in , , ,

TOFAUTI KATI YA SIMBA YA LENCHANTRE NA YA PATRICK

Nchi nzima ilikuwa Mwanza. Masikio yetu yaliazimwa miamba, macho na akili zetu zikasafiri kwa njia ya maji mpaka Mwanza.

Ngao ya jamii lilikuwa tukio ambalo lilifanyika Mwanza na kwa kiasi kikubwa kulikuwa na mafanikio makubwa sana hasa hasa kwenye hamasa ya mashabiki kuingia kwa wingi uwanjani.

Simba ndiye mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania. Ubingwa ambao alichukua chini ya Pierre Lenchantre na jana ilikuwa chini ya Patrick Aussems.

Zipi zilikuwa tofauti kati ya Simba ya Pierre Lenchantre na Patrick Ausemms?

Mfumo wa kiuchezaji.

Simba ya Pierre Lenchentre ilikuwa inatumia mfumo wa 3-5-2, mfumo ambao ulikuwa unaleta uwiano mkubwa katika eneo la kuzuia na kushambulia.

Timu ilikuwa inashambulia pamoja kuanzia pembeni mwa uwanja kwa wingbacks na katikati ya uwanja.

Na pia timu ilipokuwa inapoteza mipira ilikuwa na uwezo wa kujizuia kwa pamoja. Hii ilikuwa inaifanya timu ishambulie na kupata magoli mengi na kuzuia magoli.

Lakini Simba ya Patrick Aussems, ilikuwa inatumia mfumo wa 4-3-3 katika mchezo wa jana.

Mfumo ambao ulikuwa na watu wengi eneo la nyuma.

TIMU YENYE SAFU KALI YA USHAMBULIAJI vs TIMU YENYE UWIANO WA KUZUIA NA KUSHAMBULIA.

Simba ya Pierre Lenchantre ilikuwa Simba iliyokuwa inafunga magoli mengi, kuna utofauti sana na Simba hii ya Patrick Aussems ambayo inatumia mfumo wa 4-3-3 mfumo ambao unawatu wengi eneo la nyuma.

Hivo inaonesha Patrick Aussems amejidhatiti kwa kiasi kikubwa katika eneo la nyuma. Hivo Simba ya Patrick Aussems ni Simba ambayo itakuwa inafunga magoli machache kuliko Simba ya Pierre Lenchantre.

UKOMAVU WA SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA.

Simba ya Pierre Lenchantre safu yake ya ushambuliaji ilikuwa imebebwa na watu wawili wakomavu kimaamuzi ( Emmanuel Okwi pamoja na John Bocco).

Kuna kipindi Simba iliwakosa Emmanuel Okwi na John Bocco, washambuliaji waliotumika kuziba nafasi zao hawakuwa na ukomavu kimaamuzi ndani yao kitu kilichosababisha safu yao ya ushambuliaji kuwa butu.

Lakini Simba ya Patrick Aussems ina watu kama Maddie Kagere ambaye ana maamuzi ya kiukomavu na anakuja kuongeza ukubwa wa kikosi upande wa mbele.

Hivyo Simba ya Patrick Aussems itakuwa na mbadala mzuri kwenye safu ya ushambuliaji kama Meddie Kagere, Adam Salama, Mohamed Hussein na Hassan Dilunga

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

TATIZO GARI ALILOPANDA POGBA, DEREVA NI RAIOLA!

Tanzania Sports

TUZO MCHEZAJI BORA ULAYA