in , , ,

Tanzania 2-0 Botswana

Mambo manne tuliyonjifunza

Timu ya Tanzania, taifa stars chini ya mwalimu mpya Salumu Mayanga wamefanimiwa kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila dhidi ya Botswana kwenye mechi ya kirafiki.

Tanzania ambao ndiyo walikuwa wenyeji kwenye mchezo huo, ili wachukua dakika mbili tu za kipindi cha kwanza kupata goli lililofungwa na nyota wa Genk Mbwana Samatta.

Kwa muda mwingi wa mchezo, stars walionekana kuwazidi Botswana karibu kila idara uwanjani na walifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo hawa kuzitumia vizuri huku Samatta na Msuva wakikosa nafasi mbili za wazi.
Wakati mpira ukielekea kumalizika, Samatta aliwatungua tena Wabotswana hao kwa mpira wa adhabu ndogo ambao ulizama moja kwa moja.

Makala hii inakuletea mambo manne tuliyojifunza Tanzania na Botswana.

1. Kuna kazi kubwa ya stars kufuzu CHAN mwakani Kenya
Kikosi cha taifa stars chini ya Mayanga, kwa asilimia kubwa bado kina tegemea nguvu ya Mbwana Samatta kwenye eneo la ushambuliaji hivyo kukosekana kwake Samatta kwenye CHAN kuna uwezekano wakukipa wakati mgumu kikosi cha stars kufuzu mbele ya timu ngumu kama Rwanda na Uganda.

2.Kombinesheni ya Banda na Nyoni itatugharimu kwenye mechi za mashindano.
Nyota hao wameonekana kutokuelewana kwa muda mwingi wa mchezo kwa kuingiliana majukumu uwanjani, licha ya Botswana kufanya mashambulizi machache lakini walifanikiwa kupenya ngome kirahisi kilicho waangusha ni umaliziaji mbovu, nafasi ya beki wa Mtibwa Salim Mbonde ni kubwa ndani ya kikosi cha Mayanga, anastahili kuanza badala ya Nyoni.

3.Mbwana Samatta ameonesha utofauti wake na wengine kikosini.
Ili kupiga hatua kisoka nchini inabidi idadi ya wachezaji wanao sakata kabumbu nje ya nchini iongezeke, katika mchezo dhidi ya Botswana tumeona utofauti wa Samatta na wengine kuanzia kwenye kupokea mipira, kutengeneza nafasi na kutumia nafasi vizuri.
4.Botswana haikuwa timu ya kuipa upinzani mkubwa taifa stars.

Kama baadhi ya wachezaji wa Tanzania wangetumia vizuri nafasi zao, kulikuwa na uwezekano wa kuibuka na ushindi wa zaidi ya goli 5 Wabotswana wali zidiwa na kuaonekana ni timu ya kawaida ambayo ilishindwa kuleta upinzani mkubwa kwa stars.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

WAO NA SISI NI KAMA HESABU ZA KUJUMLISHA NA KUTOA

Tanzania Sports

Wenger anabaki Arsenal