Mabadiliko makubwa aliyafanya Hassan Mwakinyo katika mpambano ambao alishinda kwa alama dhidi ya mpinzani wake Tshibangu Kayembe.
Hii imetokana na udhaifu aliouonesha katika pambano lake la mwisho alilopigana pale uwanja wa Uhuru dhidi ya Anael Tinampay.
Kayembe ni bondia namba moja kutoka Kongo na alikuja kupamba wala sio kushiriki.
Ni mzuri sana Tshibangu akifanya mabadiliko kidogo atakuwa bora sana na atatisha barani Afrika.
Mwakinyo ameshinda kwa pointi pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Welter katika kuwania mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF.
Mabondia hao walionekana kukamiana na kushushiana vitasa vikalivikali katika pambano hilo lililofanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar na kuhudhuriwa na wadau wengi.
Wote walikuwa vizuri na mazoezi makubwa yalifanyika juu ya pambano lile.
MABADILIKO KWA MWAKINYO
1. Alijua kufumua ngumi za tumbo ili amlegeze mpinzani
2. Aliweza kutumia muda vizuri katika kuelekea mapunziko
3. Alijiandaa vizuri na mazoezi ya punzi
4. Aliongeza kitu hasa kupiga ngumi inayofumua kidevu
5. Alicheza Boxing kweli
Maelezo yake endelea kusoma hapo chini ili ujue namna gani huyu mtu alifanya kazi kubwa kubadilika.
Licha ya kushinda kwa alama βPointsβ bado haiondoi mabadiliko aliyoyafanya kutoka katika mapambano yake ya mwisho ambayo tuliyaona.
Pambano la mwisho lilikuwa dhidi ya bondia kutoka Ufilipino Anael Tinampay ambapo pia alishinda kwa alama kama alivyofanya siku ya Ijumaa.
Mapungufu yaliyoonekana katika mapambano yaliyopita ni pamoja na kujilinda sana pasipo kupiga ngumi na kuonesha mchezo mzuri( kwa lugha rahisi tunasema alipigana).
Licha ya kushinda dhidi ya Tinampay bado watu hawakuridhika kwa kile alichokionesha hivyo walitamani afanye kingine ili waridhike.
Alichokifanya aliweza kubadilika na kupigana ngumi haswa dhidi ya Kayembe.
Mchezo wake dhidi ya Tinampay haukuwa na utofauti na ule wa bondia ghalli aliyestaafu hivi sasa Floyd Mayweather yaani unapiga ngumi moja unakimbilia Kawe Ununio kisha unapiga ngumi ya pili upo Ubungo na ngumi ya tatu uko Kinondoni Mkwajuni raundi ya kwanza imeisha.
Mchezo huo wengi hawakuupenda na ndio aliotumia Mwakinyo mchezo wake dhidi ya Tinampay.
Mabadiliko aliyoyafanya dhidi ya Kayembe hakumkimbia wala hakuwa anazuia sana alichokifanya alikuwa anamfuata na kurusha makonde mengi ambayo yalimpata.
Kingine ambacho alikifanyia kazi juu ya kupiga tumboni kwa ajiri ya kumlegeza ili aachie uso achape makonde amuangushe.
Kingine alichoongeza alijua kutumia muda wakati zinaelekea kuisha kwa raundi fulani kwenda kupunzika.
Lakini pia alijua kuhesabu vizuri mapigo yake na kugundua kuwa kuna uwezekano mkubwa ameshinda kwa alama nacho kizuri japo ukiwa ugenini inatakiwa umalize mambo mapema matokeo ya ngumi ukiwa ugenini hayana usahihi sana.
Katika mchezo huu wa ngumi kuna aina nyingi za mapambano huku kila bondia alikuwa na alama zake na anapoongelewa lazima utaje sifa yake.
Mfano Mike Tyson, yeye alikuwa anapenda kushambulia sana huku ulinzi ukiwepo japo katika mapambano yote aliyopigana hayafiki matatu aliyozuia sana.
Tyson alikuwa anarusha makonde mazito ya haraka huku akikamilika kila idara katika upande wa ngumu alijizolea umaarufu mkubwa sana.
Mohammad Ali huyu alikuwa anakupiga na maneno yeye alikuwa haogopi kushindiliwa konde ila ukiingia anga zake una kaa chini.
Hao ni baadhi ya mabondia ambao mimi nawapenda ila hata walio wengi pia wanawapenda .
AONGEZE NINI MWAKINYO ?
Hassan Mwakinyo bado ana safari ndefu ya kubadilika na anatakiwa apate walimu wazuri zaidi ya hawa waliopo ili kumjenga zaidi.
Katika sehemu ya kujilinda bado hajajiweka sawa hasa akipata bondia mjanja , kwa mfano pambano aliloshinda dhidi ya Kayembe aliuweka wazi uso wake kwa muda mrefu, yes ni sahihi kumtamanisha lakini kweli unauwezo wa ku-βpunchβΒ haraka mpinzani anaporusha konde lake?
Anavyokwenda kushambulia awe na uhakika na safari yake nyingine anaenda kwa kujisahau hasa anapoona bondia ana mmudu anajisahau hilo abadilishe kidogo.
Licha ya kufauru katika punzi bado anatakiwa azidishe juhudi sana anapokutana na watu wanaoshambulia sana huenda ikawa kiama kwake hivyo aongeze zoezi la punzi.
Ayafaniyie kazi hayo kisha apate pambano lingine la ndani ashinde limjenge baada ya hapo atafute la nje.
Kwa sasa katika uzito wake ni bondia namba moja kwa ubora Tanzania hiyo haina ubishi.
Mwisho ambalo si kwa umuhimu atuwekee mbwembwe anapokuwa na uhakika wa kushinda pambano kama zile za Mohamed Ali.
Comments
Loading…