Tanzania kwa sasa imeanza kuchomoza katika matukio kadhaa ya kimichezo kwa kupitia ushiriki wake na umeisaidia kuzidi kujitangaza kimataifa. Wanamichezo kadhaa wamefanya vizuri na hivyo kuliletea sifa taifa kupitia mafanikio yao. Serikali kwa kutambua umuhimu wa mafanikio ambayo wameyapata wachezaji hao ikaanza mwaka jana utaratibu wa kutoa tuzo kwa ajili ya kuwaheshimisha wanamichezo hao kupitia baraza la michezo Tanzania na tuzo hizo zikabeba jina la tuzo za baraza la michezo.
Mwaka jana raisi wa jamhuri wa muungano ya Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alianzisha utaratibu wa kutoa zawadi kwa wanamichezo wanaofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na fungu hilo lilienda kwa wanamichezo wa michezo tofauti na kwa kiwango Fulani ulisaidia kuongeza hamasa ya wanamichezo hao kufanya vizuri Zaidi. Tulishuhudia kwenye soka vilabu vya Yanga na Simba kufika mali katika mashindano ya soka barani afrika na halikadhalika tumeshuhudia timu ya taifa kufika katika hatua ya kufuzu kushiriki mashindano ya AFCON. Timu ya taifa ya mchezo wa kabaddi ilikuwa mshindi wa pili katika mashindano ya afrika ya mchezo huo. Wachezaji wa michezo ya gofu na tenisi kwa upande wa wanawake halikadhalika walifanya vizuri katika mashindano ya afrika.
Mafanikio ambayo nimeyaeleza hapo juu yanatakiwa yawe endelevu na yazidi kukuwa siku hadi siku na ili yakuwe yanahitaji mkakati wa kitaifa ambao utakuwa ni wa mda mrefu kwa ajili ya kutafuta mafanikio ya mda mrefu. Mkakati huo kwa maoni yangu ugawe michezo kwa kanda za kinchi yaani kanda ya pwani (mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga, lindi na Mtwara ) kanda ya kati(mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Manyara) kanda za juu kusini( Mbeya, Iringa, Songwe, Ruvuma,) , kanda ya ziwa (mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Simiyu, Bukoba) kanda jumuishi
Katika kila kanda tuchague michezo ambayo ya kuipa nguvu maeneo hayo kwani si kila mchezo utakuwa unachezwa nchi nzima. Hii ni kutokana na sababu za kiuchumi, kijiografia na kijamii. Kamati za michezo za mikoa na wilaya zifanye tafiti ndogo juu ya ni michezo gani ambayo ikichezewa katika maeneo yao itakuwa na nguvu na italeta tija kubwa sana kwa taifa. Serikali pia iviagize vyama vya michezo vifanye tathmini kwamba ni mikoa ipi ama kanda zipi ambazo zinaweza kuleta wachezaji ambao watakaofanya vizuri Zaidi hususani wakishiriki mashindano ya kimataifa ili kuiletea sifa nchi katika mashindano ya kimataifa.Matokeo ambayo vyama vitaleta basi visaidiwe nguvu katika maeneo hayo ili vizalishe wachezaji wenye ushindani. Hili jambo linawezakana na ninaweza kutolea mfano mchezo wa riadha kupitia bara la afrika kwa nchi mbili nazo ni:
Kwanza ni nchi jirani ya Kenya katika mkoa wa Rift Valley kuna kabila linalofahamika kama Kalenjin. Kabila hilo lina sifa adhimu ya kutengeneza wanariadha Hodari ambao wameiwakilisha Kenya katika mashindano mbalimbali kimataifa. Tokea miaka ya 1960 wanariadha toka kabila hilo wamekuwa washindi wa mashindano ya riadha yaliyofanyika katika majiji mbalimbali ulimwenguni. Baadhi ya washindi hao ni pamoja na Kipchoge aliyeshinda medali ya dhahabu ndani ya Olimpiki iliyofanyika Mexico City mnamo