in

TFF na Soka La Ufukweni

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) linaendelea na harakati zake za kuanzisha soka la ufukweni hapa nchini baada ya kupewa mamlaka hayo na shirikisho la soka Dunia (FIFA)

Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema  hivi sasa kila kitu kinaenda vizuri na tayari baadhi ya watu wameshajitokeza kwa TFF kwa nia ya kuanzisha vilabu vya mchezo huo

Pia katibu huyo anasema kwa kuanzia wao TFF wameona kwanza mchezo huo uanze hapa jijini Dar es salaam kwa majaribio na baadae ndio uende kwenye mikoa mingine ya Pwani kabla ya kuenea kwenye mikoa mingine ya Tanzania

Hivi sasa kuna baadhi ya vilabu vichache ambavyo havipo rasmi vinacheza soka la ufukweni hapa jijini Dar es salaam na TFF ndio linazungumza na vilabu hivyo ili kuona kama wanaweza kuanzia huko

Mwakalebela amesema ili kuweza kuvitambua vilabu hivyo ameomba vijisaili kwa TFF ili viweze kutambulika na kama watafanikiwa basi wanaweza kuanza kuanda mashindano hayo kwa kuanzia kwa vilabu hivyo vichache

Mwisho kabisa Mwakalebela amesema FIFA wamekubali kutoa mafunzo ya kuendesha soka hiyo hapa nchini na ndiomana wameviomba vilabu hivyo kufanya usajili haraka ili waweze kupata mafunzo hayo toka FIFA

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Let`s extend soccer horizon beyond Simba and Yanga

I am seeking input and general advice on how a country such as Tanzania can go about developing capacity so as to be able to send players overseas and be accepted