UWANJA wa Taifa utafungwa wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kuufanyia matengenezo, kuzibua mifereji iliyoziba pamoja na kuongeza njia za kumwaga maji.
Hatua hiyo imekuwa ikiwa ni siku moja baada ya pambano la Yanga na Manyema kuvunjika kutokana na uwanja huo kujaa maji. Pia pambano kati ya Taifa Stars na Msumbiji lilishindwa kufanyika kutokana na uwanja kujaa maji.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Tanzania, TFF, Frederick Mwakalebela alisema jana kuwa busara zaidi ni kuufunga uwanja huo na tayari tarifa zimefikishwa Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA.
Tatizo la uwanja kujaa maji tuliliona muda mrefu na wiki tatu zilizopita tuliwataalifu FIFA na tayari wameagiza kutuma fedha wataalamu wawili wa FIFA, Eric Harrison na Joop Van Krimper kutoka Uholanzi walishawasili nchini tangu Machi 17 kwa ajili ya ukaguzi wa uwanja huo, alisema.
Mbali na hao, pia wataalam mbalimbali waliopewa tenda ya kutandaza nyasi bandia Dunia nzia Green Field watakuwa wakizikagua nyasi hizo.
Mwakalebela alisema FIFA walishaongea na waalamu wa hapa Tanzania ambao ni kampuni ya Ekika kwa ajili ya matengenezo hayo na mpaka sasa kampuni hiyo inasubili fedha kutoka FIFA iliianze kufanya kazi hiyo.
Alisema uwanja huo wa taifa bado uko katika garantii ya miaka mitatu kwamba kama kuna matatizo yoyote ndani ya miaka hiyo mkandalasi anatakiwa kurekebisha.
Alisema tatizo la kujaa maji si la hapa Tanzania tu bali hata nchi mbali mbali kama mvua inanyesha lakini kunakuwa na mifeleji ya kukausha maji ambayo katika uwanja wa Taifa imeziba.
Hivi karibuni, Meneja wa zamani wa Uwanja wa Ndani, Mohamed Madenge alisema kuwa kujaa kwa maji kunatokana na kupunguzwa kwa saizi ya mabomba ya kutoa maji ambayo yanatakiwa kuwa na sentimita 45 lakini yamepunguzwa hadi sentimita 30.
nafuraha moyoni mwangu kwa uwanja mpya wa taifa star na pendasana mno asante Mwenyezi Mungu awabariki