiuzulu kabla ya kufariki dunia.

Enrique alitarajiwa kuteuliwa kutokana na ukaribu wake na klabu hiyo na jinsi alivyofanya vyema kwenye timu ya pili alipochukua mikoba ya Pep Guardiola.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Rais wa Bolivia asajiliwa kucheza soka

Wane tu wana uhakika Man United