SIFA kubwa wanamwagiwa viongozi wa soka la Tanzania. Kuanzia mashabiki wa Afrika kusini Zambia, Kenya, DRC, Rwanda na sehemu mbalimbali Afrika mashariki wanamimina pongezi kwa Ligi Kuu Tanzania. Nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Bernard Morrison ameimwagia sifa Ligi Kuu Tanzania na kudai kuwa imeimarika na kuifanya Taifa Stars kuwa timu yenye wachezaji wazuri.
Tanzania imefuzu mashindano ya AFCON kwamara tatu mfululizo na kuzipiga kumbo nchi kama Ghana ambayo imejaa mastaa wanaocheza soka barani Ulaya na katika Ligi maarufu kama Uholanzi, England,Ufaransa,Ujerumani na kadhalika. Tanzania inasifiwa kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nyumbani, Ligi Kuu na hivyo wamewezesha nchi yao kufuzu mashindano ya AFCON 2025. TANZANIASPOTS inafanya uchambuzi kuhusu swali kuu; Ligi Kuu ni maarufu au bora?
Sifa ya umaarufu Ligi Kuu Tanzania
Ligi Kuu Tanzania ni maarufu nchini Kenya,Uganda,Afrika kusini, Zimbabwe, Malawi, Rwanda, Guinea, Mali,Cameroon, DRC, Somalia, Nigeria na kimsingi kote barani Afrika. Sababu ya kwanza ya kuifanya Ligi Kuu kuwa maarufu ni kutokana na ushiriki wa klabu za Tanzania. Ukitaka timu 10 maarufu barani Afrika huwezi kukosa kutaja zile za ukanda wa Afrika mashariki na moja kwa moja itaangukia Tanzania.
Yanga na Simba ni vilabu vinavyotamba barani Afrika na wachezaji wengi wanatamani kuchezea kalbu hiyo. Kwenye maandalizi ya msimu Yanga walikuwa Afrika kusini ambako walitangaza vema timu yao na Ligi Kuu. Lakini Yanga walikwenda kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa pale Afrika kusini na mbele ya maelfu wa mashabiki wan chi hiyo waliona umahiri wao.
Licha ya Mamelodi Sundowns kupenya katika hatua ile lakini Yanga walionensha kitu kilichowavutia maelfu ya wadau na wanamichezo wa Afrika kusini. Mbali na yao Yanga wametinga fainali ya Kombe la Shirikisho, huku Simba wakiwa wanashiriki na kutetemesha vigogo barani Afrika kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa. Kushiriki mara kwa mara kunaifanya Ligi ya nchi husika kujiongezea umaarufu.
Uwekezaji wa Ligi Kuu
Hakuna ubishi moja ya sababu inayowavutia wachezaji wengi wa kigeni kuja kuchez asoka nchini ni kiwango cha malipo wanachokipata. Vilabu vya Tanzania vyenye uwezo wa kusajili wachezaji wa kigeni vimeongezeka. Miaka ya nyuma timu za Simba na Yanga zilikuwa na uwezo huo, lakini sasa Singida Black Stars, Tabora United, Azam FC, Pamba Jiji, Dodoma Jiji,Namungo fc zinao uwezo wa kuajiri wachezaji wa kigeni. Uwekezaji wa uliofanywa na mdhamini na haki za televisheni zinasaidia kukuza mapato ya timu mbalimbali.
Uwezo wa kutengeneza bajeti ya kuendesha timu umetokana na udhamini uliopo huku kampuni mbalimbali zikivutiwa na suala hilo. Kwa sasa si rahisi kupata taarifa za timu kushindwa kwenda Mkoa wowote kucheza mechi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo baadhi ya timu zilikumbwa na ukata mkubwa hivyo kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji na kuendesha timu. Kwa maana hiyo uwezekaji huo umeinua kiwango cha uendeshaji na uwezo wa Ligi na timu.
Nyota wa AFCON toka Ligi Kuu
Katika mjadala wa ubora lazima tukiri kuwa wachezaji wote wanaoitwa timu ya Taifa ni wale wenye ubora na uwezo mkubwa. Kila mchezaji anayeitwa kwenye timu ya Taifa anakuwa na kitu cha ziada ambacho benchi la ufundi linahitaji. Ligi Kuu Tanzania kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 kulikuwa na mfungaji bora Emmanuel Okwi akiwa na mabao matatu na akagawana tuzo na mwenzake. Okwi wakati huo alikuwa akiichezea Simba. Hata hivyo mabadiliko yalikuja kwenye fainali za mwaka 2023 nchini Ivory Coast ambapo kulikuwa na ongezeko la idadi ya wachezaji wa Ligi Kuu waliocheza AFCON.
Katika hatua ya kufuzu wachezjai kadhaa wa viloabu vya Tanzania wamefuzu na nchi zao. Ukiangalia ushiriki wa wachezaji wa Ligi Kuu katika nchi mbalimbali zilizofuzu utakutana na majina kama nyota wa Yanga, Prince Dube (Zimbabwe), Aziz Ki (Burkina Faso), Khalid Aucho (Uganda), Djiqui Diara (Mali) pamoja na wachezaji wengi wa Taifa Stars. Hii ina maana wachezaji wa kigeni wanaleta ubora wa Ligi Kuu na kuifanya iwe na ushindani ndani na Kimataifa. Kwenye anga za kimataifa nyota hao wametamba na kutajwa hata katika hatua za awali za kuwania tuzo za mwaka za CAF.
Makocha wa Kigeni
Wimbi la makocha wa kigeni limekuwa kubwa na wanakwenda kufundisha timu za pembeni tofauti na miaka ya nyuma ambako wengi walikuja Yanga,Simba au Mtibwa na baadaye Azam. Makocha kutoka Kenya,Uganda,Cameroon, Afrika kusini, Ghana, Zambia, Rwanda, Burundi, na wengineo kutoka bara la Ulaya na Amerika wamekuwa na mchango mkubwa kiufundi na kuwezesha timu kuwa na maarifa ya kutosha. Makocha hao wameleta chachu na ushindani wa kiufundi kuanzia Ligi Kuu na mashindano ya CAF, kwa maana hiyo ushiriki wa mara kwa mara kwa vilabu vya Tanzania na kufanya vizuri vimeifanya Ligi Kuu kuinua ubora wake na kutajwa na CAF kama miongoni mwa Ligi Kumi bora barani Afrika.
Kinara wa Afrika mashariki
Ligi Kuu imekusanya wachezaji wengi wa Afrika mashariki kuanzia Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, DRC pamoja na wengine kutoka Afrika magharibi na kusini. Kwahiyo ni kinara wa kutangaza vipaji na imefanikiwa kuvichukua vipaji vizuri na kuvifikisha kwneye ngazi ya juu. wachezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali wanatamani kuja kucheza Tanzania kwa sababu wanaamini ni sehemu nzuri na jukwaa lao la kutangaza vipaji vyao. Hili ni miongoni mwa mambo yanayoifanya Ligi Kuu kuwa maarufu na yenye ubora.
Comments
Loading…