Ni ukweli hiki tunachokiona? Muhimu zaidi, je ni vizuri hili linalotokea? Moja ya mambo ya kuvutia katika mchezo wa soka ni msimu huu ulivyoanza hadi ulipo sasa, na yapo mambo kila kona.
Katika falsafa za Aristotle wa Ugiriki na Hegel wa Ujerumani wote wanajadili juu ya asili ya ukweli. Wote wanautazama ukweli kupitia matukio ya aina mbalimbali ikiwemo vifo. Mchezo wa soka lengo lake ni kushinda kila mechi, ndicho kinachowaleta wachezaj,makocha na mashabiki pamoja. Huo ndio ukweli.
Falsafa za magwiji hao wawili zinaweza kulinganishwa na kile kilichotokea msimu huu 2020/2021 wa Ligi Kuu England. Katika fikra za wanafalsafa wangeweza kujiuliza namna mchezo wenyewe ulivyo, unavyochezwa,unavyokwenda mbele, ni mchezo wa namna gani na kama yote yanayoonekana ni ukweli wa aina yake.
Msimu huu sasa umeingia robo ya pili. Mashabiki wameanza kurejea viwanjani na kuonesha dalili ya kurudi katika hali ya kawaida, kelele nyingi, nyimbo za kutosha,shangwe za kila aina bila kusahau matarajio ya ushindi na suluhu. Mwishowe hitimisho ni kwamba, hadi leo hii EPL mechi 190 zimechezwa kwa kiwango cha juu bila mashabiki viwanjani.
Haikutegemewa kufikia hatua hiyo. Itachukua muda kuamini kile kilichotokea. Ni uzoefu wa aina yake kwa wachezaji,makocha,mashabiki,wadau na viongozi wa vilabu na mataifa mbalimbali barani Ulaya. Wachambuzi wameufananisha msimu huu kama “msimu wa kipekee”, kitu ambacho kimefurahisha na kuelimisha kwa wakati mmoja.
Jurgen Klopp anaweza kuwa kocha aliyesumbuliwa msimu huu, kuona kitu tofauti na mipango yake, ni uzoefu ulioingiza timu nyingi gizani,watangazaji,viongozi wa EPL na watendaji wakuu.
Ninazo fikra zingine kuhusu msimu huu. Je, hiki tunachokiona ndicho ukweli wenyewe? Kuzuia timu zingine ambazo zilijivunia umwamba wao, je kumezalisha usawa na kuwapa kiwango bora timu zingine?
Kila msimu unakuwa na mipango inayotakiwa kufanyiwa kazi. Kuanzia wafanyabiasha wa kimataifa,masoko ya hisa,wataalamu na kadhalika hali ambayo inachangia ushindani na kuona timu inapata wakati mgumu kumaliza ligi mbele ya wenzake 37. Pengine kwa miezi michache, kumeibuka dhana nyingine kwenye mchezo wa soka.
Mambo ya kukumbuka ni umoja uliojitokeza. Umbali kutoka Tottenham waliopo nafasi ya kwanza hadi Wolves wanaoshika nafasi 7 ni pointi 4. Baada ya mechi 10 msimu uliopita kulikuwa na tofauti ya pointi 15 kati ya timu inayoongoza Ligi na ile iliyoko nafasi ya 7. Msimu wa nyuma zaidi yaani 2018/2019 kulikuwa na tofauti ya pointi 7, na ule wa 2017/2018 ilikuwepo tofauti ya pointi 12 baina ya nafasi za timu ya kwanza na ile ya 7.
West Ham na Southampton wamekuwa na mwanzo mzuri kuliko timu za Manchester City na Manchester United. Tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa nayo imekuwa ya kushangaza kuliko msimu uliopita.
Pengine chanzo cha hayo yote ni kukosekana mashabiki viwanjani mwa timu kubwa. Lakini, inawezekana hoja hiyo ikapingwa kuwa chanzo cha hayo yote. Kila mmoja anapenda kutoa mawazo yake yakizingatiwa juu ya taharuki iliyotokea msimu huu. Tafrani zilizotokea na jinsi zilivyonufaisha baadhi ya timu,matarajio,uimara wa vikosi na uwezo wao.
Jambo la kukumbukwa zaidi ni mzunguko wa 10 ambao ulikuwa na matokeo ya kushangaza. Timu zilirejesha uhodari wao katika mchezo. Inakuwa rahisi kupanda na kushuka na kupata mtiririko wa viwango. EPL imelinda kasi na viwango,ufungaji wa mabao,jitihada,makosa ya wachezaji na ulinzi kubomoka.
Wakati Chelsea walipomenyana na Tottenham walitengeneza mechi kabambe usiku ule. Ilikuwa mechi kali yenye kila aina ya ufundi, kasi, ujuzi, uhodari, ushindani na hata matokeo yalipokuwa suluhu lakini mchezo wenyewe ulisisimua. Kiwango walichoonesha kilipungikiwa kitu kimoja tu; mashabiki viwanjani. Ulikuwa mchezo ambao mashabiki wangesema hakika wamelipia viingilio sahihi na wangetaka kuongeza viingilio sababu ya kiwango kilichooneshwa jumapili iliyopita.