mwaka 1968 Wilson Kipsang ambaye alishinda mbio za Berlin Marathon za mwaka 2013 na aliweka rekodi dunia ya kukimbia ndani ya masaa 2 dakika 3 na sekunde 23 halikadhalika katika mbio hizo katika 5 bora kulikuwa na wakenya wengine. Denis Kimetto aliyeshinda nafasi ya pili katika mbio za Chicago marathon, wengine ni pamoja na Wilson Kipketer, Daniel Komen na Eliud Kipchoge. Eliud Kipchoge ndio maarufu miongo mwa wanariadha wote toka kabila la Kalenjin la Kenya kwani anachukuliwa kuwa ndio mwanariadha bora wa mda wote wa mbio za barabarani maarufu kama “Marathon”. mafanikio yake yamekuwa ni makubwa sana kwenye mbio hizo kwani amekuwa mshindi mara kadhaa na halikadhalika amevunja rekodi za dunia katika mbio hizo. Wanayansi na watafiti kadhaa wamefanya tafiti juu ya kabila la Kalenjin na wamegundua mambo yafuatayo: kwanza wakalenjin ni Hodari katika mbio kutokana na masuala ya vinasaba(genetics)kwani mababu zao walikuwa wakimbiaji wazuri pili maumbile yao yamejengeka vizuri na kuwaganya kuwa ni wepesi katika masuala ya kukimbia tatu ni mila zao kwamba wakalenjin ni watu ambao wanapenda sana mambo ya kukimbia na ni katika mila zao kuwa na desturi za kukimbia.nne ni kwamba wakalenjin maeneo yao ya kijiografia ni Rafiki kwa masuala ya mazoezi ya kukimbia kwani huwa wanafanya mazoezi kwenye maeneo yenye miinuko na hili huwasaidia wao kujienga vizuri kwenye michezo ya riadha ya kukimbia.
Nchini Ethiopia kuna Kijiji kinachoitwa Bekoji ambacho kipo katika mji wa Oromia ambacho kinasifika kuzalisha wakimbiaji wa mbio ndefu ambao wameshinda medali 16 za olimpiki ndani ya miaka 20 iliyopita. Kijiji hicho kimezalisha wakimbiaji kama vile Kenenisa Bekele, TIrunesh Dibaba, Derartu Tulu na Fatuma Roba. Ukifika Bekoji utakuta uwanja mdogo ambao umebuniwa kwa ajili ya mazoezi ya kukimbia wanariadha pindi wanapotaka kufanya mazoezi. Kijiji hicho kina kocha maarufu ambaye anazalisha wanariadha ambaye anaitwa Sentayehu Eshetu. Kocha huyo anaheshimika sana katika ulimwengu wa riadha na ndiye hakika mgunduzi na mwendelezaji mkubwa wavipaji vya wakimbiaji. Mwanafunzi wake wa kwanza alishinda medali ya Olimpiki iliyofanyika jijini Barcelona mnamo mwaka 1992 na mwaka 2000 jijini Sydney na Fatuma Roba aliyeshinda marathon ya Atlanta ya mwaka 1996. Pia mdogo wa Tirunesh na Kenenisa walishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya ndani ya dunia.
Kusema. hivyo mimi sio mbaguzi wala mkabila ila ni maoni ambayo naona kama yakifanyiwa kazi yataleta tija nchini. Hata hapa kwetu kwenye mchezo wa riadha huko nyuma wanariadha waliowahi kutuletea sifa nchi wengi wao walitokea ukanda wa mikoa ya katikati ya nchi ambapo tulikuwa na wanariadha kama vile: Filbert Bayi, Juma Ikanga’aa na wengineo. Na mpaka sasa mikoa ambayo walitoka magwiji hao wa riadha inafanya vizuri kwenye riadha kuliko michezo mengineo. Ukifika bekoji ukakiangalia kiwanja ambacho kimetengenezwa kwa ajili ya wanariadha kufanya mazoezi ni cha kawaida sana na naamini hata serikali za vijiji vyetu vinaweza kutengeneza. Kwa nini kila Kijiji kiwe na kiwanja cha soka peke yake kwa nini michezo mingine nayo isipate maeneo ya kuchezea hakika ni mda sasa wa wa kutengeneza mkakati mpya wa kimichezo.
Comments
Loading…