in , , ,

TETESI ZA USAJILI LEO

Manchester City wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba, 22, ambaye kwa sasa anakipiga Juventus.

City wapo tayari kutoa pauni milioni 45 kumnasa Pogba anayeelezwa kuwa kiungo bora zaidi duniani kwa sasa, wakati huu ambapo kiungo wake, Yaya Toure anaonekana kushuka kiwango na kutopendezwa na hali ya Etihad.

Manchester United wametajwa pia kumuwania mchezaji huyo lakini ameripotiwa akisema kwamba hana nia hata kidogo ya kurudi huko. Klabu nyingine zilizohusishwa naye ni Arsenal na Chelsea.

Mshambuliaji matata wa Palermo, Paulo Dybala, 21, ambaye kitambo sasa amekuwa akihusishwa na kusajiliwa Arsenal, Chelsea au Manchester United anaelekea kuwakatalia wote, kwani kuna maelezo kwamba anakwenda Juventus kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha dili la kujiunga nao.

Tottenham Hotspur wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 12 kumsajili mshambuliaji wa Burnley walioshuka daraja, Danny Ings, 22, kabla ya mkataba wake kumalizika hapo Turf Moor.

Hata hivyo, mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Vijana ya England, tayari amewaambia Spurs kwamba nia yake msimu huu wa kiangazi ni kujiunga na Liverpool licha ya timu yake kumaliza nyuma ya Spurs.

Liverpool wapo tayari kupunguza gharama zao za uendeshaji kwa kumuuza mchezaji wake, Mario Balotelli, 24, licha ya wakala wa Mtaliano huyo, Mino Raiola akisema kwamba ameshazungumza na Liverpool na mteja wake atabaki Anfield, ima faima.

Balotelli alisajiliwa kwa pauni milioni 16 kutoka Milan lakini hajaisaidia klabu yake, anaendelea na utovu wa nidhamu na kila wiki analipwa pauni 80,000 kama mshahara na posho nyingine juu ya hapo, kitu kinachomuudhi kocha Brendan Rodgers , viongozi wengine wa klabu hiyo na wamiliki.

Kocha wa Real Madrid aliyefukuzwa karibuni aliyepata pia kuzifundisha AC Milan, Chelsea, na Paris St-Germain, Carlo Ancelotti atakuwa tayari kuchukua fursa ya kuwafundisha Liverpool iwapo angepewa. Kuna madai kwamba kocha Rodgers atafukuzwa kabla ya msimu ujao.

Manchester United wanasema wapo tayari kuwapa Bayern Munich au Paris St-Germain nyota wao aliyewagharimu pauni milioni 59.7, Angel Di Maria, 27, lakini watatakiwa kulipa karibu kiasi chote cha fedha hiyo.

Bosi wa Inter Milan, Roberto Mancini anatarajiwa kumpigia simu binafsi Yaya Toure ili kujua mpango wake na kulikoni dili la kwenda Italia linaonekana kufifia katika siku za karibuni. Mancini alifanya kazi na Toure alipokuwa kocha wa City. Kocha Manuel Pellegrini amesema kwamba Toure hataondoka klabuni kwake.

Sunderland waliokosa fursa ya kuendelea na kocha wake wa muda, Dick Advocaat wanatarajia kumfuata mwalimu wa Real Sociedad, David Moyes ili awe kocha wao msimu ujao japokuwa pia wanamwangalia Kocha Msaidizi wa Real Madrid, Paul Clement. Moyes alikaririwa majuzi akisema anafurahia soka nchini Hispania hivyo hatarudi England kiangazi hiki.

Derby County wa Ligi Daraja la Kwanza wanataka kuwasajili moja kwa moja mshambuliaji wa Aston Villa, Darren Bent, 31, na Yule wa Hull, Thomas Ince, 23, walio kwa mkopo klabuni hapo, ili wasaidie kuwapandisha daraja baada ya kukwama msimu huu.

West Ham wameendelea kupata mapigo katika kutafuta mrithi wa kocha wao anayeondoka, Sam Allardyce baada ya mtarajiwa wao, kocha wa Marseille, Marcelo Bielsa kuanza mazungumzo ya kuhuisha mkataba wake kwa miaka mingine miwili katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa.

The Hammers wataendelea taratibu kutafuta kocha mwingine ambaye atapewa pauni milioni 25 kwa ajili ya usajili kwa msimu ujao.
Queen Park Rangers (QPR) walioshuka daraja wapo tayari kutoa pauni milioni 2.5 ili wamsajili mshambuliaji wa Liverpool, Rickie Lambert, 33, ikiwa mfungaji wao bora msimu huu uliomalizika, Charlie Austin, 25, ataeleza nia ya kuondoka Loftus Road.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Alexis Sanchez chaguo la washabiki

Ni Blatter tena Fifa