Lakini hilo laweza kusahaulika kwani matokeo ya suluhu kila mara yapo viwanjani kama kawaida. Siku moja kabla ya Chelsea na Tottenham kumenyana, kulikuwa na mechi nyingine kati ya Liverpool na Brighton, ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 1-1. Ilikuwa mechi ambayo ingewavutia mashabiki wahafidhina kwa jinsi ilivyokuwa.
Hiki si kitu cha kuchukulia mzaha. Kumekuwa na mapendekezo kwenye michezo mingine, uoneshaji wa Televisheni,mpangilio wa ratiba vimekuwa na mchango wa hali ya viwango vya timu EPL. Ushuhuda mojawapo ni msimu huu jinsi wachezaji wanavyotaka kucheza, wanavyojihamasisha, ari ya ushindani ni mambo yanayovutia.
Uchambuzi wa TanzaniaSports unabainisha kuwa kiwango kilichooneshwa na timu za EPL kimechangia kasi ya upachikaji mabao ambapo kumekuwa na wastani wa kufunga mabao 2.84 zaidi ya wastani ule wa msimu uliopita wa 2.72 uliokuwa umejaza mashabiki viwanjani. Takwimu zinaonesha kuna wastani wa mashuti 29 kuelekea langoni kila mchezo wa EPL, ambazo ni takwimu za juu zaidi kiujumla.
Kwa wachezaji na makocha kumekuwa na suala la ufanyaji kazi kulingana na mfululizo wa ratiba. Hilobila kutaja hofu ya Jurgen Klopp juu ya kubanwa na ratiba ya EPL kutokana na majeraha wanayopata wachezaji wake.
TanzaniaSports imebaini kuwa zipo timu zimecheza mechi nyingi kuliko zingine msimu huu. Kwa mfano zipo timu zinazocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool, Manchester United, Manchester City na Chelsea. Hii inaonesha kuwa malalamiko ya Jurgen Klopp kubanwa na ratiba ya mechi nyingi yana mantiki.
Tangu kuanza msimu huu Manchester United wamecheza mechi kila baada ya siku 4.6 kulinganisha na msimu uliopita katika hatua waliyofikia ambako walicheza mechi 5.6 kila siku. Chelsea wenyewe walicheza kila baada ya siku 4.5, ikiwa ni tofauti na msimu uliopita ambako walicheza kila baadaya siku 5.
Kiuhalisia Liverpool haijachza mechi nyingi msimu huu, kwani imecheza mechi kila baada ya siku 5. Liverpool pia wamecheza mechi chache, 9, wakati ,an City wamecheza mechi 14, Chelsea wamecheza mechi 13 na Man United wamecheza mechi 14.
Namba zisitumike kuzimisha hoja ya Klopp kwa sababu inaumuumiza na kusababisha mawazo mengi kwa kuwa wachezaji wake wanatakiwa pia timu za taifa. Kwa namna yoyoteile matatizo ya uchovu lazima yawakumbe wachezaji wake kwa kila mechi wanayocheza. Ndio maana kuna mjadala juu ya kuongeza wachezaji wa kubadilisha (Sub) wawe wanne au watno).
Kila mwanamichezo amekuwa akisumbuliwa na hali fulani tangu kipindi cha kukaa karantini. Mfumo wa mazoezi na ratiba vyote vilibadilika na kuwaathiri wachezaji wengi.
Wacheaji wamepimwa maambukizo ya virusi vya corona na baadhi kukutwa navyo. Baadhi ya timu zimekumbwa na majeruhi. Ukiongeza na kila mmoja kujaribu kukabiliana na hali mpya ya maisha imechangia kuwa na msongo wa mawazo. Tutajionea zaidi matokeo ya hali hiyo kadiri msimu unavyoenda mbele.
Kwa sasa inaonekana kama vile mambo yanarejea katika hali ya kawaida. Kukosa muda wa kutosha kufanya mazoezi umewaathiri makocha wengi, pengine ndicho walichogundua na kutumia mifumo ambayo iliwaletea matokeo mabaya. Mmojawapo ni Pep Guardiola ambaye anajali suala la kuimarisha umakini wa timu yake. Mchezo wa soka una maajabu yake kila siku.
Mambo yanayoweza kutokea ni kwamba kutakuwa na faida ya kusubiri muda mrefu hadi kucheza mchezo mmoja. Ukubwa wa kusubiri unaimarisha vikosi vya timu na kuwapa nafasi wachezaji kuimarika. Pia unaongeza nguvu miongoni mwa wachezaji na kama ilivyo desturi hali itakuwa imebadilika na kutakuwa na kufurahia mchezo wa soka.
Comments
Loading…