Msimu mpya wa soka unaanza England hivi karibuni, japokuwa dirisha la usajili litabaki wazi hadi Oktoba 5, huku wachezaji waliosajiliwa kujiunga na Ligi Kuu ya England (EPL) wanaweza kuwasha moto na kuzipaisha timu zao.
Wiki za mwanzo bila shaka zitakuwa na msisimko, baada ya msimu uliopita kumalizika kimya kimya kutokana na athari za virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu.
Bournemouth walioshuka daraja wamefanikiwa kubaki na Callum Wilson na Joshua King, wakati Norwich walioshuka pia bado wanaweza kuwa na akina Ben Godfrey, Max Aarons, Todd Cantwell na Jamal Lewis.
Watford, nao, wanaweza pia kuanza maisha mapya chini kwenye Championships wakiwa na wakali wao kama Ismaïla Sarr na Gerard Deulofeu. Ivan Toney ameamua kwenda Brentford.
Ama kwa timu zilizobaki EPL, kutakuwapo kazi kubwa, Liverpool wakiwa wameshaanza kuduwazwa tangu mwisho wa msimu kwa kufungwa na Arsenal, ambao walikuja tena kuwafunga wakati wa kufungua pazia la msimu huu kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
Mabingwa hao Liverpool, wanakiri kupitia kwa Jurgen Klopp, kwamba itakuwa ngumu kutetea taji walilowapokonya Manchester City ambao kwa karibuni wamekuwa wakiwania kumsajili nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Chelsea wametangaza kwamba ni msimu wao, lakini Manchester City wanaozidi kuzoeana chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, wanatarajiwa kuwa wakali, kwani wameongeza pia wachezaji wazuri, mmoja mkali sana akiwa ni Bruno Ferndandes.
Tottenham Hotspur wakiwa na ‘The Only One’ Jose Mourinho wataanzaje msimu na kumaliza vipi? Pengine ni msimu wa kuona wakubwa sita wakibadilika.
Comments
Loading…