in , ,

Tyson anarudi ulingoni

mt

BONDIA maarufu wa zamani, Mike ‘Iron’ Tyson anataka kurudi ulingoni.

Anachukua uamuzi huo wakati huu ambapo burudani za michezo karibu yote zimesitishwa kutokana na janga la virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu.

Anarejea ulingoni, unafikiri ni sawa? Nani anaweza kumlaumu? Hata mie nataka kurudi, kadhalika viwanda vinataka kurejea kwenye uzalishaji wa kawaida, wanafunzi warudi shuleni na kwenye michezo watu waanze tena kupata burudani waliyoikosa tangu Machi mwaka huu.

Naam, watu wanataka kurejea maisha ya kawaida, wawe babu au bibi, mama au baba, watoto na wajukuu, wasitake tena kujiweka kwenye kona huku wamevaa barakoa wakionekana kama watu waliojitenga sana na wakati mwingine wakiwa hawatambuliki kutokana na sura zao kuzuiwa na barakoa.

Ama kwa suala la Tyson, haionekani kwamba litakuwa gumzo sana kurejea kwake ulingoni, walau basi halitakuwa suala la gumzo sana kwa muda mrefu bila kujali jinsi anavyojitahidi kuchapa kwa maandishi kwenye simu na kutumia mitandao ya jamii.

Tyson ana umri wa miaka 53 sasa, akikumbukwa kama mtu aliyekuwa na mfano wa miujiza kwenye mikono yake enzi hizo alipokuwa akiwaponda mabondia wenzake kwenye ngumi za uzani wa juu.

Linakumbukwa sana pambano baina yake na Evander Holyfield kwenye ngumi zilizosimamiwa na WBA mwaka ule wa 1997. Leo anataka kurejea ulingoni baada ya kuwa ameweka rekodi kubwa mno kwenye mchezo huo kuliko wengine wengi. Nani atamkamata?

Tangu Machi 1985 hadi Novemba 1986 Tyson alipigana mapambano 28 na hakuna hata moja alilopoteza, akishinda 26 kwa Knock Out (KO), akicheza raundi 52 tu, akivuta umati mkubwa wa watu kuyatazama mapambano yake, lakini yakiisha mapema mno kabla hawajafurahia kile kilichowapeleka kutazama.

Lakini pia kingine kinachogusa ni jinsi wapinzani wake walivyo kwa sasa, wakiwa kama waliogandamizwa au meli zilizopita baada ya kutokwa jasho jingi wakiwa ulingoni enzi hizo. Wapo akina Larry Sims huko Poughkeepsie, Sammy Scaff wa Felt Forum, Steve Zouski kule Nassau Veterans Memorial Coliseum – jamaa waliokuwa imara sana na vifua vipana.

Linakumbukwa pia kwa namna ya pekee pambano lake la awali, ambapo hakuwa na uvumilivu kabisa, likiwa ni dhidi ya Hector Mercedes at the Plaza Convention Center, Albany, New York. Wanaume wawili wakakabiliana vilivyo, Tyson akatupa Makonde 16 yaliyompata barabara katika sekunde 10 tu, Mercedes akaanguka kama mende.

Nakumbuka wakati wa pambano lake dhidi ya Jack Johnson pale kwenye hoteli ya Atlantis, akapigwa na kutupwa kwenye mkanda wa nyuma yake kabla ya kujikusanya na kurejea hali ya kawaida, lakini pia lile pambano lake dhidi ya Donny Long, aliyejulikana pia kama ‘The Master of Disaster’.

Long alikuwa poa ana mwenye haiba nzuri tu na kabla ya pambano akasema; “naweza kutupa Makonde vyema kuliko Tyson. Huu ni ushindi mzuri kuwajulisha wote kwamba Donny Long amerejea.” Lakini ndani ya sekunde 30 akawa amegaragazwa kabisa.

Ikaja Novemba 1986 pale Berbick aliyekuwa bingwa wa WBC ambaye kwa sasa ni mchungaji anayejiita ‘Askari wa Msalaba’ lakini akaja baadaye kutiwa hatiani na mahakama baada ya kushitakiwa kwa kumbaka msichana aliyekuwa akimhudumia binti yake mdogo kabisa. Alikuja kuuliwa kinyama nje ya kanisa na mpwa wake 2006.

Bado kukawa na muda wa kumpiga Michael Spinks ndani ya sekunde 91, lakini ukaja wakati wa mambo kuanza kuanguka. Kukawa na kadhia kubwa kupita kiasi, tabia mbaya kwenye maisha. Ukaja wakati wa kupigwa kwa KO na James Buster Douglas kwenye raundi ya 10, miaka sita baada ya mambo ya Hector Mercedes.

Wakati mbaya ukaendelea kwa Tyson kukamatwa, kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka. Hakuna mengi zaidi mazuri ya kusema juu yake, kwa sababu aliishia kuwa katika hali ngumu, huzuni na kwamba muda wake wa mafanikio ukawa umepita, ikabaki historia.

Kwa hiyo kuna huzuni mbele ya uzuri wa yote aliyofanya mazuri Tyson, na alitakiwa kwa sasa awe mfano mwema na mtu wa kupigiwa mfano na wengine waliokuja nyuma yake, lakini sivyo, ameyaharibu mambo. Akapoteza mengi makubwa aliyofanya katika historia yake, hasa ikizingatiwa kwamba ni mtu aliyekulia katika mazuingira magumu kama mtoto akiwa mwanafunzi wa Cus D’Amato.

Mfikirie huyo Tyson sasa; mtu anayesema anarejea ulingoni kwa ajili ya kupambana katika umri wake mkubwa akiwa bado anafanya mazoezi kwa kuchakaza maguni ya mchanga, akiwa bado anataka sana kupata sifa kama zile za enzi za umaarufu wake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

What has killed Sports in Tanzania

Klabu EPL zinadeka