Shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka ulimwenguni ambapo TANZANIA ipo katika nafasi ya 97 kwa ubora wa soka ulimwenguni.
Viwango hivyo ni vya mwezi JUNE hadi JULAI ambapo TANZANIA awali ilikuwa katika nafasi ya 109 ulimwenguni.
Wakati huohuo IVORY COAST imeipiku CAMEROUN kwa kuwa timu ya kwanza Afrika kwa ubora wa viwango vya soka barani Africa
Afisa habari wa TFF – Floriani Kaijage amesema Ubora wa viwango hivyo umepanda unatokana na michezo ya kirafiki iliyocheza timu ya taifa (Taifa Stars) mbapo ilicheza na NEW ZEALAND na kuifunga magoli MAWILI kwa MOJA.
Mchezo huo ulichezwa June tatu kwenye dimba la Taifa na Taifa Stars ilipata ushindi huo kwa magoli ya Jery Tegete na Mwinyi Kazimoto
Akizungumzia kupanda kwa Tanzania kwa ubora wa soka Duniani kwa nafasi 12 kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo amesema ni hatua nzuri kwa soka la Tanzania
Maximo anasema si Kazi ndogo hata kidogo kufikia nafasi za chini ya mia moja ila sio kulilia kupanda katika ubora wa FIFA pia inahitajika kuimalisha soka letu
Kocha huyo amesema kitu kingine kitakachosaidia kukuza soka la Tanzania ni kwa wachezaji wake wengi kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi maana wakirudi watalisaidia taifa na kuleta changamoto kwa wenzao
Pia amepongeza wachezaji watatu wa timu ya taifa kwenda kujaribu bahati ya kucheza soka la kulipwa njee ya nchi, wachezaji hao ni Henry Josep alieenda nchini Norway, Nadir Haroub (Canavaro) na Nizar Khalfan wanaotarajiwa kwenda Canada kufanya majaribio ya kucheza la kulipwa
Pongezi kwa Tanzania kupanda katika chati ya ubora wa soka duniani.Hatua hii iwape changamoto zaidi wachezaji wa Tanzania kufanya jitihata za kwenda kucheza soka Ulaya na si Uarabuni.Zama za Usimba na Uyanga zimekwisha,tulifikirie Taifa letu zaidi.Tuige mfano wa Ivory Coast ambayo katika miaka ya mwishoni mwa 1990 ilikuwa ikimtegemea mchezaji mmoja tu aliyekuwa akicheza Ulaya,Ibrahim Bakayoko.Lakini wakati huohuo walikuwa wanaandaa mazingira ya kukuza vipaji vipya na kuviuza Ulaya.Matunda yake ndio akina Drogba,Kalou,Eboue na wengineo ambao ukiwakusanya wote,unaweza kuunda vikosi hata vitatu vya timu ya taifa ya Ivory Coast vya wachezaji wanaocheza nje ya nchi pekee,hususan Barani Ulaya! TFF wafanyieni kazi akina Lembele Jerome,Hamid Mao,Faraj Hussien,Kulwa Greyson,Razack Halfan n.k. si Akina Ngassa tena! Wapeni sapoti TSA na wenzake.
Shirikisho la soka Tanzania liweke mfumo utakaowapa urahisi wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kutafuta bahati ya kucheza soka nje(sizungumzii Uarabuni).Nazungumzia zaidi mfumo rahisi wa masiliano kati yake na wachezaji wenyewe pamoja na klabu wanazofanyia majaribio huko nje na pia Klabu walizokuwa wanazichezea awali hapa nchini .Suala hili liwahusishe wachezaji wote hata wale walioondoka kimyakimya bila taarifa kwa shirikisho hilo kwani wakifanikiwa ni faraja na hesima kwa Taifa.Pia litapunguza uwezekano wa wachezaji wa Tanzania kubadili Uraia kama alivyofanya Athuman Machupa kutokana na mizengwe ya TFF eti tu kwa sababu shikisho hilo halina taarifa nao.Tenga na wenzako changamoto hiyoo!